ad

ad

LULU AKACHA MSIBA WA KUAMBIANA, AJITETEA

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedaiwa kuukacha msiba wa
 aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana na kujitetea kuwa alibanwa
na majukumu.
Alipobanwa na mwanahabari wetu kuhusu kutohudhuria msiba huo uliodumu kwa takriban siku
 nne, Lulu alijitetea kuwa alikuwa Mwanza kikazi.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Nimebanwa na kazi, nipo Mwanza na kampuni yetu tunayofanya nayo kazi imetoa nafasi
moja tu kurudi Dar kwenye msiba, nimeshindwa,” alisema Lulu.
Mastaa wengi walijitokeza kwenye msiba huo akiwemo Jacob Steven ‘JB’ ambaye
alikuwa nchini Uturuki kikazi lakini akaziacha na kurejea Bongo kumpumzisha prodyuza wake.
CHANZO GPL

No comments

Powered by Blogger.