Kumbe Vikiungwa Vitamu - 06
“Bi
Shuu mbona wasichana hatuna vitu hivi?”
“Siku
hizi uzungu umetawala na kujikuta wakipoteza vitu vingi vya kumfurahisha
mwanaume. Kumfurahisha mwanaume kitandani si kigezo pekee cha kuilinda nyumba
yako. Kuna vitu vingi ambavyo vipo nje ya kitanda.
“Kuna
wasichana wengi wana nyonga laini kama unakula keki lakini wana mapungufu kama
chujui la nazi ambayo hayawezi kumfanya atulie kwa kwenye ndoa yake. Kama tabia
yako nzuri ulichanganya na machejo ya kitandani hata utakita hata ndege utanunuliwa
japo mwenzio hana uwezo wa kununua baskeri.”
“Mbona
hujanifunda na hivyo?”
“Siwezi
kukuichanganya kimoja kimoja, kwanza tunatengeneza mtego akiingia anase,
ukimaliza mafunzo ya mwili tunarudi tena kilingeni ili mumeo aone tofauti ya
magumegume na mwanamke.”
“Bi
Shuu mbona nimechoka sana.”
“Umelia
mara ngapi?”
“Mara
nne.”
“Mara
ya mwisho ulilia mara ngapi ulipokutana na mwanaume kabla ya leo?”
“Mara
mbili sijawahi kulia zaidi ya hapo.”
“Ndio
maana, lazima uchoke umeukamua mwili
sana na shughuli haikuwa ya kitoto kuna kipindi kidogo nisimamishe mpambano
mlikuwa kama mnataka kutoana roho.”
“Bi
Shuu umejuaje?”
“Nikuambie
mara ngapi nilikuwa nafuatilia toka mwanzo mpaka mnamaliza”
“Jamani
Bi Shuu kumbe ulikuwa unanipiga chabo,” Mbona niliona aibu mtoto wa kike,
jamani bibi huyu ana mambo kumbe mwenzie nahenyeka yeye anapiga chabo.
“Sasa
ningejuaje mapungufu yako.”
“Mmh,
makubwa madogo yana nafuu.”
“Na
hayo mengine lini maana muda wa kurudi kazini umekaribia.”
“Wiki
iliyobakia inatosha, kapumzike jioni kama kawa mpaka kieleweke.”
“Wacha
nikalale naona mwili sio wangu, kwenye pesa hiyo chukua nusu niachie nusu”
“Asante
mwali, nina imani sasa umeamini nilichokisema kinatimia”
“Wee
mwisho Bi Shuu je, ungenikamata ndio unavunja ungo naona kila aliyenionja
angeniganda kama ruba.”
Baada
ya mazungumzo nilimuomba Bi Shuu nikapumzike mwili ulikuwa na uchovu,
nilikwenda chumbani kwangu kulala kwa kulifungulia feni mpaka mwisho mtoto wa
kike nilijiachia kitanda kizima.
*******
Kama
kawaida Bi Shuu aliniamsha kwenye chakula cha mchana na baada ya chakula cha
mchana nilioga na kupanda tena kitandani. Sikuamini mwili kuchoka kiasi kile,
Bi Shuu alinieleza ni kutokana na kuzoea kulala kama gogo kitandani lakini siku
ile niliushughulisha mwili hata kumwaga machozi manne kitu ambacho hakikuwa
kawaida yangu.
Nilipogusa
kitandani usingizi haukuchelewa kunichukua, Bi Shuu aliniamsha saa mbili za
usiku nilikwenda kuoga kisha nilipata chakula cha usiku. Baada ya chakula
nilipumzika kidogo na kuingizwa unyagoni kumalizia muda ulipobakia kwa kunipa
mbinu za kummiliki mwanaume kwa sauti na matendo huku tabia ikiwa ndiyo
uliyochukua sehemu kubwa.
Katika
mafunzo siku moja alinipa nipike chakula baada ya kupika tulikula wote, kesho
yake alinipa nipike tena chakula kilekile, lakini hakunipa chumvi.
Nilipomuuliza alisema nipike vile vile na muda wa kula nilishindwa kumuelewa
baada ya kunieleza nipakue, nilipakua na kukila bila chumvi. Tulikula wote bila
kujua chakula kile kwa nini tulikila
bila chimvi.
Sikutaka
kumuuliza kwa vile hakikuwa kingi tulikuwa na kukimaliza wote. Baada ya chakula
usiku Bi Shuu akiwa ameniweka chini aliniuliza.
“Manka
kuna tofauti gani ya chakula ulichopika jana na leo?”
“Tofauti
yake cha jana kina chomvi lakini cha leo hakina chimvi.”
“Kipi
chakula kizuri?”
“Cha
jana.”
“Kwa
sababu gani?”
“kina
chumvi lakini cha leo hakina chimvi.”
“Mbona
umekila.”
“Nilishindwa
kuelewa ulikuwa na maana gani.”
“Lakini
bila hivyo usingekula?”
“Nisingekula.”
“Unajua
nilikuwa nina maana gani?”
“Hata
sijui”
“Hii
nakuonesha yaisha ya ndani ya ndoa, wanawake wengi wanawalisha wanaume chakula
kisicho na chumvi. Wapo wanaokosa uvumilivu huvunja ndoa lakini wanaoburuzwa na
mapenzi hula chakula kisicho na chumvi kila siku na kuishia kunung’unika
moyoni.”
“Lakini
Bi Shuu kama mkewe hamuwekei chumvi anashindwa vipi kuchukua mwenyewe kuweka kwenye chakula”
“Swadakta
swali zuri, ndio maana kukuweka huku ndani vitu vingi huvifanya kwa mafumbo
jibu lake huwa ndio maisha yako ndani ya mahusiano yako. Chakula na chumvi
sikuwa na maana hiyo bali kukueleza matatizo ndani ya nyumba nyingi wanawake
wengi ndoa zao uziondoa chumvi bila wao wenyewe kujua”
“Kivipi?”
“Nyumba
nyingi mwanzo wa mapenzi huwa moto moto kama kumpokea mpenzio akirudi kumtengea
chakula kula pamoja kuoga pamoja kuwa karibu yake kumpoza uchovu wa kutwa nzima
ambao ndiyo tiba ya mwanaume kutoitafuta faraja nje ya ndoa yake.
“Wengi
baada ya muda baadhi ya vitu hundoka kabisa na ndoa kuendeshwa kimazoea, moyoni
lazima utasema hivi nisivyofanya kuna nini kwani hawezi kufanya mwenyewe.
Kuacha kuyafanya hayo ni sawa kuondoa chumvi kwenye mahusiano yako na kumfanya
mpenzio kula chakula kisicho na chumvi.
“Wengi
huvumilia na kuumia moyoni lakini wasio na uvumilivu huitafuta chumvi hiyo nje
ya ndoa. Hapo ndipo tatizo linapoanza na kuipoteza ndoa yako bila kujua tatizo
ni wewe mwenyewe. Kuondoa baadhi ya vitu ndani ya ndoa yako kama kutompokea
mumeo au kutokula na kuoga pamoja ni vitu vinavyo mwanaume huona vya kawaida
lakini ni ufa mkubwa katika ndoa.
“Penzi
halizeeki bali mwili ndio unazeeka, vyote nilivyokueleza usikipunguze hata
kimoja ukiingia katika ndoa yako. Nakuhakikishia bwana atakaye kuoa watu
watasema umemuwekea libwata, limbwata mwali ni kumlea mumeo kama mtoto. Nina
imani umenielewa”
“Mmh,
kweli nimekubali Mungu kakujalia kumtengeneza mwanamke, nina imani
ungenieleza kwa maneno ningekuelewa nusu
lakini kwa vitendo nimekuelewa zaidi. Asante Bi Shuu”
“Nashukuru
kuonesha ni muelewa na mtu mwenye usongo na mafunzo”
“Lazima
Bi Shuu niwe na usongo nimeteseka sana”
Nilimalizia
mafunzo huku akilekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye mtihani wangu wa kwanza.”
Nilikuwa
sijawahi kula kungu mtoto wa kike nilikula kungu jicho ukiniangalia utanionea
huruma. Nilimaliza mafunzo salama, kabla ya kuanza kazi alinitafutia tena
mwanaume mwingine naye alikuwa mmoja wa wale walioninanga mwanzo.
Nilikuwa
na imani alikuja akijua ni yule Manka wa mwaga msigo babangu kisha uondoke.
Mafunzo niliyopata ya mwisho mtoto wa kiume chozi lilimtoka, kwenye maandalizi
tu alilia zaidi ya mara tatu. Mtindo huu nilifundishwa kama sitaki kutumika
sana kwanza namchosha mwanaume mwenye maandalizi.
Hata
ulipoingia baharini nusra anifie maji baada ya kushikwa na pumu katikati ya
safari, machejo yalimfanya aifukuze Land Curuser VX kwa bajaj. Ilibidi niingie
kazi ya kumpepea asinifie, baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida
aliniangalia mara mbili.
“Ni
wewe Manka au naota”
“Kwani
vipi?”
“Hata
siamini, kumbe ulikuwa unafanya makusudi”
“Ulikuwa
vya chukuchuku sasa vimeungwa”
”Una maana gani?”
”Una maana gani?”
“Si
umeona mwenyewe si la kusimuliwa”
“Nimekubali
lazima nirudie”
”Mmh, cha kunifia kifuani hapa namefungulia injini moja katika injini nne si ungebadilika jina.”
”Mmh, cha kunifia kifuani hapa namefungulia injini moja katika injini nne si ungebadilika jina.”
“Manka
naomba nikuoe.”
“Ni
haraka sana vuta subra”
“Lakini
niwe mmoja wa watu wa mbele kufikiriwa.”
“Hakuna
tatizo”
Yule
kijana ambaye alikuwa kama mlevi aliniachia laki moja ya asante”
Baada
ya kuondoka Bi Shuu kama kawaida yake alitoa tathimini yake.
“Mwali
japo mpinzani wako hakuonesha upinzani lakini umejitahidi sana tena sana, sasa
nina uwezo wa kukueleza kapambane na mtu yoyote. La muhimu kuzingatia
niliyokueleza hakika kila atakayehusa lazima anate sasa hivi mwili wako ni
asali yenye ulimbo”
Maneno
ya Bi Shuu yalinifanya nijiamini nimeanza kuiva kimapigano, kwa vile muda
ulikuwa umekwisha jumatatu ilipofika nililipoti kazini kwangu. Nilimkuta
aliyekuwa amenishikia, baada ya kunipokea alinielekeza kazi za kufanya na yeye
kuendelea na majukumu mengine. Kuna kitu kimoja nilisahau kukueleza baada ya
kukaa ndani kuchezwa nilipotoka nilitakata na kunawili mtoto wa kike.
Nikiwa
naendelea na kazi bosi wangu dear zilipendwa aliingia ofisini, ilionesha
hakujua kama naanza kazi siku ile. Alipofika hakuniangalia alinisalimia.
“Za
saizi?”
“Nzuri”
“Ile
kazi tayari?”
“Ndiyo
namalizia”
’Baada ya muda gani”
”Dakika kumi”
’Baada ya muda gani”
”Dakika kumi”
“Ok,
fanya haraka.”
Baada
ya kusema vile aliingia ofisini kwake, ilionesha hakujua kama nipo mimi. Baada
ya kumaliza kazi niliyoikuta niliprinti na kumpelekea, alikuwa bado ameinama
nilipofika mbele yake nilisema.
“Bosi
kazi tayari”
Sauti
yangu ilimshtua na kunyanyua macho, kwa mshangao wa ajabu alisema.
“Ha!
Manka umekuja saa ngapi?”
“Toka
asubuhi”
“Ina
maana nimekupita kwenye ofisi yako?”
“Ndiyo
bosi”
“Ooh,
samahani sana”
“Kawaida
tu bosi wala usijisikie vibaya,” mtoto wa kike nilikuwa nimekwenda kimitego na
kumuomba Mungu Mateja ajichanganye sijui aonje kidogo. Niliapa ningefanya
aliyofundishwa na mengine nisiyo yajua ili kuhakikisha anakutana na vitu vipya
katika medani ya mapenzi.
Mtoto
jicho lilikuwa limelegea kidogo jicho lilionekana kwa kujipaka wanja chini na
juu na kuongeza uzuri wangu. Japo nilijijua mi mzuri, lazima mzuri ujijue kabla
hujasifiwa na watu, lakini mapungufu yangu Bi Shuu aliyamaliza mengi niliyokuwa
nayo.
Mateja
ilionekana kama kuchanganyikiwa kuniona nimebadika nimependeza na ninavutia
tena kimitego ya kike hasaa.
“Manka
ulikuwa unakula nini?”
“Kwa
nini bosi?” nilimuuliza kwa sauti laini huku nikimchanulia tabasamu ya kufa mtu
huku jicho nalo likizungumza.
“Hapana,
umependeza na unavutia”
“Nashukuru
kwa hilo ila moja umesahau”
“Lipi
hilo?”
“Sasa
hivi si Manka chukuchuku ila Manka huyu kaungwa akaungika”
“Una
maana gani?”
“Bosi
nitakuomba kesho nikukaribishe chakula cha usiku”
“Mmh,
hakuna tatizo kwa vile wiki hii ni ya mwisho baada ya hapo nitakuwa katika
maandalizi ya harusi.”
“Hakuna
tatizo kazi njema.”
“Na
wewe pia.”
Baada
ya kumkabidhi kazi yake nilirudi kuendelea na kazi yangu, moyoni niliapa kama
kweli atakubali mwaliko wangu amekwisha.Muda wa mchana Mchumba wake alimuijia
kama kawaida na kwenda naye kupata chakula cha mchana.
Japo
moyo uliniuma lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo kutokana na
makosa kuyafanya awali. Jioni niliporudi nilimueleza Bi Shuu mwaliko niliompa
Mateja kuja kula chakula cha usiku.
“Mwali
akiingia amekwisha, hakikisha anaisahau ndoa yake”
“Bi
Shuu la kuuliza hilo”
“Nakuaminia
mtu wangu.”
“Naiona
kama kesho inachelewa”
“Itafika
punguza munkari, usije yakakamia maji”
“Si
hivyo Bi Shuu nakuhakikishia kuyafanya yote kwa umakini mkubwa labda asije.”
*****
Siku
ya pili nilikwenda ofisini na kuendelea na kazi bosi alipokuja alinisalimia.
“Mrembo
hujambo”
“Sijambo
bosi simshindi wifi”
“Manka
mbona umefika mbali salamu umeijibu sivyo”
“Samahani
bosi, za nyumbani”
“Mmh,
salama sijui zako.”
“Nami
namshukuru Mungu, haya nipo ndani”
“Sawa
bosi”
Kabla
ya kuingia ofisini aligeuka na kuniuliza.
“Mwaliko
wa usiku upo vile vile au kuna mabadiliko”
“Hakuna
mabadiliko”
“Haya,”
alisema huku akifungua mlango na kuingia ofisini kwake.
Baada
ya kuingia ofisi nilibaki nilikuwa siamini kama nimesikia vizuri kuulizia
mwaliko, niliona dalili njema zimeanza asubuhi jioni ni kumalizia tu. Huwezi
amini siku hiyo nilifanya kazi kwa furaha ya ajabu kama Mateja amenikubali nirudiane
naye.
Jioni
kabla ya kuondoka aliniaga na kuniahidi angekuja usiku.
“Kweli
Mateja utakuja?”
“Kama
siji ningekuambia”
“Karibu
sana mpe..” Mungu wangu nilitaka kujisahau kumwita mpenzi wakati tuliisha
achana long time a go.
“Niite
tu mpenzi wala usijisikie vibaya,”
“Hapana
bosi”
“Haya
baadae”
Mateja
aliondoka na kuniacha nikipanga vizuri vitu vyangu kabla ya kurudi nyumbani.
*********
Nilkipofika
nyumbani Bi Shuu aliniomba siku ile aandae chakula cha mgeni, sikuwa na hiyana
mtoto wa kike nilimuacha afanye mambo yake. Nilikiandaa chumba changu na
kukiweka katika hali ya usafi wa hali ya juu, kama kawaida Bi Shuu alinipatia
mafusho ya manukato mazuri.
Baada
ya kuhakikisha chumba changu kinapendeza niliingia kuoga mtoto wa kike na
kujifusha utuli huku nikipaka wanja wa sina mume ambao lazima mwanaume
barabarani akusalimie.
Baada
ya kusimama mbele ya kioo kujitathimini, nilizidi kujisifia mtoto wa kike kwa
upendeleo niliopewa na mwenyezi. Baada ya kuhakikisha nipo sawa, nilikunywa
kungu na kuanza kujisikia nikisisimka mtoto wa kike kama mamba mwenye njaa.
Nikiwa
nimekaa mkao wa kula kumsubiri Mateja, mara aliingia Bi Shuu na kuniongezea
mambo fulani ya muhimu pindi Mateja akiingia chumbani kwangu.
“Mwali
nilitaka kusahau kwa vile anajua anakuja kula chakula na kuondoka cha kufanya
akiingia tu, ukimvamia kwa kumkumbatia huku akimbusu hakikisha mikono yako
inafanya kazi ya haraka kumvua nguo bila kuchelewa mpatie upande wa kanga.
Wakati
huo mimi nitakuwa tayari nimepeleka maji ya kuoga bafuni niliyoyawekea viungo.
Nani alikuambia wanawake wa Tanga ndio wanajua mahaba, nataka Mateja akiondoka
kila kitakachokuja mbele yake akione shombo.”
“Nimekuelewa
Bi Shuu.”
“Sio
umenielewa bahati hairudi mara mbili, itumie kubadili matokeo.”
“Matokeo
ya nini Bi Shuu?”
“Ukimaliza
kilicho tupotezea muda nitakwambia.”
“Nitafuata
maelekezo yako.”
Baada
ya kutoa maelekezo Bi Shuu alirudi kumalizia kutengeneza maajumati ya mgeni
rasmi.
Majira
ya saa moja na nusu gari la Mateja lilisimama mbele ya nyumba yetu, ajabu
usongo wote niliokuwa nao uliyeyuka kama donge la mafuta katika kikaango cha
moto. Nilijikuta nikijawa na hofu juu ya nilichokipanga kumpa Mateja kama
ataingia katika mtego wangu.
Nilijihisi
kupoteza ujasiri niliokuwa nao kabla ya Mateja hajaja, niliikandamiza mikono
yangu kifuani na kubana pumzi na kukaa kwa muda kuvuta ujasiri kisha niliitoa
na kushusha pumzi nzito.
Baada
ya kujipa ujasiri nilijitengeneza haraka haraka ili kujiweka sawa japo nilikuwa
nimejiweka kimitego ya kike hasa. Ndani nilivalia kufuri la bikini la rangi
nyekundu juu nilivalia kanga nyepesi ukituliza macho unaona kila kitu cha
ndani.
Wakati
huo chumba kilikuwa kikinukia utuli kila kona mimi mwenyewe nilikuwa kama
Hululaini malaika wa daraja la juu. Jicho mtoto lilikuwa lemelegea kwa kungu
huku mwili ukisisimka kama nyoka mwenye hasira aliyepandisha sumu kwa ajili ya
kumgonga mtu.
Wakati
nikifanya matayarisho ya mwisho kabla ya kumpokea Mateja mbele ya kioo, Bi Shuu
muda huo alikuwa amempokea.
“Wawooo
mwanaume huyo.”
“Niambie
kipenzi changu?” Sauti ya Mateja ilisikika.
“Niseme
nini mkeo nawe umetupa jongoo na mti wake.”
“Bi
Shuu kama ningetupa leo ningeonekana hapa?”
“Mateja
kula nisishibe heri nisipewe.”
“Bi
Shuu heri nusu shari kuliko shari kamili na kidogo si haba kuliko kukosa
kabisa.”
“Nitakuwezea
wapi mtoto wa Kisukuma aliyejifanya Mzaramo kwa kujifanya unajua kuyageuza
maneno.”
“Vipi
nimewakuta?” Mateja aliuliza mimi ndani kiroho paa!
“Umewakuta
wamejaa tele wewe tu,” mmh, maneno ya Bi Shuu yalijaa nahau na misemo na kuzidi
kuniweka njia panda.
Wakati
nikijua hodi itapigwa wakati wowote nilipandisha tena pumzi na kuzishusha kisha
nilijiandaa kumpokea. Mara mlango uligongwa.
“Hodi
ndani?”
“Karibu,”
nilimkaribisha huku nikikaa mkao wa chura kuruka.
Mara
mlango ulifunguliwa na Mateja aliingia, mtoto wa kike nilijizoazoa na
kumkumbatia.
“Ooh,
karibu mpenzi.”
“Asante
za hapa?”
“Nzuri.”
Mtoto
wa kike niliutambaza mdomo wangu na kutua kwenye mdomo wa Mateja ambaye alikuwa
bado amepigwa na butwaa, nikihema kama mgonjwa wa pumu. Mateja alinipokea na
kubadilishana mate, mikono yangu alipata nafasi ya kumvua shati.
Baada
ya kumvua shati nilimsukumia kitandani na kumlalia juu, kwa haraka nilimalizia
na vilivyokuwa vimebaki chini kisha nilimpatia upande wa kanga. Kila
nililolifanya siku ile kwa Mateja kilikuwa kigeni kwake niliamini alijua bado
Manka wa mwaka 47 hohehahe asiyejua chochote.
Niliamini
muda huo Bishuu alikuwa ameisha peleka maji yaliyochanganywa na viungo bafuni.
Nilimshika mkono Mateja na kutoka naye
nje kumpeleka bafuni kuoga, Bi Shuu kweli alikuwa amepania mlangoni
nilikuta kuna ndala mpya. Mateja alivaa na kuongozana naye hadi bafuni.
“Karibu
mpenzi uoge.”
“Asante.”
Nilimwacha
Mateja bafuni na kurudi ndani kujiandaa kumlisha vilivyoungwa na Bi Shuu. Kabla
sijaweka tako chini Bi Shuu aliingia bila hodi na kusema kwa sauti ya juu.
“Wee
mwana, ndio unafanya nini?” Kauli ile ilinishtua sana.
Kutokana
na makosa ya kuruka baadhi ya sehemu katika hadithi ya wiki iliyopita kufikia
hatua ya kuwachanganya wasomaji. Leo tutaelezea kwa ufupi toka Mateja
alipomuona Manka ofisini mpaka kufikia hatua ya kumsubiri chumbani. Baada ya
Mateja kushtuka kumuona Manka jinsi
alivyopendeza kwa muda ambao hakuwepo kazini alimsifia kuwa amependeza mara
dufu. Naye Manka alitumia nafasi ile kumkaribisha Mateja chakula cha jioni
kwake. Mateja alimkubalia na kumuahidi angefika jioni kwa ajili ya chakula.
Manka
aliporudi nyumbani alimueleza Bi Shuu kuwa Mateja amekubali kuja kula chakula
cha jioni. Bi Shuu alimueleza asiipoteze nafasi ile adimu ahakikishe kama
atakubali kuvila vilivyoungwa basi achanganyikiwe. Bi Shuu alimuomba kazi ya
kupika chakula aifanye yeye ya kuandaa chakula cha ujanani kwake pale alipokuwa
akimtengenezea mpenzi wake.
Baada
ya makubaliano na Bi Shuu Manka aliingia ndani kujiandaa kwa ajili ya kumpokea
Mateja kwa kufanya usafi wa mwili na chumba huku akifusha udi na asumini
kumwagia kitandani. Yalikuwa mafunzo tosha ya Bi Shuu ambayo Manka aliyafanyia
kazi.
Baada
ya kila kitu kuwa tayari Manka alimsubiri kwa hamu Mateja mpaka alipofika.
Baada ya kumuandalia maji na kumuacha aoge peke yake ndipo Bi Shuu alipomfuata
na kumuuliza amefanya nini.
Ili
kujua kosa lake nina imani mpaka sasa tupo pamoja, haya tuserereke pamoja...
Kauli
ya Bi Shuu ilinishtua na kujiuliza nimefanya kosa gani tena.
“Bi
Shuu nimefanya nini?”
“Manka
haya ndiyo makosa mnayafanya sana wanawake wengi, kwa nini umuache aoge peke
yake. Nenda kaoge naye ikiwezekana anza kumliza kilio cha raha bafuni.”
Mmh,
mtoto wa kike haraka nilitelemsha nguo ya ndani na kubakia na upande wa kanga
nyepesi na kumuwahi Mateja kabla hajajipaka sabuni. Nilipokaribia bafuni Mateja
alikohoa kumaanisha kuna mtu.
“Mm..mm..mmh.”
Nilisukuma
mlango na kumkuta amejipaka sabuni usoni, alipofumbua macho aliniona nipo mbele
yake.
“Aah,
kumbe wewe?”
“Ulidhani
nani?”
“Nilifikiri
kuna mtu kaingia kwa bahati mbaya.”
“Nilikwenda
kutoa nguo ili tuje tuoge wote,” nilidanganya.
“Sasa
mbona hukuniambia kama tunaoga wote uliondoka kimya kimya.”
“Nilijua
nakuwahi.”
“Haya
tuoge.”
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

Post a Comment