USITOE THAMANI YA MPENZI WAKO KWA MWINGINE!
Marafiki
leo nitazungumzia juu ya jambo muhimu sana ambalo limekomaa kwenye
jamii yetu.
Ni jambo linaloweza kusababisha matokeo mabaya kwenye uhusiano lakini kwa bahati mbaya
wengi hawalioni.
Wengi (hasa wanawake) wamejikuta wakiingia kwenye mtego unaosababishwa na
kuondoa
thamani ya mwenzi wako na kuihamishia kwa wengine na mwishowe usaliti hutokea.
Chanzo cha yote hayo ni mazoea mabaya ya kuitana majina ya kimapenzi na wanaume
wengine, ambao si wenzi wake.

Hujawahi kumsikia mwanamke anamwita mwanaume ambaye si mpenzi wake kwa majina ya kimapenzi kama baby, sweetie, honey, mpenzi na mengine yanayofanana na hayo?
Majina ya kimapenzi yana thamani kubwa sana na ni vyema basi kama yakitumika kwa watu
sahihi- wenzi husika.
Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya
kimapenzi huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo.
Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na
mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile inayotambulika na anayeitwa.
TUANGALIE ATHARI ZAKE
Majina niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo,
basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.
Kama unaweza kumuita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni
wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.
HARUFU YA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Juliana,
mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi
saluni moja ya kiume. Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kuwafurahisha wateja na wakati mwingine kuwafanya wanipe tipu baada ya kumaliza kazi.
“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita
dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.
“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake.
Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”
Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu yangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka na hujiona wenye bahati na mara
hushawishika kuingia mapenzini.
Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo?
MWISHO KABISA
Kati ya majina niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na
wasio na uhusiano wa kimapenzi lakini ni undugu wa damu. Mathalani baba, mama,
kaka, dada, shangazi nk.
Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye
maana ya moja kwa moja ya kimapenzi.
Bila shaka somo limeeleweka na utachukua hatua

Post a Comment