ad

ad

Yanga yamshusha Maximo, yampa Sh milioni 230


Kocha Mbrazili, Marcio Maximo.

BAADA ya vuta nikuvute juu ya mshahara, hatimaye kocha wa zamani wa Taifa Stars, Marcio Maximo, amekubali kuinoa Yanga kwa mshahara wa dola 12,000 (Sh milioni 19.2) kwa mwezi (sawa na Sh milioni 230) kwa mwaka na tayari mkataba umeshatumwa Brazil ambapo ndipo alipo.
Championi ambalo lilikuwa gazeti la kwanza kuandika juu ya ujio wa kocha huyo kwenye kikosi cha Yanga, limepata habari za uhakika kuwa Mbrazili huyo amekubali kuifundisha Yanga kwa dau hilo kutoka dola 16,000 (Sh milioni 25) ambazo alikuwa akihitaji awali, lakini pia ada ya uhamisho wake klabuni hapo ni dola 20,000 (Sh milioni 32).
Taarifa kutoka kwa mtu ambaye anashughulikia ujio wa kocha huyo nchini, ni kuwa mara baada ya kusaini mkataba huo, maana yake ni kuwa Maximo atalipwa jumla ya shilingi milioni 262.
Kiasi hicho cha fedha kinatokana na jumla ya shilingi milioni 230 kwa mwaka ikiwa ni fedha ya mshahara, pamoja na shilingi milioni 32 ambayo ni ada ya ujio wake klabuni hapo.
“Kila kitu kinaenda vizuri na kama nilivyowahi kukwambia kuwa mkataba wake ulishatumwa, atasaini hukohuko Brazil kisha akija Tanzania anaanza kazi.
“Amekubali kiasi kisho cha mshahara na kilichobaki ni yeye kukamilisha vitu kadhaa vidogo vya mwisho-mwisho,” alisema mtoa taarifa.
Mbali na kiasi hicho cha fedha pia imeelezwa kuwa Maximo atakabidhiwa gari kwa ajili ya shughuli zake pindi atakapotua nchini pamoja na nyumba nzuri.CHANZO NI CHAMPIONI

No comments

Powered by Blogger.