MAYWEATHER AMPITA RONALDO KWA MKWANJA
Floyd
Mayweather Jnr, akiwa katika gari lake aina ya Bugatti Vevron lenye
thamani ya pauni milioni 1.8 ( sh bilioni 5) akiondoka katika Fainali
za Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) huko Miami, Marekani.
Akiwa katika moja ya mapigano yake aliyoshinda.
BONDIA Floyd Mayweather Jnr (37) wa Marekani hivi sasa ndiye mwanamichezo anayelipwa dau kubwa zaidi duniani. Amemshusha mwanasoka Cristiano Ronaldo katika nafasi ya pili ambapo mcheza mpira wa kikapu (basketball) Lebron James wa Marekani ameshuka na kufikia nafasi ya tatu mbele ya mcheza soka Lionel Messi wa klabu ya Barcelona.
Mayweather juzikati ‘alitengeneza dola milioni 105 (sh bilioni 1.7).
baada ya mapigano yake mawili ya mwisho ambapo Ronaldo ana utajiri wa dola milioni 80.
baada ya mapigano yake mawili ya mwisho ambapo Ronaldo ana utajiri wa dola milioni 80.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes la mwaka 2013 Mayweather ambaye ameshinda mapigano yake yote 46, ‘alitengeneza’ fedha hiyo baada ya kuwatwangilia mbali mabondia Saul ‘Canelo’Alvarez na Marcos Maidana katika mapambano hayo ya mwishoni na kushika nafasi ya kwanza kwa mkwanja miongoni mwa wanamichezo duniani.
Kwa vidokezo tu, miongoni mwa wanamichezo
wenye mkwanja mkali duniani ni mcheza mpira wa kikapu Kobe Bryant wa
Marekani, wacheza tenisi Serena Williams na Maria Sharapova.
Post a Comment