ad

ad

GOOGLE WAJA NA KITU KIPYA, WATENGENEZA MAGARI YANAYOJIENDESHA YENYEWE

Gar linalotembea bila kuwa na dereva kutoka kampuni ya Google. Kampuni ya Teknologia ya Google imesema itaanza kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe.
Kampuni hiyo ambayo imejijengea sifa kwa njia ya kipekee ya utendakazi wake katika sekta ya kiteknolojia imekuwa ikikarabati magari ya kawaida.
Gari hilo la kiteknolojia halitakuwa na usukani.
Google imesambaza picha ya gari hilo ambalo inasema ni la kutumiwa mijini na linapaswa kuwa chambo kwa wale ambao bado hawana imani na teknolojia hii ya hali ya juu.
Muasisi wa kampuni hiyo, Sergey Brin alizindua gari hilo la kipekee katika mkutano na wanahabari huko California.
Brin alisema kuwa teknolojia hiyo ina uwezo mkubwa wa kuimarisha maisha ya watu.

Mfumo wa gari hilo.
Watafiti wa magari yanayojiendesha yenyewe bado wanajadili iwapo kuwepo kwa magari hayo mabarabarani yatakuwa na upungufu wowote ikiwemo dhana kuwa itachangia ongezeko la msongamano wa magari.

No comments

Powered by Blogger.