ad

ad

Ferdinand kuondoka Old Trafford

Mlinzi wa Manchester United Rio Ferdinand amesema ataondoka Old trafford 
msimu ujao baada ya klabu hiyo kukataa kumuongezea muda kwenye kandarasi yake.
Kauli hiyo inamaanisha Ferdinand ambaye amefunga mabao nane Old Trafford katika
miaka 12 na kushiriki katika mechi 454 ataingia katika orodha ndefu ya wachezaji
wakongwe mabalozi wa klabu hiyo.
 haijulikani ataichezea klabu ipi.
Ferdinand alisema katika barua ya wazi kwa klabu hiyo kuwa angelipenda kuwaaaga
mashabiki wake kwa njia bora zaidi lakini kutokana na ati ati hangeweza .
Hata hivyo amesema kuwa amefikiria sana kuhusu hatima yake na umewadia wakati
wake kuwaaga.
Ferdinand aliwasili United Agosti 2002 kutokea klabu ya Leeds timu hiyo
ilipokuwaikikabiliana na Hungary Zalaegerszeg katika mechi ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya.
Ameshinda mataji 6 ya ligi kuu ya premia mbali na mataji mawili ya nyumbani .
Manchester Utd pia ilishinda taji la klabu bingwa duniani mbali na taji la mabingwa
barani Uropa.

No comments

Powered by Blogger.