BONGO MUVI WACHAFUKA! KISOMO CHA KUWAOMBEA MASTAA WALIOFALIKI
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Na: Gladness Mallya na Imelda Mtema JAMBO
limezua jambo! Baada ya hivi karibuni wasanii wa Bongo Muvi (Movie)
kufanya dua kwa ajili ya wenzao waliofariki dunia, baadhi ya ndugu wa
marehemu wamecharuka na kudai kuwa waandaaji wa kisomo hicho walifanya
kwa manufaa yao binafsi.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa marehemu wanalalamika
kuwa dua hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’ na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini
Dar, ilikuwa ni kwa ajili ya kujipatia fedha yeye ndiyo maana hakuona
haja ya kuwashirikisha.
“Dua ilifanyika lakini baadhi ya ndugu wa
marehemu hawakuambiwa na wanalalamikia sana kitendo hicho kwani si cha
kiungwana, kimsingi mamilioni waliyopewa na mdhamini wa shughuli
yametumika vibaya,” kilidai chanzo hicho bila kueleza fedha hizo
zimepatikana wapi.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza jambo.
Baada ya malalamiko hayo kutua mezani, mapaparazi wetu waliwatafuta
ndugu wa marehemu ambao hawakuonekana kwenye dua hiyo ambapo walifunguka
kwa nyakati tofauti:
MKE WA MZEE SMALL
Bi. Fatuma Said ambaye ni mke wa aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ alisema kwamba hawakupewa taarifa wao kama familia jambo ambalo limemsikitisha sana.
Bi. Fatuma Said ambaye ni mke wa aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ alisema kwamba hawakupewa taarifa wao kama familia jambo ambalo limemsikitisha sana.
Aliyekuwa mke wa muongozaji wa filamu Bongo(George Otieno Tyson) Beatrice Shayo.
“Imeniuma kwa kweli kwani sisi wajane tunatengwa sana, yaani wasanii
wakishazika hakuna anayerudi nyuma tena, kitendo cha kutokututaarifu
kuhusu dua kimeniumiza sana jamani tungepewa tu taarifa,” alisema
Fatuma.
BEATRICE SHAYO ‘MKE WA TYSON’
Huyu ni mwanadada aliyekuwa mke wa marehemu, George Otieno ‘Tyson’ ambaye naye alikiri kwamba hakuwepo kwenye dua kwa sababu hakuwa na taarifa.
Huyu ni mwanadada aliyekuwa mke wa marehemu, George Otieno ‘Tyson’ ambaye naye alikiri kwamba hakuwepo kwenye dua kwa sababu hakuwa na taarifa.
Aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ enzi za uhai wake.
“Sikujisikia vizuri na imeniuma sana kwani sikujua inafanyika wapi na
imeandaliwa na nani, ukweli walioandaa hawakufanya vizuri kwani
walipaswa kutushirikisha sisi wahusika ili tuwe kitu kimoja, sasa
nashangaa walifanyaje dua wakati ndugu na jamaa wa marehemu hawana
taarifa?” alisema Beatrice.
MAMA SHARO
Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ ambaye alisema kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu dua na ndiyo alisikia kutoka kwa mwandishi.
Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ ambaye alisema kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu dua na ndiyo alisikia kutoka kwa mwandishi.
“Ndiyo nasikia kwako, ukweli nimeumia kutokupewa taarifa kwani
ningejumuika na mimi kwa ajili ya kumuombea mwanangu, naona wamenitupa
na kunisahau kabisa, wasanii msiwe mnanitenga hivyo jamani!” alisema
Mama Sharo.
Aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ enzi za uhai wake.
SETH BOSCO
Ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba ambaye alitafutwa baada ya simu ya mama Kanumba kuita bila kupokelewa ambapo alisema wao kama familia hawakupewa taarifa ndiyo maana hawakuonekana kwenye dua hiyo jambo ambalo limewahuzunisha.

“Aliyeandaa dua hiyo hakufanya jambo la kiungwana, tumejisikia vibaya
sana kwani suala kama hilo walitakiwa kuwafuata wahusika na kuwaalika
tena ikiwezekana washirikiane kwa pamoja lakini walifanya kwa ajili ya
kujipatia fedha tu hakuna chochote,” alisema Seth.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
MSIKILIZE RAIS
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba alilaani vikali kitendo hicho na kusema waandaaji hawakufuata utaratibu.
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba alilaani vikali kitendo hicho na kusema waandaaji hawakufuata utaratibu.
“Walitakiwa kuwashirikisha wahusika na mazingira haya tata ndiyo
maana maswali yanakuwa mengi vinywani mwa watu kwamba hakikuwa kitu
chema na cha uungwana,” alisema.
NYERERE SASA!
Akizungumza muandaaji mkuu wa shughuli hiyo, Steve Nyerere alisema wahusika wote walipewa taarifa japokuwa aligawana majukumu na watu wengine kwani asingeweza kuwafikia wote.
Akizungumza muandaaji mkuu wa shughuli hiyo, Steve Nyerere alisema wahusika wote walipewa taarifa japokuwa aligawana majukumu na watu wengine kwani asingeweza kuwafikia wote.
“Sisi tuligawana majukumu na nilituma watu kwa wahusika sasa kama
hawakuwa na taarifa siyo kosa langu ni la kwao hao niliowapa hilo
jukumu, hatukufanya shughuli ile kwa masilahi binafsi zaidi ya
kuwakumbuka ndugu zetu,” alisema Steve pasipo kufafanua zaidi.
CREDIT: GPL

Post a Comment