ad

ad

VAN GAAL KUPITISHA PANGA MANCHESTER UNITED …. Nani, Anderson, Marouane Fellaini, Shinji Kagawa, Javier Hernandez hatarini kutimuliwa

KOCHA wa Manchester United Louis van Gaal amesema atafanya maamuzi mazito juu ya ‘panga’ la wachezaji baada ya ziara mechi za majaribio.

Van Gaal amedhamiria kuwatema wachezaji ambao hajamvutia kwenye ziara hiyo ambapo wataalam wa mambo ya soka wanawaona wachezaji Nani, Anderson, Marouane Fellaini, Shinji Kagawa na Javier Hernandez wako hatarini kukumbwa na panga la Mdachi huyo huku ikiaminika kuwa Wilfried Zaha anaweza kupata nafasi ya kupigania maisha ndani ya United kwa mara ya pili baada ya kuambulia kutolewa kwa mkopo msimu uliopita.

“Nitafanya maamuzi baada ya ziara hii,” alisema Van Gaal alipoolizwa kuhusu mipango ya United wakati ikijiandaa kupambana na Liverpool katika fainali ya kombe la kimataifa la kirafiki kabla ya kupaa kurejea nyumbani.

“Niliwaacha wachezaji wote wacheze na sasa ninafahamu mengi kuliko ilivyokuwa kabla ya ziara hii.

“Pengine ni mapema mno kutoa maamuzi, lakini katika soka ni lazima utoe maamuzi. Ni vizuri kumpa mchezaji muda wa kutosha kufanya mipango ya usajili kwingineko. Unapaswa kuwaambia mapema kabla ya tarehe 31 mwezi huu. Nitaweka wazi kwa wachezaji baada ya ziara lakini nitawaambia wao, sio nyinyi (waandishi).”CREDIT: SALUTI5

No comments

Powered by Blogger.