ad

ad

RIWAYA: SIKU YA GRADUATION SEHEMU YA SABA


SEHEMU YA SABA
Niliendelea kutetemeka kwa hofu, nilijuta hata kwanini tulikimbia bila ya kuhakikisha tumem 'shoot' huyu Baunsa japo jibu nilikua nalo kwamba ilikua ni hamaki tu.. Baunsa aliendelea kuongea kwa sauti ya Ukali huku nikiisikia Sauti yake ikija usawa wangu nilizidi kuingiwa nahofu Lakini nilijikaza kisabuni, "Majambazi wanatoka mjini huko wanakuja kuua watu halafu wanakimbilia huku mnawaficha, dawa yenu iko jikoni" aliendelea kutoa tambo zake Baunsa huyu, nikawa sasa nasikia sauti kama vile jamaa anaviangusha chini vile viroba vya mbele kule kwa kuvipiga na mateke huku mwanga wa tochi ukizidi kuja usawa wangu...

Baada ya kusikia sasa nyayo zao zikija upande niliokua nimejificha mimi nilianza kuomba dua za kila aina ili Mungu mkuu atetende muujiza wake naimani dua yangu ilipokelewa kwani baada ya dakika chache nilimsikia Baunsa akimwambia huyo mjumbe kua waende wakakague na kule vyumbani mwao wanakolala, kisha wakatoka nje na hali ile ya Giza ikarejea, nilishusha tena Pumzi kwa kasi nikamshukuru Mungu japokua hali ilikua bado ni tete, nilikua nikimfikiria Ntahondi hali aliyokua nayo mule kwenye Kiroba alichojikunja kama mnyoo wa Amoeba.

Sikujua huko walikoenda walienda kumkagua nani! au kama waliwakagua wanakijiji wote kwa kua hawakua wengi sana pia sikujua, tuliendelea kutulia mule kwenye viroba vya mabunzi ya mahindi mpaka baadae kabisa tukasikia sauti za pikipiki zikiondoka tena kwa kasi, baada ya dakika kama 20 nikatoka ndani ya kiroba kisha nikaenda kumtoa na Ntahondi, tukajifuta vumbi lililokua kwenye viroba vile ambalo kwa kiasi kikubwa lilikua tayari limeganda mwilini kutokana na damu zilizokua zikituvuja. baada ya hapo sasa tukaanza kujadili tutajiokoa vipi kutoka pale tulipo maana sasa Wanakijiji wameshaambiwa kua sisi ni Majambazi na tulikua na Bunduki moja ambayo nayo tumeificha nyuma ya jiko na ile Bunduki nyingine bila shaka tuliiangusha njiani wakati tunakuja huku na nadhani itakua waliiona ndomaana wakaamua kutufuatilia maeneo ya kule, tukafikia muafaka wa kusubiri kwanza kupambazuke ili asubuhi tujitokeze tuwaeleze ukweli tu hawa wazee wa kijiji pengine watatuelewa, japo swali kubwa tulilobaki nalo itakuaje endapo watashindwa kutuelewa na kutuchukulia kua ni majambazi!!?

Tuliendelea kukaa mule jikoni muda mrefu tu kisha baada ya muda hali ikaanza kubadilika na kua ang'avu ikiwa ni ishara tosha kulikua kunaanza kupambavuka, nilipochungulia nje kulikua na wazee wawili wakionekana kujadili vitu kwa umakini mkubwa, nikamwambia Ntahondi kua acha mimi niwawahi hawa wazee nikajaribu kujieleza kabla hapajakucha na hawajajua lolote, Ntahondi alionekana sasa kua hana imani tena na hawa wana kijiji kwakua wanaonesha wameshaingiwa na hofu ya mikwara ya Baunsa na wenzie Lakini ikawa haina budi ikabidi tu nijikaze kisha niwafuate, ila nikamuambia Ntahondi yeye atulie tu pale pale aisije kwanza. Nikatoka mule ndani nikiwa hoi kwa mchoko nikaanza kuwaelekea waliko wazee wale wawili mmoja akiwa ni ktu kirefu mkononi kama vile Jambia, mwingine akiwa amevaa 'Rubega' yaani kajifunga shuka upande mmoa wa Bega lake la kulia, wazee wale waliposikia sauti za nyayo zangu wote waligeuka wakaangali upande ule ninaotokea mimi huku nikichechema kwa maumivu, Mzee mmoja akanisemesha kilugha ambacho sikukielewa ikanibidi tu mie niwanyooshe mikono yangu miwili kuashiria amani..

"Usiku..??" mzee mmoja alitamka neno hilo ambalo nililielewa vema, Mara nyingi ukikutana na mtu mida ya usiku unamuuliza 'usiku' akikujibu 'mchana' ujue anamaana ya Amani na akikujibu tofauti inaashiria ni hatari, hivyo hima nikamjibu
"Mchana!!", wazee wale wakawa wamejiweka tayari kunikabili, nilipofika wakanistopisha kwa mbali kisha wakanihoji kwa lugha ambayo sikuielewa kabisa, nikawajibu kua "Siijua lugha hiyo", yule Mzee aliejifunika shuka akanihoji
"We ni nani na unatokea wapi saa hizi?"
"Naitwa Naufal, nina matatizo makubwa wazee wangu naomba mnisikilize" wote wakawa makini kunisikiliza
"Mimi niko na mwenzangu tulikua tumetekwa na majambazi karibu mwezi mzima sasa na wametutesa sana na hatimae usiku wa kuamkia leo tukapambana nao kisha tukawatoroka na kukimbilia huku.." kabla sijamaliza kuongea yule mzee mwingine akaniwahi
"Anhaa kumbe nyie ndo mliovamia kule Godown la nafaka mkataka kuiba halafu mmeua mtu huko mkakimbila huku kuja kutuletea matatizo"
"Hapana wazee sisi sio wizi sisi ni raia wema tunatoka Dar Es Salaam tulitekwa na hata hapa sipajui ni wapi"
"Mwenzio yuko wapi?"
"Yuko humo ndani" nikawasontea kwa kidole kwenye lile jiko tulikokua tumejificha..

Wakati tunaendelea na mahojiano mzee aliejifunga shuka akaondoka hadi upande wetu wa kulia ambako kuna nyumba zao ndogo ndogo za kuishi kisha nikamsikia akiwaita watu kwa majina na baada ya muda mfupi akarudi na vijana kama sita hivi na wao wawili wakawa jumla wanane, walipofika wale viajana hawakutaka kutusikiliza kabisa zaidi ya shutuma tu juu yetu
"Hawa ni wezi tu wanatoka huko mjini kuja kufanya uhalifu huku, wafungeni kamba tuwapeleke huko Godown walikua vunja" kijana mmoja alisema huku akionesha kuungwa mkono na wenzie, Mwingine akakataa na kusema
"Tusipoteze muda wa kuhangaika na hawa watu tuwachome moto tu kisha tutawafukia huko kwenye shamba la mahindi" nae alipata wenzie walio msapoti kwa rai yake hiyo, sasa hapo ndo nilizidi kuchanganyikiwa wana kijiji waligoma kabisa kunisikiliza, Mara kijana mmoja akanisogelea na kunipiga sasa makofi huku akinitaka nikae chini, nikaa chini haraka kisha kijana yule aliongea kitu kwa lugha yao nisioifahamu Lakini nilielewa kua anamuulizia huyo mwenzangu nae alipo maana baada ya swali lake hilo alielekezwa na Mzee yule aliewafuata kuwaamsha kua yupo mule jikoni..

Kijana yule akaenda haraka na kisha akatoka akiwa ameshika Ntahondi huku akimvuta kwa kasi, alipomfikisha pale nae wakamshambulia kwa kichapo cha makofi kisha wakamkalisha chini pale karibu yangu, tukawa sasa kama wizi kweli tuliokamatwa. wakati huo hawa wanakijiji wakibishana juu ya nini cha kufanya kufuatia rai zilizotolewa moja ni kutuchoma moto na nyingine kuturudisha kule Godown kwa wale maharamia wa PABLO MWAKI, Nilikua nikilia huku nikijaribu kujieleza lakini hawakunielewa kabisa wazee hawa pamoja na vijana wao wakati wanaendelea kubishana kwa fujo kuna kijana mmoja ye akaja na kamba ngumu za katani kisha akaanza kutufunga mikono kwa nyuma ya mgongo na miguu, Ntahondi alikua nae akilia kwa uchungu..

Baada ya majadiliano ya muda mrefu akaja Mzee mmoja mwenye mvi nyingi kichwani, wote wakaanza kumsalia kwa hesha sana inaonekana ni mzee mwenye cheo fulani pale kijijini,
"Shikamoo Mzee Ngozi" aliamkiwa na kila kijana pale kisha wakaanza kumfahamisha hali ilivyo pale
" Hawa ndo wale majambazi walioenda kuvamia na kuua kule Godown, sasa tunafikiri tu kuwapeleka kule kule" yule mzee akamuangalia sana mmoja wa wale vijana aliekua akimpa maelezo kisha akamuuliza kwa ukali
"Hivi mna akili Timamu nyini?, mna uhakika gani kama hawa ni majambazi? mmewasikiliza mkathibitisha? mnakijua walichokiiba? na hata kama ni kweli ni majambazi Je huko mnakotaka kuwapeleka ni Polisi? na wakipatwa na mabalaa huko hata kuuawa hamuoni na ninyi mmeshiri?" Yaani nilitamani nimbebe huyu mzee, kundi zima likawa kimya, yule Mzee aliekua kajifunika shuka alijaribu kumuelewesha mzee mwenzie huyu lakini alizidi kuwapinga kwa hoja za msingi kutokana na kila walichomueleza, wakafikia muafaka kua wapige simu polisi ili watuijie askari pale na si kutuchoma moto wala kutupeleka kule Msituni ambako sasa nilianza kuelewa kua walio wengi wanaamini kua lile jengo ni ghala la kuhifadhia nafaka..

"Simu yangu mimi haina charge karibu wiki sasa, nendeni hapo kwa Mzee Banzi mkamwambie namuita hapa aje na simu yake" alitoa agizo huyu ambae alikua ni kama Mkombozi wa maisha yetu kwa sasa, kisha akaendelea kutoa Amri
"Wafungueni na hizi kamba, mbona hamna huruma ninyi?! angalia huyo binti mpaka mikono imeanza kuvimba jinsi mlivyomfunga kamba, na nyinyi wazee wenzangu manakosa hekma kiasi hiki?" vijana hawa walikua wakitii kila amri iliyotolewa na mzee huyu inaonekana alikua akiheshimiwa sana Wakati wanatufungu kamba yule kijana alietumwa nae akawa maeshawasili akiwa na Mzee mwingine wa makamu bila shaka ndie Mzee Banzi huyo, alipofika tu mzee huyu nae akasimuliwa kila kitu kisha nae kaanza kuzungumza kwa ukali
"Hili suala limeanza kunishtua sasa unajua kwa maelezo ya hawa vijana kuna kitu kinazunguka kichwani" aliakua akiongea huku akimtazama Mzee Ngozi
"Unajua juzi alikuja mwanangu kutoka mjini japo hakukaa sana ila katika mazungumzo akaniambia kua huko mjini kuna kijana ameuawa, halafu kuna wengine wawili wamepotea katika mazingira ya kutatanisha na akanitajia mpaka jina la huyo Binti alietekwa sema tu nimelisahau, sasa isije ikawa ni kweli ndo hawa halafu ninyi mnataka kuwapeleka huko huko wanaposeama ndiko walikokua wametekwa" kauli hii liwashtua wote pale, wakaangaliana kwa hofu sasa kisha Mzee Jonga aliekua akitikisa kichwa kuashiria kua anamuunga mkono mzee mwenzie aliekua akiendelea kuongea
"Ngoja tumpigie simu Mwanagu atutajie jina la huyo binti alitekwa kisha tutajua tu na hata kama sio huyu pia tutamtuma haraka aende kituo cha polisi akatoe taarifa kisha aje nao hao polisi mpaka hapa wawachukue ili haki ikatendeke huko huko mini" akamaliza kuongea Mzee huyu kisha akatoa simu na kumpigia huyo mwane...

"Hallow, hebu nipigie haraka Baba simu yangu haina salio" aliongea Mzee Banzi baada ya kuitoa simu yake katika mfuko wa Kanzu yake iliyochakaa, wakati tunasubiri huyo mwanae apige simu, huyu Mzee Ngozi akawahi kumuuliza Ntahondi
"Unaitwa nani Binti?" nilijua lengo lilikua ili ajue kama atakua ndie yeye ili afananishe majibu watakayopewa na huyu mtoto wao ambe bado hatujamjua ni nani na Je ana tujua sisi au Laa,
"Naitwa Ntahondi", hapo hapo simu ikaita tena akapokea huyu Mzee,
****************

ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA

 LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

1 comment:

Powered by Blogger.