ad

ad

UJUMBE WA TIMU WEMA KUELEKEA KWA DIAMOND PLATNUM NI HUU HAPA



“Mambo vipi? Sisi mashabiki wa @wemasepetu tunakuomba umsaidie Wema kama yeye anavyokusaidia. Labda niseme kwa uwazi bila woga kwamba mahali ulipo kimziki umefika sababu ya Wema. 

Wengine hatukuwa mashabiki wako lkn sababu ya mapenzi kwa Wema tukajilazimisha kukupenda tu... so unajua vema bila wema we mziki huna! Tunakuteteaga tu lkn huwezi kujilinganisha na wanamuziki wengine tunaowajua wanafanya vema kuliko wewe....leo sitawataja majina! nije kwa point yangu sasa wewe si mwanaume? Tuoneshe sasa! 

"Umetembea tembea nchi mbali mbali" umekutana na watu wa aina mbali...hujamtambulisha wema huko kibiashara, unaishia kusema maneno maneno ya sifa lkn unamwacha wema anapotea. Angekuwa wema she's always proud of you kukutaja popote hata angepata ile nafasi ya kuongea na karuache angekutaja, umeonana na kina davido+iyana bila kutaja waigizaji wakubwa Nigeria...Wema ni brand tunamlinganisha na top stars Africa!! We una nafasi kubwa sana kumfanya wema aonekane..but what your doing unampoteza kwa makusudi. Unamchezesha viduku, Ulipomwacha alikuwa na maendeleo makubwa alikua ameshatengeneza wanamuziki wake, nyumba yake, kipindi chake cha in my shoes kilianza bila mkono wako...ukaona hapa atakuzidi na unajua jinsi anavokupenda ukamtumia..hujawahi kusema hadharan feelings zako kwake zaidi ya mafumbo mafumbo...hujawahi kukanusha ile interview ya spora uliyomdiss vibaya wema....Je tueleweje sasa? Si lazima kuanika kila kitu mambo yenu binafsi.

 Wema haoni kwa sasa sababu ya mapenzi yake kwako...tunakuambia leo kama hauna nia nzuri na wema tunakuomba umuache. Maana unajua tu akimpigia promo mwanamuziki wake mirror utapotea kwa game. She has all this power tunaomba usimtumie kwa maslahi yako binafsi. #bringbackourwema

Majibu ya Diamond yalionesha wazi kuwa kinachompoteza mpenzi wake huyo ni kujikita zaidi katika maisha ya anasa na kuendekeza marafiki wanaopenda starehe huku pesa yake nyingi akiielekeza katika kuwapigisha bata mashoga zake na kusahau kuwekeza katika vitu vya msingi na kufanya kazi.
“Nafikiri ningewaona kweli mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa wasanii  wenu….kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze  Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe.”
Jiwe hilo limeupiga upande mwingine wa Wema Sepetu na kuonesha kuwa kinachomponza ni uvivu na kubase katika mapenzi na starehe akisahau kuhusu tasnia.
Inaonekana pia Wema amebadilika na kuwa tegemezi kwa Diamond ambaye amekiri kuwa anahakikisha anacheza nafasi yake kama mwanaume.
“Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie????

No comments

Powered by Blogger.