ad

ad

Esperance yamtimua Krol

Klabu ya Esperance ya Tunisia imemfuta kazi kocha wake Ruud Krol kufuatia matokeo
mabaya katika mechi za makundi katika ligi ya vilabu bingwa ya Afrika.
Mholanzi huyo alitimuliwa baada ya klabu hiyo kushindwa katika mechi mbili.
baada ya kushindwa kwa mabao 2-1 na Entente Setif ya Algeria.
Timu hiyo baadae ilishindwa kwa mara ya pili mfululizo ilipofungwa mabao 3-2 na Al-Ahly Benghazi ya Libya, katika mechi iliyochezewa ugani Sfax Tunisia, kwa sababu za kiusalama.
Krol, ambaye amewahi kuwa nahodha wa Uholanzi katika kombe la dunia alikuwa amejiunga na Esperance mwezi Januari katika kandarasi ya miaka 3.
Wasaidizi wake vile vile wamefutwa kazi.
Esperance ndio timu yenye mafanikio zaidi katika historia ya ligi ya Tunisia.
Imewahi pia kushinda kombe la vilabu bingwa mara mbili.

No comments

Powered by Blogger.