TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 02
“Ooh! My Good,” Shuku alishtuka.
“Bwa mzee hizo glasi nakata kwenye hela yako.”
“Kata tu bwa nshee,” Shuku alilidhika kukatwa hela kutokana na hali iliyomtokea hakuelewa hata boksi lilivyomponyoka. Yule msichana alimtesa sana moyoni na kujikuta akishindwa kujielewa.
SONGA NAYO....
Rafiki yake yaliyekuwa karibu aliyekuwa akiona picha yote ya Shuku kuchanganywa na yule msichana alimuuliza:
“Shuku vipi?”
“Wee acha tu yule demu kanichanganya sana hata sijielewi na si kawaida yangu.”
“Tafuta ipo siku nawe utakula bata.”
“Wapi?”
“Usikate tamaa ukiwa bado unaishi, mbona mambo ya kawaida tu yale.”
“Aah wapi, tutaendelea kula kwa macho wenye fedha kila kituzuri watapata wao, majumba, magari na wanawake wazuri kama wale.”
“Maisha kibidubidu unaweza kulala maskini kesho unatumwagia maji unasahau kuna siku ulivunja glasi kwa ajili ya mrembo mmoja wakati huo wanakugombania kama mpira wa kona. Kaka fedha kama maua kila nyuki atatua.”
“Hizo ni ndoto za mchana.”
Shuku akiwa ameshindwa kabisa kuendelea na kazi macho yale yaliendelea kushuhudia mateso bila chuki jinsi yule mwanamke na sharobaro walivyojifanya wazungu kwa kuonesha mambo ya chumbani hadharani. Baada ya kuachiana msichana alikwenda upande wa uskani na mwanaume upande wa pili kisha yule mwanamke aliondoa gari kwa kasi.
Baada ya gari kuondoka eneo lile walimalizia mzigo ulikuwa umebakia kidogo kwenye gari na kulipwa fedha yao waliyokatwa fedha kwa ajili ya glasi alizovunja Shuku. Kwa vile ilikuwa bado asubuhi washikaji zake walimweleza watafute sehemu nyingine wakapige mzigo.
Lakini Shuku aliyekuwa amechanganywa sana na yule msichana aliona siku ile kwake mbaya aliamjua mfadhaiko aliopata asubuhi ile heri aende nyumbani kulala ili siku ile ipite salama. Kama kawaida alipanga akifika nyumbani lazima amvutie hisia na kuitafuta pwani ya utamu kwa mkono.
Akiwa anarudi nyumbani toka Temeke kwenda gheto kwake Buguruni kwa Mnyamani.
Alitembea huku akiwaonea wivu vijana wote wenye kutembelea mikoko ya nguvu pembeni yao wakiwa na warembo wa nguvu. Alipofika mataa ya Tazara akiwa anataka kuvuka barabara aliliona gari moja lilikuwa lipo kawaida lilipofika pale ilijifungua na kuwafanya vijana waliokuwa karibu kushangilia.
Kitendo kile kiliongeza maumivu kwa Shuku na kutamani gari lile angekuwa akilitumia yeye basi angerudi kwa yule mwanamke aliyemfanya ashindwe kujielewa. Gari lile la rangi nyekundu baada ya kufanya manjonjo lilisimama kusubiri mataa.
Shuku alipokuwa akilishangaa huku akilisogelea alishtuka kumuona mtu aliyekuwa akiendesha lile gari na kujikuta akipayuka kwa sauti.
“Ha! Mjuni.”
Yule aliyekuwa ndani ya gari aliyelipuka na mikufu na mipete ya kizungu la unga alishtuka kidogo na kujiuliza nani anayemfahamu jina la utoto ambalo toka akinyake mapene kwa kuuza unga alijiita Tajiri mtoto au MJ.
“Wee nani?” alimuuliza huku kamkazia macho.
“Mjuni ni mimi Shuku.”
“Shukuuu..John?”
“Eeh Mjuni.”
“I cant beliave my eyes, ni wewe Shuku?” Zungu hakuamini kukutana na rafiki yake walipotezana muda mrefu sana.
“Ni mimi Mjuni?”
“Ingia kwenye gari tutakwenda kuzungumza mbele ya safari.”
Shuku aliingia kwenye gari wakati huo mataa yalikuwa yanaruhusu Mjuni aliondoa gari kufuata barabara ya Mandela kuelekea Ubungo.
Gari lilitembea kwa mwendo mrefu bila mtu kuzungumza, muda wote Shuku alikuwa akimshangaa Mjuni jinsi alivyoyakatia denge maisha. Alikuwa amelipuka pamba za uhakika pia kumiliki gari la bei mbaya. Alikumbuka mara ya mwisho kuachana na Mjuni ilikuwa nyumbani kwao Mbeya baada ya Mjuni kuzamia magari yanayokwenda South kutafuta maisha. Shuku yeye baada ya kuondoka rafiki yake alikaa mwaka mmoja na kuhamia Dar kwa mjomba wake na kutafutiwa kazi katika kiwanda cha Simba Plastic akiwa kama wafanyakazi wa kutwa.
Alifanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili, kwa vile fedha aliyopata ilimtosha aliamua kuhama kwa mjomba wake na kuhamia Buguruni kwa Mnyamani aliyaanza maisha ya kujitegemea ambako alipanga chumba chake cha uani.
Kutokana na kupungua kwa kazi za uzalishaji kiwandani kwao baadhi ya wafanyakazi wa kutwa walisimamishwa kwa muda usiojulika mpaka uzalishaji utakapokuwa mzuri.
Mmoja wapo alikuwa Shuku ambaye aliamua kutafuta katika makampuni mengine lakini hali ilikuwa ileile. Yeye na washikaji zake waliosimamishwa pamoja waliamua kujichanganya kufanya kazi yoyote kupunguza ukali wa maisha.
Kila siku walikuwa wakijichanganya kila kona kila kazi iliyotokea mbele yao hawakuchagua mpaka siku alipotokewa na kimuhemuhe kile cha kuchanganyikiwa kumuona msichana mrembo ambaye aliamini hawezi kumpata zaidi ya kumla kwa macho na kumpa kasi ya kumfikisha pwani kwa mkono.
Mpaka gari linaingia ndani ya jumba la kifahari Shuku bado alikuwa katika ndoto za kumkumbuka Mjuni aliyeondoka kwenda South akiwa mwembamba lakini baada ya kurudi kaonekana mtu mwenye mwili wa fedha.
“Shukuuuu, karibu mtu wangu,” Mjuni amkaribisha rafiki yake huku akishuka kwenye gari.
“Ooh! Tumefika?” alikuwa kama mtu aliyetoka usingizini.
“Tumefika, karibu sana ndugu yangu.”
“Asante Mjuni.”
“Nitafurahi ukiniita MJ.”
“Poa MJ.”
“Basi karibu sana,” MJ alisema huku akibonyeza rimoti na mlango ulifunguka kitu kilichomuacha hoi Shuku na kuona mambo mageni kwake. Waliingia wote ndani ya jumba la Mjuni lilikuwa na kila kitu cha thamani kuonesha jamaa alikuwa amejipanga kimaisha na maisha alikuwa ameyapatia.
“Karibu sana rafiki yangu.”
“Asante sana.”
“Nimefurahi sana kukuona, nilikwenda home baada ya kurudi Bongo kutoka duniani nikaambiwa amezamia jijini. Nilishangaa kusikia umezamia Bongo badala ya nje ya nchi.”
“Ndugu yangu elimu yangu unaijua nitaweza kwenda sehemu gani, najua lugha ya asili na kiswahili tu.”
“Maisha ukifikiria hivyo utakufa bila kelele kama wafuasi wa kibwetele, mimi darasa la ngapi darasani wewe ulikuwa unaniburuza.”
“Mmh! Za siku?”
“Kama unavyoziona sasa hivi nafahamika kama umeme wa mgao hakuna mtu jijini asiyemjua MJ tajiri mtoto.”
“Mmh! Kweli unatisha siku hizi unavaa hereni wewe si ulikuwa ukisema wanaofanya hivyo mashoga?” Shuku alimuuliza rafiki yake.
“Ndugu yangu kama hujatembea utaona ajabu nimekutana na mambo ya ajabu na kuona kumbe kawaida. Kama mchungaji anaingia kanisani katoga sikio mimi nani mbele ya Mungu?”
“Lakini mila na destuli zetu hazikubaliani na utamaduni huo.”
“Kweli Shuku upo nyuma, pamoja na kuwahi jiji bado mgeni wa mambo, mbona huwashangai Wakulya wanaume wanatoga sikio na kuvaa hereni pia Wamasai wanawake wananyoa wanaume wanasuka.”
“Haya kaka umeshinda, Za siku?”
“Kama unavyoziona, vipi wewe maana nakuona umezeeka bado kijana mdogo?”
“Maisha ndugu yangu,” Shuku alimueleza maisha yake yalivyo, baada ya kumsikiliza alimuuliza.
“Ulipokuwa unakaa kuna kitu gani chako cha muhimu sana kwako?”
“Una maanisha?”
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA YA SIMULIZI HII HAPA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
:: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.
:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.
Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.
TUKUTANE HAPA SIKU YA KESHO

Post a Comment