She is too young to die – 6
Baada ya mke wake (Salome) kuwa amekwama kijijini kwao eneo lililokumbwa na mafuriko akiwa mjamzito anayevuja damu nyingi, jambo linalohatarisha uhai wake, Gilbert (mume) anaamua kukodisha helkopta kutoka Dar es Salaam hadi kijijini ambako amemkuta mke wake akiwa amekwama kwenye daraja lililovunjwa na mafuriko, alichokifanya ni kumchukua yeye pamoja na mama yake (mama mkwe wa Gilbert) na kuondoka nao hadi hospitali ya Sengerema ambako helkopta ilitua na Salome kukimbizwa chumba cha upasuaji baada ya kugundulika kuwa tatizo linamsumbua ni Abruption Placenta (kondo la nyuma limeng’oka kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi) ambayo inasababisha damu nyingi sana kuvuja kiasi cha kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.
Uamuzi uliofikiwa ni kumwongezea Salome damu haraka iwezekanavyo, baada ya hapo ndipo atapelekwa chumba cha upasuaji ambako madaktari walifanikiwa kumfanyia upasuaji na kumtoa mtoto tumboni akiwa hai, wakati hayo yote yakifanyika Gilbert, mama mkwe wake na mwalimu Mchele walikuwa nje ya chumba cha upasuaji wakimsubiri mgonjwa wao mpaka mlango ulipofunguliwa, muuguzi akatokeza na kumwita Gilbert kumpongeza kwa kupata mtoto wa kike! Gilbert aliruka juu na kushangilia lakini ghafla alipousoma uso wa muuguzi alishtuka na kuacha kushangilia. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
“Mke wangu je?” Gilbert aliuliza alipotulia.
“Mke wako…ah…” muuguzi alijiumauma.
“Muuguzi niambie ukweli, mke wangu anaendeleaje au kapoteza maisha?”
“Hapana! Madaktari wamejitahidi sana, ni kweli hali yake si nzuri lakini bado tuna matumaini, anavuja damu nyingi mno, hivi sasa wanajitahidi kuidhibiti, tunashindwa kuelewa ana tatizo gani!”
“Sasa?”
“Inabidi muendelee kuvumilia, mtoto hivi sasa ameingizwa kwenye chumba maalum cha kuokoa maisha, anahema kwa taabu imebidi afungiwe mashine za kupumulia! Lakini tuna uhakika hali yake itakuwa nzuri!”
“Namwomba Mungu asaidie!” Gilbert aliongea.
“Hata sisi pia, sasa endeleeni kusubiri!”
“Sawa dada!”
Gilbert alishuhudia mlango wa chumba cha upasuaji ukifungwa nyuma ya muuguzi na yeye akatembea kurejea mahali alipokuwa ameketi awali, akawasimulia mama mkwe wake pamoja na Mwalimu Mchele ambaye alishatokea kuwa rafiki yake mkubwa, kila kitu alichoelezwa na muuguzi, mama yake Salome akapiga magoti chini na kuanza kusali! Haukupita muda mrefu sana mvua kubwa yenye upepo ikaanza kunyesha, kwa mbali wakaanza kushuhudia mabati yakiezuliwa lakini hawakudiriki kuondoka eneo hilo, kila mmoja akisali kimoyomoyo kumwombea Salome.
Saa nzima baadaye Gilbert akiwa amezama kwenye mawazo juu ya mke wake na mtoto, mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguliwa tena, moyo wake ukaruka mapigo kadhaa, kichwani mwake alijua hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya pengine juu ya kifo cha aidha mtoto au mke wake. Akasimama wima baada ya kumwona muuguzi aliyetokeza mwanzo na kumpa habari za kuzaliwa kwa mtoto, safari hii na kutoa sauti wakati akimwita, bali alionyesha ishara tu, Gilbert akaanza kukimbia akimfuata.
“Ndio sista!”
“Ingia ndani!”
“Kuna nini?” Aliuliza kwa wasiwasi.
“Dk. Besige anataka kuongea na wewe!”
“Juu ya nini?”
“Salome”
“Kimetokea nini?” Gilbert alizidi kuuliza maswali mengi mfululizo huku moyo wake ukidunda kwa kasi na jasho jembamba kumtoka, alikuwa katika wakati mgumu kuliko mwingine wote maishani mwake.
“Gilbert ingia tu ukamsikilize daktari!”
Kwa unyonge bila kuuliza swali jingine tena, Gilbert alianza kuvuta miguu yake kuingiza ndani ya chumba cha upasuaji, mlango ukafungwa nyuma yake! Taratibu akamfuata muuguzi mpaka kwenye chumba kilichoandikwa ‘Dr. J. Besige, consultant obstetric surgeon’ juu ya mlango ambao muuguzi aliufungua na wote wakaingia ndani, ambako macho ya Gilbert yaligongana na sura ya mzee mfupi, maji ya kunde mwenye nywele nyeupe kichwa kizima, macho yake yakionyesha hofu picha iliyomwonyesha Gilbert kwamba, mke wake alikuwa amefariki.
“Pole” ndivyo alivyoanza kusema daktari huyo mara tu Gilbert alipoketi mbele yake.
“Mke wangu amekufa?”
“Hapana, tulia kijana usiwe na shaka, nakupa pole kwa matatizo yaliyokupata, mkeo hajafa ila lazima nikueleze ukweli, tangu nianze kazi hii miaka karibu thelathini iliyopita sijawahi kukutana na mgonjwa wa aina yake, anavuja damu nyingi sana! Tumejaribu kadri ya uwezo wetu wote kuidhibiti lakini tumeshindwa, wenzangu wanaanza kufikiri labda ana matatizo katika mchakato mzima wa ugandaji wa damu au amepungukiwa Vitamini K au ana ugonjwa uitwao Haemophilia, unaufahamu?”
“Hapana!”
“Ni ule ambao mtu akijikata anaweza kuvuja damu mpaka kifo kwa sababu chembechembe zake za damu haziko sawa, kwani ana tabia ya kuvuja damu puani?”
“Hapana!”
“Sasa sijui ni kitu gani, enewei tuyaache hayo, uamuzi tulioufikia sisi ili kuokoa maisha yake ni kuuondoa mfuko wake wa uzazi, tunahitaji kufanya upasuaji uitwao Hysterectomy!”
“Nini daktari?”
“Ili kuokoa maisha ya mkeo inabidi tuuondoe mfuko wa uzazi!”
“No! Siwezi kukomea mtoto mmoja! Hata yeye Salome angekuwa na fahamu zake, hakika asingekubali hilo lifanyike”
“Vinginevyo mkeo atapoteza uhai!”
“Kwani hakuna njia nyingine?”
“Siwezi kukudanganya, tumefikiria kila namna lakini hatujapata jibu na tunataka mkeo aishi ili amlee mtoto wake! Nakushauri ukubali”
“Siwezi! Siwezi! Daktari siwezi!”
“Sasa utafanya nini?”
“Tukienda mkoani, kwenye hospitali kubwa kama Bugando?”
“Hata uende wapi kijana, jibu utakalolipata ni hilo hilo!”
“Daktari nisaidie kitu kimoja, nipatie kundi la madaktari na vifaa vya kuwasaidia mke na mtoto wangu ili tu tufike Bugando, nitalipia gharama zote ikiwa ni pamoja na posho zao lakini nifike kwenye hospitali hiyo labda kunaweza kuwa na jibu tofauti!”
“Gilbert!”
“Ndio!”
“Nakushauri kitaalam!”
“Nafahamu!”
“Kwanini usichukue ushauri wangu? Mwisho utapoteza uhai wa mkeo!”
“Naelewa lakini ndani ya moyo wangu nahisi, Salome akija kuzinduka hatafurahia uamuzi huo! Daktari…daktari…daktari, naomba uniruhusu niondoke na mke wangu kwanda Bugando, nisaidie tu madaktari na wauguzi ambao gharama zao nitachukua mimi, ninayo helkopta nje kwa hiyo nina uhakika wa kufika Mwanza haraka!”
“Sawa, lakini itabidi usaini fomu ya kumchukua mgonjwa tofauti na ushauri wa daktari, ili lolote likitokea mimi na wenzangu tusiingie hatiani!”
“Sawa daktari” Gilbert aliitikia, moyoni mwake alihisi uamuzi aliokuwa akiuchukua ulikuwa sahihi, ilikuwa ni lazima ajaribu kadri ya uwezo wake kunusuru maisha ya mke wake lakini pia kuokoa mfuko wake wa uzazi ili waweze kupata watoto wengine zaidi.
Fomu ilipoletwa aliisaini na hapo hapo taratibu zikaanza kuandaliwa, madaktari wawili na wauguzi wawili pamoja na vifaa vya kuokolea maisha na mashine maalum ya mtoto wao kupumua na kumpa joto iliingizwa ndani ya ndege, helkopta ikaruka kutoka Sengerema na kutua nje ya hospitali ya Bugando kwenye uwanja wa shule ya msingi, tayari gari la wagonjwa lilishafika kwani Dk. Besige aliwasiliana na uongozi wa hospitali ya Bugando kabla helkopta haijaruka.“Mke wangu je?” Gilbert aliuliza alipotulia.
“Mke wako…ah…” muuguzi alijiumauma.
“Muuguzi niambie ukweli, mke wangu anaendeleaje au kapoteza maisha?”
“Hapana! Madaktari wamejitahidi sana, ni kweli hali yake si nzuri lakini bado tuna matumaini, anavuja damu nyingi mno, hivi sasa wanajitahidi kuidhibiti, tunashindwa kuelewa ana tatizo gani!”
“Sasa?”
“Inabidi muendelee kuvumilia, mtoto hivi sasa ameingizwa kwenye chumba maalum cha kuokoa maisha, anahema kwa taabu imebidi afungiwe mashine za kupumulia! Lakini tuna uhakika hali yake itakuwa nzuri!”
“Namwomba Mungu asaidie!” Gilbert aliongea.
“Hata sisi pia, sasa endeleeni kusubiri!”
“Sawa dada!”
Gilbert alishuhudia mlango wa chumba cha upasuaji ukifungwa nyuma ya muuguzi na yeye akatembea kurejea mahali alipokuwa ameketi awali, akawasimulia mama mkwe wake pamoja na Mwalimu Mchele ambaye alishatokea kuwa rafiki yake mkubwa, kila kitu alichoelezwa na muuguzi, mama yake Salome akapiga magoti chini na kuanza kusali! Haukupita muda mrefu sana mvua kubwa yenye upepo ikaanza kunyesha, kwa mbali wakaanza kushuhudia mabati yakiezuliwa lakini hawakudiriki kuondoka eneo hilo, kila mmoja akisali kimoyomoyo kumwombea Salome.
Saa nzima baadaye Gilbert akiwa amezama kwenye mawazo juu ya mke wake na mtoto, mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguliwa tena, moyo wake ukaruka mapigo kadhaa, kichwani mwake alijua hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya pengine juu ya kifo cha aidha mtoto au mke wake. Akasimama wima baada ya kumwona muuguzi aliyetokeza mwanzo na kumpa habari za kuzaliwa kwa mtoto, safari hii na kutoa sauti wakati akimwita, bali alionyesha ishara tu, Gilbert akaanza kukimbia akimfuata.
“Ndio sista!”
“Ingia ndani!”
“Kuna nini?” Aliuliza kwa wasiwasi.
“Dk. Besige anataka kuongea na wewe!”
“Juu ya nini?”
“Salome”
“Kimetokea nini?” Gilbert alizidi kuuliza maswali mengi mfululizo huku moyo wake ukidunda kwa kasi na jasho jembamba kumtoka, alikuwa katika wakati mgumu kuliko mwingine wote maishani mwake.
“Gilbert ingia tu ukamsikilize daktari!”
Kwa unyonge bila kuuliza swali jingine tena, Gilbert alianza kuvuta miguu yake kuingiza ndani ya chumba cha upasuaji, mlango ukafungwa nyuma yake! Taratibu akamfuata muuguzi mpaka kwenye chumba kilichoandikwa ‘Dr. J. Besige, consultant obstetric surgeon’ juu ya mlango ambao muuguzi aliufungua na wote wakaingia ndani, ambako macho ya Gilbert yaligongana na sura ya mzee mfupi, maji ya kunde mwenye nywele nyeupe kichwa kizima, macho yake yakionyesha hofu picha iliyomwonyesha Gilbert kwamba, mke wake alikuwa amefariki.
“Pole” ndivyo alivyoanza kusema daktari huyo mara tu Gilbert alipoketi mbele yake.
“Mke wangu amekufa?”
“Hapana, tulia kijana usiwe na shaka, nakupa pole kwa matatizo yaliyokupata, mkeo hajafa ila lazima nikueleze ukweli, tangu nianze kazi hii miaka karibu thelathini iliyopita sijawahi kukutana na mgonjwa wa aina yake, anavuja damu nyingi sana! Tumejaribu kadri ya uwezo wetu wote kuidhibiti lakini tumeshindwa, wenzangu wanaanza kufikiri labda ana matatizo katika mchakato mzima wa ugandaji wa damu au amepungukiwa Vitamini K au ana ugonjwa uitwao Haemophilia, unaufahamu?”
“Hapana!”
“Ni ule ambao mtu akijikata anaweza kuvuja damu mpaka kifo kwa sababu chembechembe zake za damu haziko sawa, kwani ana tabia ya kuvuja damu puani?”
“Hapana!”
“Sasa sijui ni kitu gani, enewei tuyaache hayo, uamuzi tulioufikia sisi ili kuokoa maisha yake ni kuuondoa mfuko wake wa uzazi, tunahitaji kufanya upasuaji uitwao Hysterectomy!”
“Nini daktari?”
“Ili kuokoa maisha ya mkeo inabidi tuuondoe mfuko wa uzazi!”
“No! Siwezi kukomea mtoto mmoja! Hata yeye Salome angekuwa na fahamu zake, hakika asingekubali hilo lifanyike”
“Vinginevyo mkeo atapoteza uhai!”
“Kwani hakuna njia nyingine?”
“Siwezi kukudanganya, tumefikiria kila namna lakini hatujapata jibu na tunataka mkeo aishi ili amlee mtoto wake! Nakushauri ukubali”
“Siwezi! Siwezi! Daktari siwezi!”
“Sasa utafanya nini?”
“Tukienda mkoani, kwenye hospitali kubwa kama Bugando?”
“Hata uende wapi kijana, jibu utakalolipata ni hilo hilo!”
“Daktari nisaidie kitu kimoja, nipatie kundi la madaktari na vifaa vya kuwasaidia mke na mtoto wangu ili tu tufike Bugando, nitalipia gharama zote ikiwa ni pamoja na posho zao lakini nifike kwenye hospitali hiyo labda kunaweza kuwa na jibu tofauti!”
“Gilbert!”
“Ndio!”
“Nakushauri kitaalam!”
“Nafahamu!”
“Kwanini usichukue ushauri wangu? Mwisho utapoteza uhai wa mkeo!”
“Naelewa lakini ndani ya moyo wangu nahisi, Salome akija kuzinduka hatafurahia uamuzi huo! Daktari…daktari…daktari, naomba uniruhusu niondoke na mke wangu kwanda Bugando, nisaidie tu madaktari na wauguzi ambao gharama zao nitachukua mimi, ninayo helkopta nje kwa hiyo nina uhakika wa kufika Mwanza haraka!”
“Sawa, lakini itabidi usaini fomu ya kumchukua mgonjwa tofauti na ushauri wa daktari, ili lolote likitokea mimi na wenzangu tusiingie hatiani!”
“Sawa daktari” Gilbert aliitikia
Moyoni mwake alihisi uamuzi aliokuwa akiuchukua ulikuwa sahihi, ilikuwa ni lazima ajaribu kadri ya uwezo wake kunusuru maisha ya mke wake lakini pia kuokoa mfuko wake wa uzazi ili waweze kupata watoto wengine zaidi.
Fomu ilipoletwa aliisaini na hapo hapo taratibu zikaanza kuandaliwa, madaktari wawili na wauguzi wawili pamoja na vifaa vya kuokolea maisha na mashine maalum ya mtoto wao kupumua na kumpa joto iliingizwa ndani ya ndege, helkopta ikaruka kutoka Sengerema na kutua nje ya hospitali ya Bugando kwenye uwanja wa shule ya msingi, tayari gari la wagonjwa lilishafika kwani Dk. Besige aliwasiliana na uongozi wa hospitali ya Bugando kabla helkopta haijaruka.
Je, nini kitaendelea? Maisha ya Salome yatanusuriwa? Mfuko wake wa uzazi je?

Post a Comment