• PRIVACY POLICY
  • About 2jiachie
  • Contact us
  • What We Do

2jiachie Official Website

ad

ad
  • Home
    • Habari
    • Ajira
    • Mastaa
    • Video Mpya
    • Music Audio
    • Michezo
    • Simulizi
    • MAHUSIANO
    Home / SIASA / MAJAMBAZI 10 WANAOUNDA MTANDAO HATARI WA UHALIFU NCHINI WAMETIWA MBARONI

    MAJAMBAZI 10 WANAOUNDA MTANDAO HATARI WA UHALIFU NCHINI WAMETIWA MBARONI

    Thursday, July 31, 2014 SIASA


    MAJAMBAZI 10 wanaounda mtandao hatari wa uhalifu nchini, wametiwa mbaroni wakati wa msako mkali uliofanikisha pia kukamatwa kwa silaha mbalimbali.
    Silaha hizo ni bunduki tisa zikiwemo SMG tatu, bastola mbili, short gun nne na risasi 15 zilikamatwa.
    Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliyasema hayo ofisini kwake kwenye mkutano na waandishi wa habari.
    Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
    Katika msako huo watuhumiwa walisachiwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 9 kama ifuatavyo:-
    SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
    SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
    BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
    BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
    S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
    MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
    BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
    SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
    SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako
    Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
    1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
    2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
    3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
    4. SAID S/O FADHIL MLISI – miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
    5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
    6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
    7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
    8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
    9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
    10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilakala
    Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.
    Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.
    Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.
    Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
    Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kutafuta majalada yao ya kesi mbali mbali.
    S.H. KOVA
    KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
    DAR ES SALAAM


    Related Posts

    SIASA

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    HIZI HAPA NYINGINE ZIPITIE

    Afya Yetu Audio BURUDANI MAHUSIANO MICHEZO Magazeti Makala Mastaa Nafasi Za Kazi SIASA Simulizi VIDEO MPYA

    Featured Post

    TEMESA Yatangaza Nafasi 6 za Meneja wa Kanda, Maombi Mwisho Februari 20

      Kwa niaba ya Wakala wa Huduma za Ufundi za Umeme, Mitambo na Elektroniki Tanzania (TEMESA), Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika U...

    2JIACHIE PAGEVIEWS

    Random Posts

    Popular Posts

    • WAKAZI WA SINGIDA WAKUNWA TAMASHA LA FIESTA...PICHA ZIPO HAPA
      WAKAZI WA SINGIDA WAKUNWA TAMASHA LA FIESTA...PICHA ZIPO HAPA
       Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua...
    • PENZI LA JACKLINE WOLPER NA HARMONIZE LAZIDI KUNOGA,WOLPER AJIACHIA NA MAMA MKWE WAKE NA KUANDIKA UJUMBE MZITO
    • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Balozi Wa Tanzania Nchini Uingereza, Dkt. Asha- Rose Migiro
      Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Balozi Wa Tanzania Nchini Uingereza, Dkt. Asha- Rose Migiro
      Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Balozi wa Tanzania  nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose  Migiro kabla ya mazungumzo yao...
    • Tundu Lissu: Kwanini sikutokea Lowassa akijiunga CHADEMA?
      Tundu Lissu: Kwanini sikutokea Lowassa akijiunga CHADEMA?
      Mbunge Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa CHADEMA alikutana na ripota Fredrick Mwakikato wa TZA (millardayo.com) na kuzungumzia ishu...
    • Wema: Siasa bila kujipanga hutoki, ‘utakatwa’ tu!
      Wema: Siasa bila kujipanga hutoki, ‘utakatwa’ tu!
      Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu. Leo tunaye msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ambaye hivi karibuni alithubutu kugombea ubunge...
    • MAN UTD HAITABADILI MSHAHARA WA LUIS NANI
      MAN UTD HAITABADILI MSHAHARA WA LUIS NANI
      LONDON, ENGLAND WINGA Luis Nani ameelezwa kuwa hataongezwa mshahara kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka minne, hivyo ana hiyari ...
    • CAR FOR SALE
      CAR FOR SALE

    Top Headlines

    Recent Updated

    MICHEZO

    Created By Hit Media & Hit Media
  • Powered by Blogger.