Hadi sasa watu wameshonana uwanjani kutoa sapoti yao kubwa kwa UKAWA katika kupigania Katiba inayotokana na maoni ya wananchi.
Ameshasimama Prof. Abdul Sheriff kutokea kundi la 201 ambaye amesema wazi kuwa wahuni wa kuhujumu hawatafanikiwa mbele ya UKAWA.
Katibu wa Shura ya Maimamu na Taasisi za Kiislamu amesema taasisi zote
za Kiislamu zinaunga mkono Shirikisho la Serikali Tatu na kwamba walitoa
maoni yao mbele ya tume na wanaungana na UKAWA kulidai hilo. Hakuna
atakayeweza kuhimili vishindo vya UKAWA na wapenda haki na matumaini kwa
ajili ya amani ya kweli nchini kwetu, Tanzania.
Ameishambulia Serikali na CCM kwa uchochezi wa kidini, kuwachonganisha
Watanzania, kutokana na kauli ya uchochezi iliyotolewa na Waziri wa
Serikali ya CCM, aitwae William Lukuvi tena kanisani akiwasema waislamu.
Amehoji je mashehe nao wakifanya hivyo, nchi itatawalika?
Ametoa rai kwa viongozi wa UKAWA kuimarisha UKAWA na kuhakikisha kuwa UKAWA haufi.
mambo yanazidi kunoga
Jussa alipanda kuwakilisha
wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe
tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti
wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.
Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James
Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama
kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha
Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.
Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu
wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la
Katiba.
Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria
ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo
lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.
Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.
Lisu;
Jussa alipanda kuwakilisha
wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe
tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti
wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.
Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James
Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama
kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha
Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.
Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu
wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la
Katiba.
Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria
ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo
lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.
Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.
Lisu;
Wazanzibar wanamwita Lissu
Christiano Ronaldo. Wananchi wameshangilia balaa alipoanza kwa
kuwasalimia kwa jina la Zanzibar Huru na Tanganyika Huru na Shirikisho
lenye hadhi kuu ya nchi.
Kwa miaka 50, anasema Tundu Lisu, Zanzibar imekuwa koloni la Tanganyika,
Zanzibar imefungwa minyororo na Tanganyika na sio huru tena.
Kwa miaka 50 masuala yote ya nje yamekuwa yakiamriwa Dar es Salaam,
Mambo ya Ulinzi yanaamriwa na Dar, masuala ya fedha ya Zanzibar yamekuwa
yakifanywa na Dar na kwa hiyo ni koloni la Tanganyika.
Anasema mtia minyororo kwa mtu mwingine naye pia hawezi kuwa huru.
Akatolea mfano wa mfunga minyororo wa magereza kuwa naye hawezi
kuondoka., hivyo Tanganyika iliyoifunga Minyororo Zanzibar nayo haiko
huru.
Akasema Tanganyika ilikana jina lake na kuliondoa kwenye katiba ili
iendelee kuinyonya Zanzibar, anasema ilikuwa na Tanganyika huru ni kuwa
na Zanzibar huru.
Anamkaribisha sasa Maalim Seif;
Maalim Seif jukwaani sasa;
kaanza kwa kumtambulisha Mzee Moyo ambaye alikuwa Waziri wa Katiba wa
Mzee Abeid Amani Karume, Mzee Moyo kasema 'ni tatu, tatu, tatu bila
mzaha'. Kasema leo anaacha majembe yazungumze.
Maalim amesema kama wanaogopa Shirikisho la Serikali Tatu, basi yeye
yuko tayari kuunga mkono serikali mbili kwa maana ya Zanzibar huru na
Tanganyika huru, tofauti na hapo kila mtu na lwake.
Maalim anawatambulisha viongozi wa UKAWA nje ya bunge, akianza na Mosena Nyambabe- Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi.
Maalim Seif akaongeza kusema kuwa kama Kikwete anao uwezo wa kuwadhibiti Wazanzibar basi aende na cha moto kitaonekana.
Amesema kuwa kuna magari yameletwa kwenye mkutano na vikosi vya KMKM,
akaasa kuwa ole wake aguswe mtu akasema anazungumza kama Makamu wa Rais,
watajua jini liliko Zanzibar, uwanja ukalipuka kwa shangwe na nderemo.
Akapanda Emmanuel Makaidi mzee wa 'Moto moto motoooo...uwachome CCM'...
Dkt. Slaa amesema kuwa Jeshi la
Tanzania halijakosa uzalendo kama walio nao mafisadi wa CCM na serikali
yake. Kutokana na uzalendo ambalo JWTZ linao kwa wananchi na nchi,
haliwezi kupindua serikali eti tu kwa sababu ni Shirikisho la Serikali
Tatu.
Anasema kuwa wanajeshi wetu wamekuwa wazalendo kiasi cha kuvumilia
kukosa mishahara, maslahi yao madogo na shida nyingine iweje wafanye
hivyo kwa serikali tatu, amesema Kikwete halijui jeshi ndiyo maana
amepotoka...
Maalimu Seif aliendelea ambapo aliwasihi viongozi wa UKAWA kujiimarisha na kuulinda UKAWA kwani wabaya wao wanajipanga.
Akasema kuwa wakati wa kutishana tishana umeshapita. Kuendelea kutisha Wazanzibar ni kuwaongezea ari na hamasa.
Makaidi amesema kuwa
Watanganyika wamebakia bila serikali kwa sababu Mwalimu Nyerere Baba wa
Taifa aliitupa serikali yote ya Tanganyika kwenye Muungano na Karume
hakuitupa yote na ndiyo maana wamekuwa ngaringari leo.
Amewaomba Wazanzibar kuungana na Watanganyika kudai serikali zao...
Makaidi anasema CCM hakuna wanasiasa bali wajasiriamali na ndiyo maana
hawataki kujisahihisha kama Mwalimu alivyotaka. Kisha akapanda
Mtikila...
Mtikila; Kinachowasumbua CCM
kuhusu serikali tatu ni unywani. Watanganyika wanapumbazwa kuwa uhuru
ni mizinga uwanja wa taifa. Anasema kuwa kuwatisha wananchi na majeshi
ni ugonjwa wa apedomia. Wanasahau kuwa wanajeshi wana ndugu zao wengi
uraiani. Akamalizia kwa kusema saa ya ukombozi ni sasa...
Mbatia; muungano haukuridhiwa
kwa sheria za Zanzibar kwa hiyo ni batili. Anasema Zanzibar
kujitangazia mamlaka yake ni kuikomboa Tanganyika. Amesema kuwa wajumbe
wa UKAWA kutoka Zanzibar wamewanyima turufu majiCCM huko BMK hivyo
asitokee mtu wa kuisaliti Zanzibar.
Amesema kuwa chokochoko za udini zinapandikizwa na CCM, lakini hazitafua
dafu. Anasema huwezi kuwa muislamu safi halafu ukahubiri udini na
ubaguzi wa aina yoyote, huwezi kuwa Muislam safi kisha ukahubiri matusi
na kejeli. Vivyo hivyo kwa mkristo safi.
Mbowe; maandamano nchi nzima ya
kudai Katiba Mpya na bora inayotokana na maoni ya wananchi yanakuja
baada ya mikutano ya Zanzibar. UKAWA haitarudi bungeni kushiriki dhambi
ya kupingana na maoni ya wananchi, dhambi ya kuhubiri matusi kwa
wananchi.
Amesema kuwa UKAWA huu si kwa ajili ya Katiba tu bali ni kwa ajili ya
maslahi halisi ya wananchi. Ametangaza rasmi kuvunja Baraza Kivuli na
sasa ataliunda upya kwa ushirika na NCCR, CUF CHADEMA.
Wananchi wamelipuka kwa furaha baada ya Kamanda Mbowe kutangaza kuwa UKAWA utaendelea hadi uchaguzi.;
Prof. Lipumba; wanaopinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama
hawajielewi. Anasema nchi inaingizwa kuzimu kwa matumizi ya hovyo na
mabovu ya serikali kila siku.
Amesema ofisi ya rais inaongoza kwa matumizi ya hovyo. Anatoa mfano
ambavyo imekuwa ikitumia mabilioni kwa Rais Kikwete kujitangaza Vasco Da
Gama kwa kuzurura ughaibuni.
 |
WAKAZI WA KUTOKA KISIWA CHA TUMBATU WALIFIKA KWENYE UKAWA NA MABANGO YAOKIWANJA CHA KIBANDA MAITI |
 |
MUASISI MZEE NASORO MOYOALIFIKA KWENYE UKAWA |
 |
MAKAMU
WA KWANZA WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMADI AKIKUMBATIANA KATIBU
MKUU WA CHADEMA DR WILBROD SLAA KULIA KATIBU MKUU WA NCCRMAGEUZI MUSONA |
 |
MAKAMU WA KWANZA ZANZIBAR SHARIFF HAMAD AKISALIMIANA NA KATIBU MKUU CHADEMA DR SLAA |
 |
KATUIBU MKUU WA CUF MAALIM SEFU HAMADI AKIWASALIMIA WANANCHI |
 |
WANANCHI WAKISHANGILA |
 |
WANANCHI WAKIWA KATIKA MKUTANO WA UKAAWA |
 |
WENYEVITI
WA UKAWA JAMES MBATIA NCCR MAGEUZI KUSHOTO PROFES IBRAHIM LIPUMBA CUF
KATIKATI NA KULIA NI MWENYEKITI FREEMAN MBOWE CHADEMA WAKIWASALIMIA
WANANCHI |
 |
ASKARI WA KIKOSZI CHA FFU AKIWA KATIKA ULINZI |
 |
WANANCHI WAKIWA NA MABANGO YENYE UJUMBE WA KUONYESHA SERIKALI TAU |
 |
EMMANUEL MAKAID AKIWA ANASALIMIANA NA MZEE NASORO MOYO MUASISI |
 |
WANANCHI WAKIWA MABANGO YAO |
 |
MWANANCHI HUYU AKIONYESHA PICHA ALIYOIWEKA MGONGONI KWA YA RAIS MSTAAF WA ZANZIBAR NAYE ANATAKA TATU |
Post a Comment