AMANDA YAMKUTA YA MAREHEMU RECHO...ACHANJWA USIKU
MMWIGIZAJI mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’ ameamka na kushtuka akiwa amechanjwa chale na watu wasiojulikana kama alivyowahi kufanyiwa marehemu Recho.
Mwigizaji mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema lilitokea siku ambayo
dairekta mkongwe nchini George Tyson alipofariki dunia (Mei 30) ambapo
hakujua ni nani aliyemfanyia ‘unyambilisi’ huo usiku kwani alishtuka
asubuhi na kuona akivuja damu zikiashiria kuchanjwa kwa wembe." Nimeamka asubuhi nikiwa nikiwa najipaka sabuni kipindi naoga nikashtuka kuona nimechanjwa kwenye mkono,lakini nimelala nikiwa sina hata doa tena nilichelewa kulala bda ya kupokea taharifa ya msiba wa kaka TYSON ,hii unamaanisha tukio la kuchanjwa limetokea alfajiri...sasa sijaelewa ila ninachoweza kusema ni kuwa wote tumeumbwa na MUNGU na wote tunamtegemea huyo huyo ingawa wapo wanaofanya ushetani wao lkn mwisho wa siku wote tumeumwa na MUNGU...na hili pia namuachia MUNGU maana yy ndio muamuzi na ndio mlinzi wangu...."
“Nilijikuta nimechanjwa lakini Mungu ni mwema, waliofanya hivyo kama walikuwa na nia mbaya, wameshindwa kwani nilikwenda kuombewa kanisani halitanipata lolote,” alisema Amanda.
Post a Comment