ad

ad

VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 10


Wakati huo muda nao ulikuwa umekwenda sana, hakutaka kujilaza kwa kuhofia kumkuta kama aliyokutana nayo kwa Stella alipojikuta akirudi nyumbani usiku mkubwa kitu ambacho kingeanza kuwatia wasiwasi wazazi wake pia hata kwa mpenzi wake Betty.
  Muda wote aliokuwa amejilaza pembeni ya Diana, mwenzake alikuwa amejilaza akionesha si wa kuamka muda ule kutokana na kuonekana amechoka sana.
Ilibidi amuamshe kwa kumwita huku akimtikisa.
“Diana.”

“Bon niache nimechoka,” Diana alijikuta akichanganya madawa kwa kufikiri yupo na mpenzi wake wa siku zote Bon, lakini hiyo haikumshtua Shaka aliendelea kumuamsha.
“Muda umekwenda sana Diana amka tuondoke.”
“Bon, imeanza lini kuamshana kuwa muda umekwenda au leo una mwanamke mwingine?”
“Diana mimi siyo Bon,” Shaka alisema baada ya kuona Diana anachanganya madawa.
Kauli ile ilimfanya afumbue macho na kumkuta ni Shaka, alishtuka na kumuuliza:
“Eti Shaka nimekuita nani?”
“Bon.”
“Ooh! Sorry Shaka,” Diana alisema kwa aibu.
“Samahani ya nini?”
“Kukuita Bon.”
“Kwani Bon ndiye nani?”
“Aa..aah! Wacha tu,” Diana alionesha uso wa taharuki.
“Au ndiyo shemeji?”
“Hakuna ni mdogo wangu hupenda kunisumbua ninapokuwa nimelala.”
“Mmh! Sawa,” Shaka alijibu kwa sauti ya chini.
“Jamani Shaka usinifikirie vibaya.”
“Kuhusu nini Diana mbona unajishtukia, nimekuamsha ili nikueleze tuondoke na si kubishana.”
“Lakini naomba usinielewe vibaya, nina imani utajua tu nina mwanaume mwingine.”
“Diana kipi cha ajabu sijakukuta na usichana hivyo wala lisikuumize kichwa, la kawaida, la muhimu nimekuamsha ili tuondoke nitachelewa nyumbani si unajua nimeondoka bila kuaga.”
“Sawa, lakini naomba kwanza uamini sina mwanaume anayeitwa Bon.”
“Ila?”
“Sina kabisa mwanaume kwa sasa, nilitaka niwe na wewe lakini Stella kaniwahi.”
“Kwa hiyo?”
“Basi tuache,” Diana hakuwa na jibu baada ya kuchanganya madawa na kujiuliza siku akiwa na Bon na kumtaja Shaka sijui itakuwaje kutokana na Bon kuwa na wivu kama dume la mbwa.
Baada ya kwenda kuoga kwa pamoja walirudi kuvaa nguo na kutoka huku Diana akimpa Shaka elfu hamsini japo alipanga kumpa elfu kumi kwa kujua atampaka shombo. Lakini alichokutana nacho na kosa la kuchanganya madawa alitoa elfu hamsini bila kupenda katika laki moja aliyopewa na bwana yake Bon ambaye pamoja na kuwa mtu mzima kidogo lakini hakuwa mtundu kama Shaka.
Hakujua utundu ule aliongezewa na Betty na kumfanya Shaka awe moto mkali kutokana na uwezo wake wa damu changa na utundu mdogo alioongezewa.
“Shaka lakini naomba usinielewe vibaya,” bado Diana aliendelea kujitetea kwa kuhofia Shaka kumtema mapema.
“Sikiliza Diana wewe si mke wangu hata kama yupo Bon siwezi kumkasirikia, pengine Bon ndiye anayetufanya tupendeze. Basi wewe kuwa na amani moyoni mwako,” Shaka alimtoa Diana wasiwasi.
“Sawa nimekuelewa.”
Diana alimkodia teksi Shaka mpaka kwao, alipofika waliteremka pamoja na kumsindikiza kidogo, walipofika kwenye uchochoro Diana alimweleza Shaka:
“Shaka naomba siri asijue Stella, lazima tutakorofishana anakupenda sana.”
“Diana hivi mnaniona mtoto mdogo sana?” Shaka alimuuliza huku amemkazia macho.
“Hapana Shaka huenda akakudodosa na wewe ukajisahau.”
“Siwezi labda wewe umwambie.”
“Siwezi, Shaka tutaonana kesho shule.”
“Ila acha kupagawa tukifika kila mtu ajifanye hamjui mwenzake siyo kujifanya unanijua sana nitakutoa  nishai.”
“Siwezi Shaka namheshimu sana Stella.”
“Mbona umekula raha zake?”
“Uzalendo ulinishinda.”
“Haya, siku njema.”
“Bai Shaka.”
“Bai Ste..ooh! Sorry Diana.”
“Shaka najua unalipa kisasi cha kukutajia Bon.”
“Walaa, ulimi hauna mfupa tu, lakini sina mawazo hayo.”
“Haya, mimi nifanyeje na nimeishalikoroga mwenyewe.”
“Walaaa usiwe mnyonge, ili kujua sina hata moja, siku utakayoniita utajua kweli ninayo au sina.”
“Nitashukuru sana Shaka.”
“Haya wahi mama.”
“Asante....mmmwa.”
Diana alifurahishwa na maneno ya Shaka na kumbusu kisha alikimbilia kwenye gari na kumwacha Shaka akienda kwao huku akishukuru siku ile Betty kutokuwepo maeneo yale alimueleza angerudi usiku na kukubaliana kuonana siku ya pili. Kutokana na kuchoka sana alishukuru  kutokuwepo kwani lazima angetaka mchezo angechemka.
                                                    ***
Siku ya Jumatatu Shaka alikwenda shuleni akiwa na wasiwasi wa kugombana na kipenzi chake Stella kwa kuhofia kujua uhusiano wake na shoga yake Diana.  Lakini ilikuwa tofauti hata alipokutana na Stella akiwa ameongozana na Diana hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kumwita Shaka shemeji.
“Za wikiendi mpenzi?” Stella alijishaua mbele ya mpenzi wake bila kujua jana yake shoga yake katia mkono kwenye kapu lake la burudani.
“Nzuri.”
“Nilikuwa na mzuka na wewe ile mbaya sema tu nilikwenda shamba na mama.”
“Siku si zipo.”
“Yaani nilikasirika kidogo nipasuke baada ya kuvimba kwa hasira, tena ndiyo nilikuwa najiandaa kuja kwenu mama akaniita eti nimsindikize shamba.”
“Pole mpenzi,” Shaka alisema huku akimshukuru mama Stella kuepusha shari.
“Shaka leo lazima unipe raha nilizozikosa jana lazima unipe.”
“Hakuna tatizo mpenzi.”
Kengele ya mstarini iliwakatisha mazungumzo.
“Shaka tutazungumza mapumziko,” Stella alisema huku akimpatia Shaka elfu kumi ya matumizi.
Shaka alipokea na kukimbilia mstarini na kumuacha Stella akimsindikiza kwa macho na kujitapa kwa shoga yake:
“Yaani sema tu bado tunasoma, tungekuwa kidato cha sita, baada ya mtihani angenioa hata chuo nisingeenda.”
“Shoga acha kuchanganyikiwa.”
“Lazima nichanganyikiwe  mara ngapi nimeteswa na Twalipo, ni wewe uliyekuwa ukinipa sifa za Bon kukuliza kilio cha mbwa mwizi mwenzio nilikuwa naumia ile mbaya lakini sikuwa na jinsi. Lakini toka nilipokutana na Shaka, kweli udogo wa mchi wa kutwangia viungo vya pilau lakini ndio unaoleta harufu nzuri ya chakula.”
“Sawa lakini unachanganyikiwa vibaya kila mtu atajua Shaka mpenzi wako na kukudharau na kukuona umepotea njia kwa kuwakataa wakina Steve mwenye mishiko ya haja.”
“Steve wa nini, kwanza nasikia umeshadondoka na Steve kwa hiyo ulitaka tuchangie mwanaume?”
“Wewe!  Umejuaje?”
“Japo ulifanya siri lakini kila kitu chako kipo hapa mkononi.”
“Mmh! Si alijipendekeza siku ya kwanza kukutana naye alinipa laki tatu niziache nimerogwa.”
“Basi mimi kwa Shaka nataka penzi si pesa, huyo Steve aliishawahi niahidi milioni kama nitamvulia nguo yangu ya ndani siku moja. Lakini nilimwambia sina dhiki ya fedha wala mimi si dada poa.”
“Basi shoga yanatosha, tuwahi mstarini,” Diana alibadili mada baada ya kuona amechokoza nyuki na mbio hana.
“Bado hayajatosha, tena nina mpango wa kujitangaza kuwa Shaka ni mchumba wangu ili wasio na haya wamkome.”
“Stellaaa! Unataka ufukuzwe shule.”
“Wana ubavu huo, ehe! Nilitaka kusahau nasikia Steve anatembea na mwalimu Monica.”
”Muongo!”
“Wala sishangai kwa yule mwalimu anapenda sana usister du.”
“Mmh! Kwa hiyo mke mwenzangu?”
“Lakini Diana wewe si umesema Bon anakupa kila kitu?”
“Ndiyo.”
“Sasa kwa nini usitulie naye kuliko kurukaruka ona mnavyochanganywa na mwanaume mmoja. Unafikiri Steve ana mpenzi mmoja hapa shuleni? Acha tamaa mtoto wa kike tulia na mmoja!”
“Dada wewee! Alijipendekeza na vijihela vyake niviache nimerogwa?”
“Ulijipendekeza mbona bado nasikia unakwenda naye kila siku.”
“Shoga, ukimchunguza sana bata humli.”
“Nimekuelewa tuwahi mstarini.”
                                                         ***
Jioni ya siku ile Stella hakuwa na hamu na Shaka kwani alitaka apumzike angalau kwa siku mbili ndipo alianzishe tena. Lakini ilikuwa tofauti na shoga yake Diana ambaye alitamani mchezo wa marudiano.
 Pamoja na kupata kipigo cha pweza bado aliamini Shaka alibahatisha. Lakini ukabaji wa Stella wa kutompa nafasi Shaka ulimnyima raha alikosa hata nafasi ya kutia neno. Alipanga kama atamkosa siku za kawaida basi wikiendi kama kawaida atamzukia kwao.
 Stella alimkodia Shaka Bajaj huku akimweleza dereva.
“Kaka hakikisha unamshushia mlangoni kwao.”
“Hakuna tatizo.”
“Bai my husband,” Stella alimuaga Shaka kwa kumbusu mbele ya Diana ambaye aliangalia pembeni kwa wivu.
“Bai my wife,” Shaka naye alimbusu na kumkumbatia Stella huku akimminya jicho Diana.
Dereva aliondoa Bajaj na kuwaacha Stella na Diana wakimsindikiza kwa macho.
“Dogo vipi?” dereva wa Bajaj alimsemesha Shaka.
“Poa bro.”
“Yule demu mkaliii, wako?”
“Kwani vipi?”
“Naona kama maigizo vile hamuendani.”
“Elewa ulivyoelewa.”
“Au shemeji yako?”
“Bhana eeh, sipo mahakamani, awe asiwe demu wangu wewe unapungukiwa na nini?” Shaka alikuwa mkali kidogo.
“Basi dogo yameisha, lakini kama kweli wee mkali.”
“Haikuhusu.”
                                                       ***
Shaka akiwa anaelekea nyumbani kwao baada ya kushuka kwenye Bajaj alishtuliwa kwa sauti iliyokuwa ikimwita nyuma:
“Shaaaka..Shaaaka.”
 Shaka aligeuka kuangalia nani anayemwita, alikuta ni shoga wa Betty.
“Aah! Da’ Edna shikamoo.”
“Asante, za shule?”
“Nzuri tu.”
“Shaka una kazi gani ukifika nyumbani?”
“Mmh! Sina ila Betty aliniambia nikitoka shule niende kwake.”
“Sasa ni hivi nilikuwa na shida na wewe mara moja.”
“Shida gani?”
“Nitakwambia kabadili nguo basi.”
“Kwa hiyo nije kwako?”
“Mmh! Fanya hivi,” Edna aliweka kidole mdomoni kutafuta neno na kumfanya Shaka amtazame usoni na kumuuliza.
“Kwani shida ni kubwa?” Shaka aliuliza.
“Fanya hi..hi..vi....”
“Shaaakaaaa.”
Sauti ya Betty ilikatisha mazungumzo, walipogeuka walimuona akija akiwa amependeza kimtoko.
“Shaka akikuuliza usimwambie tulichozungumza.”
“Poa.”
“Diana vipi unazungumza nini na mpenzi wangu?” Betty aliuliza huku akisogea walipokuwa wamesimama
“Jamani Betty nizungumze nini na Shaka?” Diana alijibalaguza.
“Inawezekana umeanza kumzengea, oho! Tutatoana meno.”
“Shoga mbona mi namchukulia Shaka kama mdogo wangu tu.”
“Shaka unazungumza nini na Diana?” Betty alimkazia macho Shaka.
“Betty kwa nini umeniuliza swali hilo?”
“Shaka nataka jibu siyo swali juu ya swali,” Betty alisema kwa ukali.
“Au kwa vile mi mdogo ndo unanikosea heshima mbele ya rafiki yako, yaani unaniuliza kama mtoto mdogo?” Shaka naye aligeuka mbogo.
“Siyo hivyo Shaka siku hizi mashoga hatuaminiani, naweza kumuamini akanigeuzia kibao.”
“Kwa hiyo mi nimekuwa baba huruma wa mtaa siyo?”
“Hapana shaka nilikuwa na wasiwasi tu,” Betty ilibidi awe mpole.
“Kwa hiyo ndiyo kazi yenu kuchukuliana wanaume?”
“Walaa, lakini siku zote nyuki mkali kwa asali yake.”
“Basi ondoa wasiwasi asali yako ipo salama.”
“Shaka, tuzungumze pembeni.”
MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie
Website: www.2jiachie.com
ANGALIZO: ITAENDELEAMPAKA MWISHO HAPA KAMA SHARE ZITAFIKA 3,000 NA COMMENT 2,000 VINGINEVYO MTAMALIZIA KATIKA KITABU


No comments

Powered by Blogger.