RAMADHANI YAMALIZA BIFU LA WEMA, PENNY!
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada
ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo,
Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe,
nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye
kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na
nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”
Mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila
nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa
marafiki tena kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Post a Comment