ad

ad

UKAWA wakutana na waandhishi wa habari jijini Dar leo



Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa Tamko kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na wa pili kulia ni Mwenyeti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa.


Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono kuashiria umoja mara baada ya kuongea na wandishi wa habari kutoa Tamko la Ukawa kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi,Mosena Nyambabe,Mwenyekiti wa Chadema,Mh.Freeman Mbowe ,Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa wakiwa nje ya makao makuu ya cuf.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),umesema umesikitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa dini zilizotolewa wakati wa baraza la Iddi za kuwataka warejee katika bunge maalum la katiba huku viongozi hao wakinyamaza bila ya kukemea matendo yaliyosababisha wajumbe wa umoja huo kususia vikao vya bunge hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa umoja huo, Mwenyekiti wa chama cha wananchi-CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema UKAWA wanatambua kuwa viongozi wa dini ni watu wenye heshima na nafasi ya pekee katika jamii, hivyo wana kila sababu ya kuheshimu miito na ushauri wao.

Prof. Lipumba amesema hayo leo jijini Dar e s salaam wakati viongozi wa UKAWA walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko kuhusu miito ya viongozi wa dini kuwataka kurejea kwenye bunge maalum la katiba Jumanne ijayo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amesema kuwa anasikitika kuona kauli za viongozi mbalimbali wa CCM pamoja na Serikali wakitoa matamko ambayo hayaashirii kutafuta muafaka.

Aidha Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi Jemes Mbatia amesema ipo haja ya serikali kuangalia namna ya kuboresha sheria ya uchaguzi ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi mwakani kutokana na dalili zilizopo ni dhahiri kuwa katiba mpya haiwezi kupatikana katika kipindi kilichopangwa.

UKAWA wamedai kuwa waliamua kuondoka bungeni ili kupinga njama zilizokuwa zikifanywa na wajumbe wa chama cha Mapinduzi za kuhujumu mchakato wa katiba mpya, kupinga kauli za kejeli, lugha za ubaguzi, uchochezi na matusi, pamoja na kile walichosema ni kushindwa kwa mwenyekiti wa Bunge hilo kuwadhibiti wajumbe wanaokiuka kanuni


No comments

Powered by Blogger.