Ubeljiji 2-1 Marekani
Mfungaji bao la Ubeljiji Lukaku
Mabao ya muda wa ziada ya
Kevin de Bruyne na mchezaji wa akiba Romelu Lukaku yaliwezesha
Ubeljiji kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la dunia timu hiyo
ilipoilaza Marekani mabao 2-1 huku Salvador Brazil.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ubeljiji kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali baada ya kipindi cha miaka 28 .
Kipa wa marekani Tim Howard
alitajwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo kufuatia mchezo mzuri
aliodhihirisha kwa kuokoa mikwaju tele kutoka kwa vijana wa Marc
Wilmots .
Tineja mshambulizi wa Lille mzaliwa wa Kenya
Divock Origi alianza katika mechi hii badala yake Lukaku na alichangia
katika mashambulizi ya lango la Marekani kwa ushirikiano na Jan
Vertonghen na De Bruyne.
Hata hivyo kocha Jurgen Klinsmann alilazimika
kufanya mabadiliko baada ya Fabian Johnson, kujeruhiwa na nafasi yake
ikachukuliwa na DeAndre Yedlin.
Marekani pia walipoteza nafasi nyingi ya kushinda mechi hiyo Chris Wondolowski alipopiga nje pasi yake Jermain Jones.
Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kufikia mwisho wa muda wa kawaida matokeo yakiwa ni 0-0 .
Lakini punde baada ya kuanza kwa muda wa ziada De Bruyne alichonga mkwaju wa Lukaku na kumwacha Howard ameduwaa.
Ubeljiji itachuana na Argentina
Lukaku mwenyewe aliihakikishia ubeljiji tiketi
ya robo fainali alipofunga bao la pili kunako dakika ya 15 ya kipindi
cha ziada na kutokea hapo Ubeljiji wakarejea nyuma kulinda ngome yao.
Labda hatua hiyo haikuwa nzuri sana kwani iliiruhusu Marekani kushambulia lango lao kila walipopata mpira .
Juhudi zao vijana wa Klinsmann zilizaa matunda
Green alipofuma kimiani pasi ya Michael Bradley na kuipa marekani
matumaini ya kufufua kampeini yao .
Marekani iliendeleza wimbi baada ya wimbi la
mashambulizi wakitafuta bao la kusawazisha lakini wapi muda ulikuwa
umekwisha na hivyo sasa wakalazimika kuyaaga mashindano hayo.
Ubeljiji sasa watachuana na Argentina jumamosi
ya tarehe 5 julai katika mechi ya Robo fainali kwa mara ya kwanza katika
miaka 28.
Argentina ilijikatia tikiti ya kushiriki robo fainali hiyo baada ya kuilaza Uswisi 1-0.

Post a Comment