MAREFA WAGANDA ‘WAINYONGA WAZI WAZI’ TANZANIA ZIMPETO IKICHAPWA 2-1 NA KUTUPWA NJE AFCON
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MAREFA
WA Uganda, wakiongozwa na Dennis Batte leo wameitupa nje ya michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Tanzania, baada ya kuwapendelea waziwazi
Msumbiji katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Zimpeto mjini hapa na
kupata ushindi wa mabao 2-1.
Matokeo
hayo yanamaanisha, Tanzania au Taifa Stars imetolewa katika hatua ya
mwisho ya mchujo ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya
AFCON mwakani nchini Morocco kwa jumla ya mabao 4-3, baada ya awali
kulazimishwa sare ya 2-2 Dar es Salaam.
Mambas
inaingia moja kwa moja kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na
Zambia kupigania tiketi ya AFCON ya mwakani Morocco.
Hadi
mapumziko, tayari Msumbiji walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na
Josimar Machaisse dakika ya 45 aliyeunganisha krosi kutoka upande wa
kulia.
Stars
ilicheza kwa kujihami tangu mwanzo na kujibebesha mzigo wa kudhibiti
mashambulizi mfululizo ya Mambas, huku yenyewe ikishambulia kwa
kushitukiza.
Pamoja
na mfumo huo, mashambulizi machache ya Stars yalikuwa yenye uhai na
kama si refa Dennis Batte kuwabeba wenyeji, Tanzania ingemaliza na bao
kama si mabao dakika 45 za kwanza.
Batte
alikataa bao zuri la kichwa la beki Said Mourad aliyeunganisha mpira wa
adhabu wa Khamis Mcha ‘Vialli’ baada ya Thomas Ulimwengu kuangushwa
dakika ya 17.
Mshika
kibendera nambari moja alimnyooshea kibendera cha kuotea mshambuliaji
John Bocco akiwa anakwenda kufunga, wakati alikuwa hajaotea dakika ya
44.
Hali
hiyo iliwakasirisha makocha wa Stars wakiongozwa na bosi wao, Mart
Nooij waliokwenda kumkaripia mwamuzi huyo. Batte alisogea kwenye benchi
la Tanzania na kuwaonya maofisa hao.
Kipindi
cha pili, kocha Mholanzi alianza na mabadiliko Stars, akimuingiza
kiungo Amri Kiemba kwenda kuchukua nafasi ya Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mabadiliko
hayo yaliibadilisha Stars pia na kuanza kutawala mchezo, wakifanya
mashambulizi mfululizo langoni mwa Mambas. Hata hivyo, refa Batte na
wasaidizi walitumia ujanja wa kitaaluma kupunguza kasi na mipango ya
Stars kusaka mabao.
Kila
wachezaji walipopamiana, mpira ulielekezwa kwa Tanzania- wachezaji wa
Msumbiji walikuwa wana maisha mazuri mno mbele ya marefa wa Uganda leo.
Pamopja
na yote, mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Ally Samatta
aliifungia Stars bao la kusawazisha dakika ya 75 baada ya kumkokota beki
wa Mambas hadi karibu na lango la Msumbiji kabla ya kufumua shuti
lililomshinda kipa Dario Khan.
Baada ya bao hilo, kasi ya mashambulizi ya Stars iliongezeka hasa baada ya kuingia Mrisho Ngassa aliyekwenda kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na Simon Msuva aliyechukua nafasi ya John Bocco. Hata hivyo, refa Batte na wasaidizi wake waliendelea kuifanyia ‘roho mbaya’ Tanzania akiua mashambulizi na kuwaruhusu wachezaji wa Msumbiji kucheza na muda. Elias Pelembe aliiandikia Msumbiji bao la pili dakika ya 81 kwa shuti la mpira wa adhabu lililotinga nyavuni moja kwa moja, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Kevin Yondan. Stars ilianzisha mpira haraka na kuendelea kusaka mabao, lakini bado Batte aliendelea kikwazo kwao- kwa kuwabeba wenyeji. Baada ya Mganda huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo, wachezaji wa Stars walimfuata kumlalamikia huku wakilia kwa kuwanyonga wazi wazi leo.
Wachezaji wa Stars walishindwa kuificha huzuni yao baada ya kuanza kulia uwanjani kwa matokeo hayo, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Thomas Ulimwengu na Shomary Kapombe ambao walikuwa hoi baada ya kulia sana. Stars ambayo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza AFCON mwaka 1980 enzi hizo bado ikiitwa Kombe la Mataifa Huru ya Afrika, sasa itasubiri mbio za kuwania fainali za michuano hiyo za mwaka 2017 nchini Libya. Kikosi cha Stars kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Said Mourad, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngassa dk75, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Simon Msuva dk65, Mbwana Samatta na Khamis Mcha ‘Vialli’/Amri Kiemba dk46. Msumbiji; Dario Khan, Momed Hagi, Zainadine Junior, Saddan Guambe/Eduardo Jumisse dk80, Francisco Mioche, Elias Pelembe/Isaac de Carvalho, Josemar Machaisse, Reginaldo Fait, Apson Manjate/Clesio Bauque dk41, Almiro Lobo na Richard Campos.
![]() |
| Shomary Kapombe akilia baada ya mechi |
![]() |
| Kapombe akimtoka beki wa Msumbiji |
![]() |
| Refa Dennis Batte akisindikizwa na Polisi na mbwa baada ya mechi |
![]() |
| Mbwana Samatta akilia baada ya mechi |
Baada ya bao hilo, kasi ya mashambulizi ya Stars iliongezeka hasa baada ya kuingia Mrisho Ngassa aliyekwenda kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na Simon Msuva aliyechukua nafasi ya John Bocco. Hata hivyo, refa Batte na wasaidizi wake waliendelea kuifanyia ‘roho mbaya’ Tanzania akiua mashambulizi na kuwaruhusu wachezaji wa Msumbiji kucheza na muda. Elias Pelembe aliiandikia Msumbiji bao la pili dakika ya 81 kwa shuti la mpira wa adhabu lililotinga nyavuni moja kwa moja, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Kevin Yondan. Stars ilianzisha mpira haraka na kuendelea kusaka mabao, lakini bado Batte aliendelea kikwazo kwao- kwa kuwabeba wenyeji. Baada ya Mganda huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo, wachezaji wa Stars walimfuata kumlalamikia huku wakilia kwa kuwanyonga wazi wazi leo.
Wachezaji wa Stars walishindwa kuificha huzuni yao baada ya kuanza kulia uwanjani kwa matokeo hayo, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Thomas Ulimwengu na Shomary Kapombe ambao walikuwa hoi baada ya kulia sana. Stars ambayo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza AFCON mwaka 1980 enzi hizo bado ikiitwa Kombe la Mataifa Huru ya Afrika, sasa itasubiri mbio za kuwania fainali za michuano hiyo za mwaka 2017 nchini Libya. Kikosi cha Stars kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Said Mourad, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngassa dk75, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Simon Msuva dk65, Mbwana Samatta na Khamis Mcha ‘Vialli’/Amri Kiemba dk46. Msumbiji; Dario Khan, Momed Hagi, Zainadine Junior, Saddan Guambe/Eduardo Jumisse dk80, Francisco Mioche, Elias Pelembe/Isaac de Carvalho, Josemar Machaisse, Reginaldo Fait, Apson Manjate/Clesio Bauque dk41, Almiro Lobo na Richard Campos.
CREDIT: BIN ZUBEIRY BLOG

Post a Comment