ROSE MUHANDO AMTAMANI GWAJIMA
Nyota wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
NYOTA wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando amesema anatamani sana kuhamia kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima kutokana na mahubiri yake mazuri.
Katika siku ambayo kulikuwa na sala ya shukurani kanisani kwa Gwajima Jumapili iliyopita Kawe jijini Dar es Salaam, mchungaji huyo alimwambia Rose aliyealikwa kuimba, kwamba yupo tayari kumjengea kanisa Dodoma anakoishi na yeye mwenyewe alisimamie.
CREDIT GPL

Post a Comment