ad

ad

WASANII SERENGETI FIESTA 2014 NDANI YA BREEZE FM



Wasanii wanaotarajiwa kufanya shoo kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 leo wakisubiria kufanyiwa mahojiano ndani ya kituo cha Redio cha Breeze FM cha mjini Tanga mapema hii.



Msanii kutoka Kundi la Yamoto Band, Dogo Aslay akizungumzia namna watakavyotoa burudani kwa mara ya kwanza mjini Tanga katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.

Nay wa Mitego akizungumzia namna atakavyoendeleza historia ya kuwakalisha wenzake leo usiku kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mo Music akiwapanga wakazi wa Tanga ili waelekee katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga tayari kwa kumshuhudia akifanya makamuzi kwa mara ya kwanza mjini hapo.


Chege naye hakuwa nyuma kuwakaribisha wakazi wa Tanga ili waweze kuhudhuria kwa wingi kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 tayari kwa kujionea staili mpya ya wimbo wake wa Wauwe.

 Mwanadada Rachel kutoka THT akieleza namna atakavyowakosha na nyimbo zake za mahaba wakazi wa Tanga.



Ommy Dimpoz akiimba moja ya kipande cha wimbo wake mpya wa Ndakushima wakati wa mahojiano mafupi juu ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 mapema leo kwenye kituo cha Breeze FM mjini Tanga.

Vijana wanaounda Kundi la Yamoto Band wakiimba kwa pamoja ndani ya Breeze FM.

PICHA NA 2JIACHIE, TANGA

No comments

Powered by Blogger.