Maximo ataja sababu 3 za kuwatosa Okwi, Kiiza
Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, ametaja vitu
vitatu vitakavyoamua nani wa kubaki kwenye kikosi chake kati ya Emmanuel
Okwi na Hamis Kiiza kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mbrazili huyo, hadi hivi sasa bado hajaamua nani wa kumuacha kwenye kikosi chake hicho kutokana na idadi ya wachezaji kuvuka watano kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza Maximo alisema kuwa kabla ya kuamua nani atakayemtema, kwanza anaangalia uwezo wa kila mmoja ndani ya uwanja kwa kutazama video za mechi ambazo wamecheza viungo hao washambuliaji.
Maximo alisema pia ataangalia nani anatimiza majukumu yake vizuri akiwa uwanjani na mwisho ambacho ni muhimu ni nidhamu ya kila mmoja.“Mimi ninapenda sana mafanikio ya timu ndani ya uwanja, ndiyo maana nimeweka msingi mzuri katika timu, lengo langu ni kutengeneza kikosi cha ushindani.
“Hao akina Okwi na Kiiza kabla ya kuamua nani wa kubaki na nani atakayeondoka, nimeona ni bora nitumie video za mechi zao walizocheza.“Pia nitaangalia nani anatimiza majukumu yake vizuri akiwa uwanjani ikiwemo msaada wake na mwisho ni nidhamu katika timu ambayo nimepanga kukutana na uongozi kujua kila mmoja nidhamu yake,” alisema Maximo.

Post a Comment