ITALIA
imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay,
bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis Suarez
alimng’ata Giorgio Chiellini.
Godin
alifunga bao hilo dakika ya 81 na kipa Buffon wa Italia alilazimika
kuingia uwanjani dakika ya mwisho kusaidia nguvu ya kusaka bao, Azzuri
ikihtaji sare tu kusonga mbele.
Italia ilimpoteza mchezaji wake Marchisio aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Arevalo Rios dakika ya 60.
 |
| Mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo (kushoto) akibadilishana jezi na Edisnon Cavani wa Uruguay baada ya mechi |
 |
| Suarez baada ya kumng'ata Chiellini |
 |
| Refa hakumpa adhabu Suarez |
 |
| Chiellini akilalamika kung'atwa na Suarez begani |
Costa
Rica imemaliza kileleni mwa Kundi D baada ya sare ya 0-0 na England leo
ikifikisha pointi saba, Uruguay pointi sita na Italia pointi tatu,
wakati England imeondoka na pointi moja.
Kikosi
cha Italia kilikuwa; Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Marchisio,
De Sciglio, Verratti/Motta dk75, Pirlo, Darmian, Balotelli/Parolo dk46
na Immobile/Cassano dk71.
Uruguay:
Muslera, Caceres, Gimenez, Godin, A.Pereira/Stuani dk63, Gonzalez,
Arevalo Rios, Rodriguez/Ramirez dk78, Lodeiro/M Pereira dk46, Cavani na
Suarez.
Post a Comment