TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 09
“Wee acha, mimi bonge la fala.”
“Bonge la fala! Una maana gani?”
“Yaani nimefanya bonge la mistake.”
“Mistake gani tena, umeibiwa?”
“Hapana.”
“Umefanya kosa gani lililokuchanganya?”
“Si yule demu.”
“Eeh! Kafanya nini?”
“Si nimekutana naye na kunipa namba ya simu, bahati mbaya nilisahau kuisevu, uliponipigia ikafutika kutoka nje nimemkuta ndo anaishia.”
“Sasa tatizo nini?”
“Si kaniambia nimpigie simu kesho, sasa akikosa simu yangu si ataniona miyeyusho hata kunipiga chini mtu anayeutesa moyo wangu.”
“Kwani somo si kalielewa?”
“Ndiyo.”
”Sasa tatizo nini?”
“Wasiwasi wangu atasubiri simu akiikosa atanidharau.”
“Kwao si unapojua?”
”Ndiyo.”
“Basi kesho mtilie timu kwa vile umesema mtu wake mchovu chukua gari lolote mwibukie tumia kiasi chote cha fedha. Kesho nitakuongezea nyingine ili kukuhakikishia rafiki yangu na wewe unafurahia maisha.”
“Zile ulizonipa nimempa zote sijui itakuwaje?”
“Achana nazo tayari samaki kala chambo wewe kazi yako kumvuta tu tena hutumii nguvu.”
“Yaani bila wewe nilikuwa nimeisha changanyikiwa.”
Shuku alinyanyuka na kuelekea kwenye gari ili warudi nyumbani.
Wakiwa njiani Shuku alionekana kujifyonza mwenyewe kitu kilichomfanya MJ amuulize rafiki yake.
“Vipi Shuku mbona sikuelewi?”
“Wee acha tu.”
“Si tumezungumza, ni hilohilo au kuna lingine?”
“Leo nimefanya ujinga wa mwaka.”
“Shuku acha ushamba huyo demu wako yupo vipi kiasi cha kukuchanganya kiasi hicho?” MJ alimshangaa rafiki yake kudatishwa na demu.
“Siyo demu bali ujinga niliofanya wa kutosevu namba, mfano kama nisingekuwa najua anapoishi si ingekuwa imekula kwangu.”
“Ile kwako kivipi kwani watoto wazuri wamekwisha, hii ndiyo tabu ya kutotembea matokeo yake umekuwa kama kipofu aliyeona kwa bahati mbaya kila kitu akiambiwa huamini akifanani na kile alichokiona.”
“Huwezi kuamini MJ mi si mtu wa mademu lakini yule demu nimejikuta kanichanganya hata sijielewi.”
“Mmh! Haya siwezi kuingilia utashi wa moyo wako.”
Walipofika nyumbani MJ alimkuta mtu wake aliyempigia simu. Kwa mara nyingine Shuku alishuhudia msichana mwingine wa nguvu akiwa anamsubiri Mj. Alipomuona walikumbatiana na mabusu mengi.
“Baby kidogo nikufuate nilijua nitaibiwa,” alilalamika mtoto wa kike ambaye alikuwa na umbile dogo lakini mzigo msalie mtume.
“Hakuna baby unaniona kicheche siyo?” MJ alijitetea na kumfanya Shuku ajiulize anawezaje kutembea na wanawake wengi kiasi kile bila kufumaniana na wote huja nyumbani kwake bila taarifa.
Walipoingia chumbani kwao Shuku naye alikwenda kulala, siku ile hakutaka kuangalia filamu kama ilivyo kawaida yake. Kufutika kwa namba katika siku yake kulimnyima raha sana.
(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','//www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-50361043-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); /> *****
Siku ya pili Shuku aliwahi kuamka na kujiandaa kumfuata yule demu aliyemchanganya. Baada ya maandalizi yote alimfuata MJ chumbani kwake, baada ya kugonga kwa muda MJ alitoka kajifunga taulo. Baada ya kufungua mlango na kumkuta rafiki yake alimuuliza akifikicha macho.
“Vipi mzee?”
“Poa.”
“Mbona asubuhi asubuhi? Halafu umeulamba safari ya wapi, kanisani?”
“Si kwa yule demu.”
MJ alijikuta akicheka mpaka machozi yakamtoka na kumfanya Shuku ashtuke na kumuuliza rafiki yake.
“Unacheka nini sasa?”
“Kweli rafiki yangu umepania.”
“Si unajua leo jumapili anaweza kwenda sehemu ikawa tatizo na yeye anajua nitampigia simu.”
“Mmh! Haya kaka ulikuwa unasemaje?”
“Nataka gari?”
“Unataka gari gani?”
“Utakalonipa.”
“Shuku hebu acha kujishusha, nimekueleza humu ndani wewe si mgeni chukua chochote unachotoka sitaki mtu ajue hii mali ni yangu kuanzia leo mali yangu ni yako.”
“Nimekuelewa best.”
“Funguo zipo kwenye kabati.”
“Poa wacha niwahi huenda akaenda kanisani.”
“Kumbe demu wako ni mkristo?”
“Hata najua.”
“Kwani anaitwa nani?”
“Ndugu yangu wee, hata nilikumbuka kumuuliza jina lake.”
“Kweli umechanganyikiwa mpwa wangu.”
“Wee acha tu,”
“Sijui ukimpata itakuwaje?”
“Lazima nitangaze ndoa.”
“Acha ushamba, kula raha wewe, huwezi kukimbilia kuoa watoto wazuri kama hawa utamuachia nani.”
“Ngoja nimpate nitajua yote.”
“Unaweza kumpapatikia kumbe si mali kitu utafanya nini?”
“Tutayajua yote nikimtia mkononi.”
Baada ya mazungumzo ambayo Shuku aliona kama yanamchelewesha kwa kurefusha maneno, aligeuka ili aondoke MJ alikumbuka kitu.
“Una fedha ya kutosha?”
“Sina hata senti tano.”
“Zote nilizokupa umezifanya nini?”
“Si unakumbuka nilikuambia nimempa zote yule demu.”
“Ooh! Sorry, nilisahau, subiri,” MJ alisema na kurudi ndani, baada ya muda alitoka na fedha mkononi na kumpa Shuku.
Shuku alipokea na kushukuru kidogo amlambe miguu.
“Asante sana rafiki yangu.”
“Kawaida usijali huu ni mwanzo nataka usahau shida zako.”
“Nashukuru wacha niwahi.”
“Kama zikipungua nijulishe nikutumia kwenye akaunti ya simu yako.”
“Hakuna tatizo.”
“Kwa fedha niliyokupa mnaweza kwenye hoteli yoyote kubwa jijini na kula chochote na msiimalize.”
“Asante, wacha niwahi.”
“Wahi mzee nakuona una ugwadu naye usije ukachemsha si unajua mkamia maji.”
“Haya lazima niyanywe hata kwa dilip.”
“Teh teh teh.. haya baba kila la heri,” kauli ya Shuku ilimchekesha MJ.
Shuku alitoka nje na kwenda kuchukua gari la kufunuka juu ambalo alilipenda sana. Akiwa amepiga pamba za kweli na kamba nzito kifuani aliondoka na gari kuelekea Temeke Mikoroshini kwa yule demu aliyemdatisha kichizi.
Shuku aliendesha gari hadi Temeke Mikoroshini eneo analoishi yule msichana. Alipokaribia pale aliendesha gari taratibu huku akipepesa macho kuangali nyumba aliyomuona akiingia yule msichana siku ya kwanza akichota maji .
Akiwa bado aking’aa macho kwenye nyumba ile macho yake yalitua kwa msichana mmoja aliyekuwa anatoka kuchota maji akiwa amevaa dela lililokuwa limechomekwa kwenye nguo ya ndani na kufanya umbile ya nyuma kuonekana huku likipishana kama wasafiri wa mbagala wakigombea kuingia kwenye daladala muda wa jioni.
Shuku alitabasamu moyoni baada ya kumtambua kumbe ni yule msichana aliyemfuata na kujisemea moyoni. “Nitafaidi” alimuona akikaribia kuingia kwenye geti la kwao. Alipiga honi lakini yule msichana hakugeuka aliingia ndani, alisogeza gari na kwenda kulisimamisha sehemu ambayo alimuona Sharobaro anayemchukua yule demu akilisimamisha siku alipomfuata.
Alilifungua gari na kuwa wazi kumsubiri akitoka, kama asingetoka ingebidi amtume mtu amfuate. Alitoka nje ya gari na kulikalia kwa mbele mguu mmoja ukiwa chini na mwingine umekanyaga mbele ya gari.
Akiwa ananyanyua macho alipokuwa akiangalia simu yake, alimuona yule msichana akiwa na ndoo mkononi akielekea bombani. Shuku alimshtua:
“Psiiii,” yule msichana aligeuka na kumtazama lakini hakumtambua, aligeuka kuendelea na safari yake,Shuku alirudia tena kuita.
“Psiiiiii.”
Yule msichana alisimama tena na kugeuka kisha alijishika kifuani na kuuliza.
“Mimi?”
“Ndiyo.”
Yule msichana alirudi taratibu akiwa amemkazia macho mtu ambaye alionekana anazo kutokana kulipuka kwa pamba pia mkoko wa nguvu. Alipomkaribia alimgundua Shuku, alishtuka na kuitupa ndoo kisha alikimbia hadi aliposimama huku akipiga kelele na kwenda kumvamia.
“Wawooo baby,” alimkumbatia kwa nguvu na wote kulalia gari.
“Jamani baby ndiyo nini kunitesa mwenzio yaani nimesubiri simu yako kama wokovu?”
“Wee acha tu.”
“Niache nini baby, nilijua labda umenitosa.”
“Nikutose mtoto mzuri kama wewe?”
“Sasa mbona hujanipigia simu.”
“Nilitaka nikufanyie Surprise.”
“Mmh! Asante, umejuaje ninapokaa?”
“Huwezi kuamini nakupenda muda mrefu, nimekufuatilia muda mrefu.”
“Jamani baby, mi sitaki, mbona hukuniambia zamani au sikukuvutia siku za nyuma?”
“Walaa, nilijua nimewahiwa, wasiwasi wangu yule mchovu amekuoa sikupenda kuingilia ndoa yako.”
“Kipi kilichokufanya unitokee?”
“Aah! Nilimuona jamaa mwenyewe mchovu hata kiganjani hajai.”
“ Kweli baby yaani hata usafiri wako si wa kawaida.”
“Tuachane na hayo, nimekufuata.”
“Kweli baby?”
“Sikutanii kama upo tayari tuondoke nikakupe maisha ya ndotoni.”
“Mbona asubuhi sana baby?”
“Au baby una safari nyingine?”
“Walaaa,” mtoto wa kike aliruka kimanga.
“Basi baby nipendapo huwa sina subra.”
“Mmh! Haya, basi nakuja,” yule msichana alirudi ndani, safari ya kwenda bombani ilikufa.
Shuku aliingilia kwenye gari na kufungulia muziki kwa sauti ya juu kidogo. Kila mtu alivunja shingo kumuona tajiri mtoto. Ilikuwa ni vigumu kumwambia mtu huyo siku mbili zilizopita alikuwa hajui kula yake na kuishi maisha ya kubahatisha alitembea kwa miguu miguu imempauka asingekubali hata kwa mtutu.
Shuku akiwa na simu yake ya bei mbaya muda wote alijifanya yupo bize na simu yake ili tu kuwakonga watu mtaani ambao walimtazama kwa jicho la matanio. Shuku alijiuliza mtoto mzuri kama yule ampe machejo gani ili akigusa anase asitoke tena.
Moyoni alijiapiza kumaliza utundu wote anaoujua na asioujua ili kuhakikisha anagawa dozi maridhawa itakayomfanya mtoto wa kike kila akimkumbuka basi ampigie simu. Wazo la kumpeleka nyumba hakukubaliana nalo.
Aliamini kwa vile alikuwa na mshiko wa nguvu alitakiwa ampagawishe ili hata jamaa akija ampe kibuti cha nguvu. Akiwa ameinama alishtushwa na sauti tamu.
“Sweeeti.”
Shuku alinyanyua macho na kukutana na mtoto mrembo, siku ile alipendeza mara dufu. Binti alikuwa amevaa gauni fupi la rangi ya papo lililoishia chini kidogo ya makalio lenye mkono mmoja na upande mwingine bega lilikuwa wazi juu alivalia wigi liliongeza uzuri wake na chini alivaa viatu virefu vyenye rangi sawa na gauni lake.
Begani alikuwa amebeba mkoba mdogo mwenye rangi sawa na gauni. Aliachia tabasamu pana na kuonesha meno yake madogo kama mahindi ya bisi yaliyonakshiwa na mwanya mwembamba. Midomo yake ilipambwa na rangi ya midomo inayofanana na gauni na kumfanya apendeze zaidi.
“Wawooo, kweli najua kuchagua, wewe ni mwanamke mzuri kuliko wote walio chini ya jua.”
“Asante baby wangu.”
Shuku bila kujielewa baada ya kuchanganywa na uzuri wa mrembo yule alijikuta ameteremka kwenye gani na kwenda kumlaki mrembo ambaye mpaka muda ule hakulijua jina lake na kumpokea kama malkia. Alimshika mkono na kuingia naye ndani ya gari.
“Karibu malkia wangu.”
“Asante mfalme wangu,” binti alijibu kwa sauti ya kudeka huku akiketi kwenye kiti kwa mbwembwe.
Shuku alikaa upande wake kabla ya kuondoka alilifunika gari kwa juu na kumfanya yule mrembo kushtuka.
“Wawooo, baby sikuwezi upo juu.”
“Kawaida tu haya ni mambo madogo.”
Baada ya kufungua kiyoyozi na kuwasha muziki kwa sauti ya chini tofauti na mwanzo alifungua muziki wa matangazo. Alimgeukia mrembo na kumsifia:
“Hongera mpenzi umependeza sana.”
“Asante, na wewe pia baby wangu hongera umependeza.”
“Asante,” Shuku alisema huku akimbusu na kuondoa gari
“Asante baby, yaani busu lako limenisisimua sijui mambo yatakuwaje?”
“Kawaida tu, mmh, niambie unataka twende hoteli gani ambayo unaamini tukipumzika leo utafurahi.”
“Yoyote?”
“Yoyote ile ambayo unaamini tukipumzika leo moyo wako utakuwa kwatu.”
“Mmh! Unajua mimi na ujanja wangu sijalala hoteli ya Serena zamani Royal. Lakini naona kama ya gharama sana, ungechagua yoyote baby kwangu sawa.”
“Babiii utaniangusha, nimekueleza fedha si tatizo bali matumizi.”
“Basi Serena baby.”
Shuku aligeuza gari na kuelekea katikati ya jiji kula raha na mrembo. Walipofika Serena hoteli walipaki gari kwenye maegesho na kuingia ndani kwa mwendo wa madaha kama wapenzi wa muda mrefu. Shuku akijifanya kujichelewesha nyumba ili aweze kuzisanifu sehemu za nyuma za binti mrembo. Kila alivyotembea mtikisiko wa nyuma ulizidi kumuacha hoi huku akijiuliza ndani itakuwaje wakati wa hukumu ya kisu na nyama.
Msichana naye baada ya kujua sababu ya kutangulizwa aliongeza manjonjo ya kulegeza makalio ambayo yalizidi kutetemeka kama yamemwagiwa maji baridi usiku wa manane.
Shuku alijisahau na kusimama akishika mikono kiunoni kumtazama binti mrembo na kutikisa kichwa na kunyanyua mikono juu kumshukuru Mungu kwa utundu wake. Binti mrembo baada ya mwendo mfupi aligeuka nyuma na kumkuta Shuku akimshukuru Mungu.
“Babiii vipiiii mbona huji?”
“Nakuja mpenzi.”
Shuku alichepua mwendo hadi alipokuwa amesimama mrembo na kumshika kiunoni hadi mapokezi.
“Karibuni wapendanao,” msichana wa mapokezi aliwakaribisha.
“Asante, habari yako?” Shuku alimsalimia mfanyakazi wa mapokezi.
“Nzuri tu kaka yangu, karibuni sana.”
“Asante, tunahitaji chumba.”
“Vipo, unataka cha daraja lipi?”
“Cha daraja la juu.”
“Daraja la juu ni VIP.”
“Ndicho hichohicho ninachokitaka.”
“Mmh! Lakini unajua bei yake?”
“Tatizo bei au kulipata chumbani?”
“Si kulipia chumba bali kutumia fedha nyingi wakati kuna vyumba vizuri ambavyo vya daraja la kati unavyoweza kuinjoi na wifi yangu. Vyumba kama hivi hulala wageni kutoka nje kama marais na watu wazito.”
“Samahani dada yangu, hivi hapa Dar kuna hoteli nyota tano ngapi?”
“Zipo nyingi.”
“Kwa nini nimekuja hapa?”
“Kwa sababu umeipenda hoteli yetu.”
“Na kwa nini nimechagua chumba cha VIP?”
”Sijui, lakini wasiwasi wangu labda ulidhania bei yake ni ndogo, hivyo sikupenda Mtanzania mwenzangu kutumia fedha nyingi bila sababu.”
“Hebu nipe menu niangalie.”
Dada wa mapokezi alimpa Shuku menu ambayo aliingalia bei ya vyumba na kusema:
“Mbona fedha kidogo hata ingekuwa mara tatu yake ningelipa,” Shuku alijitapa mbele ya mrembo.
“Hebu baby.”
Mrembo alichukua na kuitazama na kushtuka lakini hakuonesha mshtuko wake na kuona tofauti ya nyumba za wageni wa uswazi na za anga za wakubwa.
Shuku alitoa kiasi cha kulipia chumba, baada ya kuandikisha walielekezwa chumba kwa kupelekwa na mhudumu. Baada ya kuingia ndani mrembo alifurahi sana kuona bonge la chumba ambalo hakuwahi kuingia katika maisha yake yote.
“Wawooo baby hii ya leo umenifanyia bonge la surprise.”
Mrembo alisema huku akimkumbatia Shuku.
“Kawaida tu baby hivi vitu vidogo sana kwangu.”
Shuku alijikweza wakati na yeye ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kuingia kwenye chumba kama kile. Shuku alimbeba juujuu hadi kwenye kitanda cha nguvu na kutua.
“Yaani baby siamini kuingia na kulala kwenye hoteli na chumba cha gharama kama hiki.”
“Mbona mambo madogo tu jiandae kula raha zaidi ya hizi.”
“Kwa nini usinioe kabisa?”
“Ni haraka sana kula kwanza raha mambo mengine baadaye.”
“Nakuahidi mimi Lily sitampenda mwanaume yeyote zaidi yako,” Shuku alijikuta akifahamu jina la yule mrembo kwa mara ya kwanza.
“Lily wewe tu, tulia ule raha.”
“Yaani yule mchovu anikome tena anikome.”
“Wewe mwenyewe kuamua kuishi Masaki au Tandale kwa Mtogole.”
“Baby sihami Masaki hapa nimefika sihami tena.”
” ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA
KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.
:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.
Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

Post a Comment