SOKO LA MCHIKICHINI DAR LILILOVYOUNGUA MOTO
SOKO la Mchikichini jirani na Uwanja wa
Karume jijini Dar limeungua na kusababisha hasara kubwa kwa
wafanyabiashara wapatao 4, 000, kwa mujibu wa mwenyekiti wa soko,
Jumanne Kangogo.
Moto huo inasemekana ulianza kuwaka jana
saa 4 usiku huku chanzo hakijajulikana, wengine wakisema ni shoti ya
umeme na wengine wakidai ni hujuma ambazo zimefanyika kulichoma soko
hilo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti waliwapigia watu wa Zimamoto walikuja kwenye saa 4.45 lakini walishindwa kutokana na kasi ya moto ilivyokuwa kubwa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti waliwapigia watu wa Zimamoto walikuja kwenye saa 4.45 lakini walishindwa kutokana na kasi ya moto ilivyokuwa kubwa.
Kwa niaba ya wafanyabisahara hao, Kangogo
ameiomba serikali kuwasaidia kwa njia yoyote kwani mali zao zimeteketea
katika moto huo.
Aidha amewataka wafanyabishara wawe
watulivu kwa kipindi hiki kigumu kwani mpaka sasa thamani halisi ya mali
iliyoteketea na kuibiwa haijajulikana.
(PICHA/HABARI NA GABRIEL NG'OSHA/GPL)
Post a Comment