Kumbe Vikiungwa Vitamu - 01
Toka nimezaliwa nimekuwa mwanamke mwenye mkosi kila mpenzi wangu mwanzo wa mapenzi yalikuwa motomoto. Lakini baada ya muda fulani mwanaume alinimwaga bila sababu za msingi. Kila siku ya Mungu nilishindwa kuelewa nina matizo gani mtoto wa kike miye. Kibaya zaidi ndoa niliyofunga miezi minne iliyopita ilivunjika huku mpenzi wangu akipagawa na penzi la nje. Jamani mbona makubwa, huyo mwanamke aliyenivunjia ndoa yangu hata mkonioni hajai, hanizidi kwa lolote si kwa sura wala umbile. Niliamini maneno ya watu huenda yule mwanamke ni mchawi. Kitendo cha ndoa yangu kuvunjika na historia yangu ya nyuma ya kuachwa kwenye mataa na wanaume kiasi cha kugeuzwa jina ubao wa shabaha kila mwanaume kujifunza kulenga kwangu na akichoka hiondoka bila kwaheri. Bahati niliyokuwa nayo mwanaume yeyote aliyenitaka, yupo radhi kunihonga hata milioni ili mradi anipate, Mungu alijilalia umbile na sura lakini niliamini kuna kitu kikubwa kimepungua kwangu kinachofanya wanaume wanikimbie. Kwani moto anaoanza nao mwanaume kama maji ya moto lakini baada ya muda hupoa. Lakini hachelewi kupoa, wapo niliokaa nao mwezi mwili, mitatu , wiki na wengine wakionja hawarudi tena. Kuna watu walionifuata na kunieleza labda niende kwa waganga wa kienyeji ili nisafishwe nyota yangu. Ushauri ule niliufuata baada ya kutumia dawa zile sikuchelewa kupata bwana aliyetangaza ndoa kabisa. Lakini baada ya miezi minne ndoa yangu ilivunjika, kitendo kile kilinitia aibu, yote ya kuchezewa na wanaume na kuachwa ilikuwa tisa, kumi ilikuwa kuachwa bila sababu huku mume wangu akizama kwenye penzi ya kinyago msela mwanamke asiye na mbele wala nyuma. Kitendo kile kilinidhalilisha sana, sikuweza kuvumilia bila kujieleza siku ya pili nilipanda gari mpaka Dar na kufikia kwa rafiki yangu niliyekuwa nasomanaye shule moja ambaye baada ya kumaliza shule alikwenda Dar kutafuta maisha na baadaye alinieleza amepata chumba tena anafanya kazi kwenye kampuni ya mtu binafsi. Kwa vile nilikuwa na siku yake nilipomjulisha nakwenda Dar hakunikatalia Nilipanda basi hadi Dar. Baada ya kufika nilikaa mwa muda wa mwezi mmoja na kunitafutia kibarua katika kiwanda kimoja, ajabu msimamizi alinizimikia na kuanzisha mahusiano na mimi. Kwa vile kila mmoja alikuwa na ujiko kuwa na uhusiano na bosi basin a mimi nilimkubalia. Kama kawaida haikuchukua hata mwezi akanimwaga na kashfa nyingi kwamba heri atembee na mwanaume mwenzake kuliko kulala na mimi. Kwa kweli kitendo kile kilizidi kunidhalilisha na kuniweka kwenye wakati mgumu, kibaya kila mwanaume niliyekuwa nakutana naye na kuniacha hakunieleza tatizo langu. Kwa kweli niliumia sana na kuamua kuacha kazi, niliapa sitakuwa tayari kufanya kazi wala kuanzisha uhusiano na mwanaume yeyote. Baada ya shoga yangu kupata bwana ilinibidi nihame kwa kutafutiwa chumba sehemu za uswahili kwa bibi mmoja maarufu pale mtaani Bi Shuu, ni bibi wa miaka 55 lakini mambo yake temea chini. Bibi yule alinilea kama mwanaye wa kuzaa hata kodi yangu hakuitaka. Kuhamia kwa Bi Shuu nilijikuta nikiingia dunia nyingine kabisa, kweli nimekubali tembea uone mambo, ningekaa Arusha ningeyajua haya. Nazidi kukubali kweli vikiungwa vitamu, tena mtu ataomba aongezwe na akimaliza kula lazima ajilambe vidole. Najua una hamu kuvijua hivyo vitamu vilivyo ungwa mpaka watu wakajilamba, Naomba twende pamoja tuipate wote faida ya kuwa karibu na makungwi kama Bi Shuu. ******** Katika mambo niliyokuwa siyapendi katika maisha yangu ni pamoja na kusumbuliwa na mwanaume wakati wa kilimo cha mhogo. Ooh! Inama, mara jipinde hivi, mara geuka hivi. Siku zote nilijiuliza kwani bila kukusumbua hivyo mwanaume hawezi kufikisha mzigo wake. Kitendo cha kijana huyu ambaye alinipata kupitia kwa Bi Shuu kutaka kunisumbua kilinikera sana. “Manka mbona hivyo sasa raha ya mapenzi ipo wapi?” “Nimesema sifanyi unavyotaka, sipo kwenye mazoezi ya yoga hapa kama huwezi hivi, vaa nguo zako ondoka, ” nilisema kwa ukali bila kumuangalia nyuma yangu alipokuwa amekaa. “Lakini Man…,” “Ee..ee..eeh, nasema hivi kwani tatizo nini bila hivyo unavyotaka hufiki safari yako?” Nilimkata kauli Edward. “Manka raha ya chakula ubadili mapishi mchele mmoja lakini una mapishi zaidi ya kumi.” “Kwani huo mchele ukipika bila kubadili mapishi hauivi?” “Lakini Manka kuna tatizo gani kufanya ninavyotaka, sema niongeze kiasi gani ukubaliane na mimi ili nami nifaidi raha ya mapenzi?” “Kaka eeh! Mimi sio chombo cha mazoezi, mlango huoo, unaweza kuondoka hukuitwa na mtu chumba changu mwili wangu eeh.” Yule kijana alipandwa na hasira, alinyanyuka na kupitia suruali yake na kutoka bila kuaga, nilifyonza na kujilaza huku nikinyanyuka na kupitia upande wa kanga na kujifunga kisha nilirudi kujilaza kitandani. Nilijikuta nikipandwa na ghadhabu kitendo cha Bi Shuu kunitafutia wanaume na kugawana kitakacho patikana. Nilijikuta nikijiona nimekataa nini na ninafanya nini. Sikuwa na tofauti na wale wanawake wanaojiuza kwenye vyumba vyao kwa wanaume kupanga foleni. Japo kwangu haikuwa hivyo, mimi ilikuwa naitwa na Bi Shuu na kuelezwa juu ya kijana kunipenda na kuwa mtu wangu wa karibu wakati mambo yangu hayajawa mazuri. Lakini kila mvulana aliyekuja baada ya kunionja hakurudi tena, lakini wa leo yeye alikuwa tofauti na waliotangulia, alikuwa mwanaume msumbufu ambaye sikukubaliana naye. Baada ya kuondoka nikiwa bado nimejilaza katika vazi la kanga moja Bi Shuu aliingia chumbani kwangu kama askari aliyevamia chumba cha jambazi. Sikushtuka niligeuza shingo na kumtizama, mama mtu mzima asiye na haya wala kujua vibaya kunigeuza kitega uchumi chake. Japo alinisaidia vitu vingi kama chakula na matumizi madogo madogo ninapokwama kipindi kila nilipoacha kazi bila kujua hatima ya maisha yangu. Akiwa amenisimamia pembeni ya kitanda changu kama jini la kutumwa huku akinikata jicho kali ambalo hakuwahi kulionesha kwangu. Nilijikuta nikishtuka na kujiuliza kulikoni kuniijia kama shetani wa kutumwa. “Manka,” aliniita jina langu. “Abee.” “Unataka msaada gani kwangu?” “Upi huo?” nilimuuliza huku nikaa kitako. “Kila kijana ninayemleta kwako anaondoka bila kuaga tatizo nini?” “Kwani wao wamekueleza nini?” “Hakuna hata mtu wa kuelezea kitu zaidi ya kuondoka bila kuaga, kwani kuna tatizo gani?” “Kwangu sina, labda wao.” “Kwa mtindo huu, hali itakuwa ngumu si muda utageuka mzigo wa moto usioshikika wala kubebeka.” Mmh! Nilijua nimenyea kambi, nilijiuliza kama Bi Shuu kama ataniona mzigo sikujua nitakwenda wapi. Kurudi Arusha sikuwa tayari, kuendelea kulipiwa chumba na shoga yangu niliona aibu baada ya kujitoa kwake, lakini ningefanya nini katika mji wa watu. “Kwa mtindo huo kuanzia mwezi ujao utalipa kodi,” Bi Shuu aliniambia kwa sauti kavu. “Bi Shuu, nitatoa wapi pesa za kodi nami kazi sina.” “Kazi huna au hutaki kazi.” “Kazi za kudhalilishana hata siwezi.” “Kipi cha ajabu dunia ya leo, Mungu amekupa vitumie.” “Navitumia lakini sina bahati.” “Basi habari ndiyo hiyo, mwezi ujao utalipa kodi, la huna rudisha chumba changu.” “Bi Shuu, lakini si wewe ndiye uliyemkataza shoga yangu kuwa aache kulipia kodi nitaishi nawe kama mwanao?” “Mwanangu gani asiye na msaada, mimi na mzee wangu ninatulia na mwanaume akionja lazima arudie na akimaliza sharti ajilambe.” “Sasa mimi nimekataa mwanaume gani, wenyewe ndiyo wananikataa.” “Basi utakuwa na kasoro ambayo unaificha, lakini nitaijua muda si mrefu.” Bi Shuu alisema huku akitoka nje, nilibakia nimejilaza kitandani nikiwa na mawazo mengi juu ya mapungufu yangu kwa wanaume, kufikia hatua kila mwanaume akionja harudii tena. Kingine kilichonichanganya ni kulipa kodi na kazi sina, nilishangaa Bi Shuu kunigeuka kama kinyonga. Nikiwa katikati ya mawazo nilisikia hodi ikigongwa chumbani kwangu. “Pita mlango u wazi,” nilipaza sauti kumruhusu anayegonga aingie. Mlango ulifunguliwa na mtu aliingia, ha! Kumbe alikuwa shoga yangu Mage. “Aah, Mage umenikumbuka leo.” “Ni kweli Manka, vipi mbona ka.a.maaa?” Nilijua kuna hali ilimfanya aingie wasiwasi, nilishukuru Mage hakumkuta yule mwanaume alikwisha nionya nisikubali kuugeuza mwili wangu kitega uchumi na kunieleza ninapozidiwa kimaisha nikimbilie kwake. Lakini niliona aibu motto wa kime niliye kamilika kuomba kwa mtu kila siku. “Hamna kitu, nilikuwa nataka kwenda kuoga,” nilidanganya. “Ni hivi shoga yangu, shemeji yako amekupatia kazi kwenye kampuni moja kama secretary, si bado unakumbuka kutaipu kwa computer?” “Mmh muda, lakini sijasahau, labda wepesi.” “La muhimu uipate hiyo kazi, mengine yatajulikana humo humo.” “Nitashukuru shoga yangu.” “Na kazi yenyewe ni kesho asubuhi jiandae shemeji yako atakupitia, kesho asubuhi na kukupeleka kwenye hiyo kazi kisha atakwenda kazini kwake.” “Nashukuru shoga yangu kweli wewe ni ndugu wa damu” Nilimkumbatia Mage huku nikimuomba Mungu asitokee mwanaume atakaye nitaka kimapenzi. Niliamini hata kama nitamkataa huo utakuwa mwanzo wa kuchukiwa na mwisho wa siku kufukuzwa kazi. Lakini nilimuomba Mungu kabla ya kuianza hiyo kazi, aniepushe ni matamanio ya wanaume japo kila vazi nililovaa liliwaweka katika wakatii mgumu wanaume. Lakini nilimuomba Mungu usiku na mchana ili aniepushe na mataanio ya wanaume. &&&& Japo nilikuwa na furaha ya kupata kazi kwenye ofisi, lakini bado moyo wangu ulikosa raha kutokana na kuwa na bahati ya kupendwa lakini mkosi wa kuachwa. Lakini nilijipiza moyoni kuwa na msimamo wa kutojirahisi kwa wanaume yoyote.
ITAENDELEASIKU YA KESHO

Post a Comment