Yanga yasajiliwa kiungo
KLABU ya soka ya Yanga jana iliwapa mikataba mipya wachezaji wake watatu,
kiungo Omega Seme na mabeki Oscar Joshua na Juma Abdul.
Yanga imeanza kucharuka na kuwapa wachezaji wake mikataba mipya baada ya
Didier Kavumbagu na Frank Domayo kutimkia Azam FC hivi karibuni.
Ni sawa na kusema kuwa Omega ndiye mchezaji mpya kwenye lisiti hiyo kwa
kuwa msimu uliopita hakuwa na kikosi hicho baada ya kupelekwa Prisons kwa mkopo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa wachezaji hao walisaini
mikataba hiyo chini ya katibu mkuu wa klabu hiyo Beno Njovu,
huku wakishuhudiwa na baadhi ya viongozi wengine wa timu hiyo.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa Abdul ameongezwa mkataba huo baada
kuomba kusajiliwa kutokana na awali kugoma kuongeza mkataba kutoka na
kutaka fedha nyingi.
“Wachezaji hao kuanzia leo (jana) ni mali halali ya Yanga kwani tayari
wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja wa kuendelea kuitumikia
klabu hii,” kilisema Chanzo hicho cha habari.
Hata hivyo, wachezaji hao walipotafutwa kila mmoja aligoma kulizungumzia
suala hilo ambapo jibu walilokuwa wakitoa ni kwamba “Nani kakwambia suala hilo kaka.”
Kwa upande wake Njovu, alipotafutwa azungumzie suala hilo hakuweza
kupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.

Post a Comment