BIEBER KULIPA FAINI YA DOLA 80,900 KWA KUMRUSHIA MAYAI JIRANI YAKE
July 9, Justin Bieber akiwakilishwa na wakili wake aliyefahamika kwa jina la Shawn Holley amehukumiwa kufanya kazi za jamii kwa muda wa siku tano ikiwa ni pamoja na kusafisha mazingira. Pia anatakiwa kumlipa jirani yake $80,900 kama fidia ya uharibifu wa nyumba yake.
Mahakama imemtaka Justin Bieber kukaa umbali usiopungua hatua 100 na jirani yake wala familia ya jirani huyo kwa kipindi cha miaka miwili na pia ahudhurie program maalum itakayomsaidia kudhibiti hasira (enger management program).


Post a Comment