TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA
TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA.
A. UTANGULIZI
Ndugu wanahabari.
Mbele yenu ni viongozi halali wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutoka mikoa yote ya Tanzania kwa uchache tumekutana jumla ya wajumbe 78 kuwakilisha wenzetu walioshindwa kufika kwa sababu mbalimbali.
Sisi
ni wajumbe wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chama ambapo pamoja nasi
tumejumuika na wenyeviti wa mabaraza ya WANAWAKE WA MIKOA YA TABORA NA
SINGIDA, MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TABORA pamoja na MUASISI WA
CHADEMA kutokea mkoa wa SINGIDA na mwenyekiti wa M4C wilaya ya
SINGIDA hivyo tunafanya jumla ya tuliokutana kwa jambo hili kuwa ni
wanachadema 82.
Tumewaita kuwaeleza
namna ambavyo tumekuwa tukisononeshwa na mwenendo wa chama chetu kwa
kipindi kirefu sasa, hivyo tunaomba mtusaidie kuufikishia umma mawazo ya
wanachadema tunaowawakilisha huko mikoani tutokapo.
B. KUSHINDWA KWA UONGOZI WA KITAIFA.
Tunasikitika kuona kwamba kadri siku zinavyoenda Uongozi wa juu wa chama unazidi kushindwa kufanya kazi ya kukiimarisha chama.
Baada
ya jitihada tulizozifanya kwenye uchaguzi wa 2010 sehemu mbali mbali,
ni dhahiri ushindani kwa sasa ungekuwa mkubwa sana kiasi cha chama
kushika dola uchaguzi ujao iwapo chama kingejikita kwenye jitihada za
ujenzi wa chama.
Badala
yake uongozi wetu umewasaliti Watanzania waliokuwa na tumaini kubwa
sana na chadema na kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye Kuimarisha migogoro
baina ya viongozi wakuu wenyewe kwa wenyewe, wanaimarisha ubinafsi
miongoni mwa wanachama, wanaimarisha Udini na Ukabila pamoja na
ubadhilifu wa mali za chama.
Matendo
haya ya viongozi wetu ni UNAFIKI wa kisiasa, kiasi cha kutumia
mabilioni ya shilingi kwenda kumshambulia ama kummaliza kisiasa kiongozi
mwenzao (Zitto Kabwe) na kuacha ujenzi wa chama ukiendelea kuporomoka.
Kwenye ujinga huu, hakuna wa kumlaumu zaidi ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na na Katibu MkuuDkt.Wilbrod Slaa. Hawa
wanafaa sasa kuhukumiwa na watanzania wanaopenda mabadiliko ya kweli
kwa kurudisha nyuma jitihada za kuwakomboa na kukiimarisha chama na
badala yake wamekuwa wakitumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi za chama
kujiimarisha wao wenyewe.
C. UBADHILIFU WA FEDHA NA MALI ZA CHAMA.
Ndugu WanaHabari.
Mtakumbuka
kwamba baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2010 ruzuku ya chama
iliongezeka kutoka million 56 mpaka milioni 239 kwa mwezi.
Tunasikitika
kuona kwamba mpaka sasa chama kimeshindwa kufanya uwekezaji wenye tija
ili kukisaidia chama kiweze kujiendesha bila kutegemea Ruzuku ama kukopa
kutoka kwa Mbowe kama mwenyewe anavyopenda tuwe tunafanya.
Mpaka sasa chama kimepokea jumla ya shilingi BILIONI 10.038 kama
ruzuku kutoka serikalini ili chama kijiendeshe. Ni narudia, mpaka sasa
chama kimepokea kutoka serikalini jumla ya SHILINGI BILLION KUMI, NA
MILIONI THELASINI NA NANE.
Cha
kusikitisha kwa kipindi chote hicho na kiasi chote hicho cha pesa
zitokanazo na kodi za waTatanzania pesa ambazo zinasababishwa na kazi
kubwa tuliyoifanya ya kukipigania chama kwenye uchaguzi mkuu wa 2010,
leo chama hakina hata jengo moja la OFISI MIKOANI KOTE na OFISI zote za
mikoa tunapanga kwenye FREMU za maduka na hata Pango la fremu hizo
tunajilipia wenyewe kwa kuchangishana, Mbowe na Slaa wanatumia MABILIONI
HAYA KURUKA NA CHOPA sisi huku chini tunaendelea kumenyeka kwa kigezo
cha UKAMANDA ,huu ni utumiaji mbaya wa mali za chama.
Tunasikitishwa sana na kitendo cham mwenyekiti MBOWE kusema anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila siku, kiasi cha zaidi ya MILLIONI 700 Mbowe
anajilipa kama madeni aliyokikopesha chama. Sasa tunashindwa kuelewa
deni hili ni deni gani lisiloisha?, na je deni hili alikikopesha chama
kwa mkataba gani?, na aliusaini mbele ya nani huo mkataba wa mkopo?,
Taratibu za chama kukopa zipo wazi je zilifuatwa?. Haya ni matumizi
mabaya ya fedha za umma.
Tunasikitishwa
na kitendo cha mwenyekiti mbowe kukiuzia chama MAGARI CHAKAVU kwa zaidi
ya million 600, Huku akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia
chama alikuwa anakikodisha magari hayo.
Masikitiko
yetu ni kitendo cha MBOWE kununua LANDCRUISER V8 VX 2 kwa pesa za chama
na kasha kuja kukiuzia chama, lakini kama haitoshi mpaka leo hii Gari
hizo zimesajiriwa kwa majina ya MBOWE HOTELS. Haya ni matumizi mabovu
mno ya mali za umma na kwamba yampasa sasa ajitathmini kama anapaswa
kuendelea kuwa kiongozi mtetezi wa wanyonge ama mnyonyaji wa wanyonge.
Tunahudhunishwa
na kitendo cha Dkt. SLAA kutufanyia huduma ya kutuuzia ukombozi,
haiwezekani kwa akili ya kawaida, ukawa katibu mkuu unayelipwa zaidi ya
million 130 kwa mwaka na chama halafu makatibu na viongozi wako wa
mikoani wanalipwa 0 kwa mwaka. Huu ni udalali na unafiki wa kisiasa.
D. UVUNJIFU WA KATIBA NA KANUNI ZA CHAMA.
Mpaka sasa viongozi wakuu hawa, wamevunja katiba ya chama kwa mambo makuu matatu yafuatayo.
1. Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge la katiba bila kuruhusiwa na vikao halali vya chama.
Bunge la katiba lilikuwa ni mazao ya Juhudi zetu sisi wanaCHADEMA tuliopambana nchi nzima kuidai katiba.
Chama
chetu kilikuwa na fursa kubwa ya kutuwakilisha kwenye kuandika katiba
hiyo na kufanya marekebisho makubwa kwa kadri tulivyoazimia.
Lakini
kususa Bunge la katiba lililotokana na Sheria mliyoishiriki kuitunga,
ni kutufanya sisi sote tunaowakilishwa na viongozi hawa tuonekane ni
majuha.
Kwa
kuwa CHADEMA ni miongoni mwa waasisi wa mchakato huu wa Katiba. Ni
kuwasaliti Watanzania na kuikosesha nchi fursa ya kuandika katiba
kususa.
2. Kitendo cha Kuunda Baraza Kivuli la mseto na vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushirika na CCM.
Kwenye
hili, chama kinapaswa kuelezwa kama mazingira yaliyowafanya wenzetu
hawa kuungana na CCM yamebadilika ama bado yapo?, Chama kinapaswa
kuelezwa na mbowe na Slaa kuwa Uteuzi wa Mbatia kuwa Mbunge wa kuteuliwa
na Rais wa CCM umebatilishwa ama la?.
Lakini
chama pia kitueleze kama Nafasi ya juu ya viongozi wa CUF kwenye
serikali ya mseto na CCM kule Zanzibar haipo tena. Vinginevyo viongozi
wetu wote walioshiriki hili wanatakiwa wawajibike haraka iwezekanavyo.
3. Kutokuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu.
Katiba yetu inatuagiza Kuwa Baraza kuu la chama litaitishwa kila baada
ya miezi kumi na mbili. Kwa kuwa baraza kuu la mwisho liliitishwa
February 2013, kulipaswa kuitishwa tena baraza kuu lingine kabla ya
mwezi February 2014 kuisha.
E. AGIZO
· Tunawaagiza
viongozi wetu waitishe haraka MKUTANO WA BARAZA KUU ili pamoja na mambo
mengine viongozi wetu wajieleze mbele ya Wajumbe ni kwanini
Tusiwachukulie hatua za kinidhamu kwa makosa ya UBADHILIFU, KUSALITI NDOTO ZA WATANZANIA, na KUHAMASISHA MGAWANYIKO NA UBAGUZI NDANI YA CHAMA.
· MBOWE na Dkt. SLAA wanatakiwa wajipime wenyewe kama ni sahihi chama kukodi HELKOPTA(CHOPA) 3 na kutumia zaidi ya BILIONI 1.4 za ruzuku ambazo ni kodi za Watanzania halafu eti tunashinda KATA TATU kati ya zaidi ya KATA 27, Yaani kila HELKOPTA MOJA imeleta KATA MOJAama kila SHILINGI MILLIONI 466.6 kwa KATA MOJA, halafu chama hakionyeshi kushtuka wala Kujali
· MBOWE
na Dkt. SLAA wajipime zaidi kama wanafaa kuendelea kuwa viongozi wa
chama huku chama kikizidi kudidimia kila uchao kiasi cha KUDHARIRISHWA
KWA kupata KURA 2000 CHALINZE na KURA 5000 KALENGA huku chama kikitumia
zaidi ya MILLIONI 600 kushiriki CHAGUZI HIZO.
N;B. ORODHA YA WAJUMBE WALIASHIRIKI IMEAMBATANISHWA
Imesomwa leo 23.6.2014 kwa niaba ya wajumbe nami;-
ATHUMANI H. BALOZI
…………………………..
0756767672
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TABORA
MJUMBE BARAZA LA MASHAURIANO KANDA YA MAGHARIBI
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA.


Post a Comment