BAADA YA KUTOSWA NA DAVID MOYES, WILFRIED ZAHA ATAMBA KUNG`ARA NA LOUIS VAN GAAL
WINGA
wa Manchester United , Wilfried Zaha amesema anatarajia kuwa mchezaji
wa aina aitakayo Louis Van Gaal baada ya msimu uliopita kutoswa na
aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes.
Zaha
alitoshwa na kocha Moyes na kumtoa kwa mkopo katika klabu ya Cardiff
mwezi januari kwa madai kuwa nyota huyo ana mitazamo mibaya.
Kinda
huyo mwenye miaka 21, sasa amepewa nafasi ya kuonesha uwezo wake kwa
Van Gaal na katika mechi ambayo Man United ilishinda kwa penati dhidi ya
Inter Milan, kocha huyo alimwacha Zaha mpaka kipindi cha pili ili
aoneshe ujuzi wake katika mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya kabla ya
msimu.
Van Gaal amemuambia Zaha kuwa anatakiwa kujitahidi kuwa mshambuliaji wa kati ili aingie katika mfumo wake wa 3-5-2 msimu ujao.
Zaha alisema: “Nilikuwa nacheza winga, lakini kama kocha anataka nizoee nafasi nyingine, nitafanya,”
“Sio kwamba mimi naweza winga tu, nitacheza nafasi nyingine”.
“Nimesikia anataka kuwapa nafasi
wachezaji vijana. Hiki ndicho nilihitaji tangu nimefika hapa. Nataka
kuwa mchezaji wa Man United. Natumaini kupata nafasi msimu ujao”.
Sir Alex Ferguson alimnunua Zaha januari mwaka 2013 kutokea klabu ya Crystal Palace.
SOURCE: SHAFFIH DAUDA

Post a Comment