VANESSA, JUX YADAIWA NI WAPENZI...JIONEE WAKIFANYA YAO
Stori: Musa Mateja aliyekuwa Tanga
MBONGO-Fleva anayefanya poa na ngoma yake ya Nitasubiri, Juma Mussa ‘Jux’ na staa mwenzake ambaye ana kofia nyingine ya utangazaji, Vanessa Mdee ‘V-Money’ wanadaiwa kuwa ni wapenzi, Risasi Jumatano limeinyaka.
Juma Mussa ‘Jux’ akiwa na Vanessa Mdee ‘V-Money’ wanaodaiwa kuwa ni awapenzi.
Madai ya wawili hao kuhusishwa kimapenzi yameendelea kujidhihirisha
siku hadi siku na zaidi ni hivi karibuni walipokutana kwenye ziara ya
Serengeti Fiesta 2014 mkoani Kagera na Tanga, ambapo muda mwingi
walionekana kugandana kama luba hadi wenzao kudai kuwa walikuwa hata
wakilala chumba kimoja hotelini.Katika kuwafuatilia, mwanahabari wetu alifanikiwa kupata baadhi ya picha za matukio yao yaliyoonesha michakato na harakati zao za kimalovee zinavyokuwa siku zote.
Wakiteta jambo.
Jux na Vanessa, wakiwa mkoani humo walionekana muda mwingi wakiwa
pamoja kwenye gari walipokuwa wakienda kumuona Babu Njenje na wakati
wakiwa wanaelekea Uwanja wa Mkwakwani kwenye shoo.Hata baada ya Jux kushuka stejini, alionekana akiwa amekaa ‘very close’ na Vanessa huku wakiwa kwenye mazungumzo yaliyodaiwa ni ya kimahaba niue.
Wakiwa pamoja kama kumbikumbi.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuzungumza na Jux juu ya uhusiano
wao, lakini jamaa huyo alimchomolea kwa kusema kwamba hayuko tayari
kuzungumzia ishu hiyo kwani Vanessa ni mshikaji wake tu na hakuna kibaya
juu yao zaidi wanafanya kazi pamoja tu.“Kiukweli sihitaji kuzungumza lolote juu yangu na Vanessa ila ni mwanamuziki mwenzangu hivyo tunafanya kazi pamoja,” alisema Jux.Vanessa kwa upande wake alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alimtaka mwandishi wetu ‘kuipotezea’ habari hiyo kwani si muhimu kwa sasa.

Post a Comment