The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 10
NDEGE inaanguka kwenye Msitu wa Congo, watu wote
waliokuwemo ndani wanakufa isipokuwa wawili (Johnson na mwanaye
Melania). Hawa wawili wanatenganishwa, Johnson anaokolewa na majeshi ya
Serikali ya Congo lakini Melania mwenye umri wa miaka mitano tu
anachukuliwa na waasi wa Kundi la Congolese Patriotic Front (CPF).
Melania, mama yake Loveness, ambaye walikwenda nchini Congo alikokuwa akifanya kazi na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi kumtembelea, anaanguka na kupoteza fahamu baada ya kupata taarifa za ndege kuanguka, mshipa umepasuka kichwani, baadaye anafanyiwa upasuaji nchini Tanzania lakini akapoteza kumbukumbu.
Johnson anatibiwa nchini Congo na kupona, akihojiwa na
televisheni ya CNN, mke wake anaona mahojiano hayo na kumbukumbu zote za
nyuma zinarejea! Akataka kwenda Congo lakini familia ikamzuia, baadaye
Johnson alirejea nyumbani na kuungana naye.
Wote wawili wakakubaliana kwenda Congo kumtafuta mtoto wao, huko walijiunga na jeshi baada ya kueleza nia yao, kwa miaka mingi wakawa msituni wakimtafuta Melania aliyeaminika kuwa mikononi mwa waasi.
Mwisho Johnson na Loveness walitekwa na waasi na kupelekwa kambini kwao, huko Melania ambaye hivi sasa anaitwa Kamanda Janette ndiye mkuu wa waasi, anaamuru wapigwe risasi mbele yake bila kujua kuwa wazazi wake ni miongoni mwa mateka hao.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
akuna kitu kilichomfurahisha Melania au Kamanda Janette, jina aliloitwa na wafuasi wote wa kundi la waasi la Congolese Patriotic Front, kama kushuhudia mtu akifa kwa kupigwa risasi! Akili yake ilishaharibika kabisa, kwa macho alishashuhudia watu wengi mno wakifa na yeye kuua kwa mkono wake.
Kifo cha mwanadamu kwa risasi alikiona ni sawa na mtu kupuliza dawa ya kuulia mbu chumbani, hakujali kabisa kama mbu aliokuwa akiwaua nao walikuwa na familia au ndoto maishani mwao.
“Shoot!” (Piga risasi!) alimuamrisha muasi aliyekuwa amesimama mbele ya mateka wa jeshi la Serikali ya Congo, bunduki yake ikiwa imejazwa risasi ipasavyo na ikiachia moja baada ya nyingine.
Bado Melania hakuwa hata na hisia kidogo kwamba miongoni mwa watu waliokuwa wakipigwa risasi pia, baba na mama yake ambao kwa miaka mingi waliteseka porini wakimtafuta walikuwemo! Macho yake yalikuwa yamezama kwenye albamu aliyoikuta ndani ya begi walilokamatwa nalo mateka, akitaka kufahamu picha ndani ya hiyo albamu zilikuwa ni za kina nani.
“No! Stop!” (Hapana! Acha!) alipiga kelele kwa sauti ya juu baada ya kusikia risasi ya tisa ikilia, hiyo ilimaanisha tayari kwamba watu tisa walikuwa marehemu.
Macho ya Melania, mwanamke katili, asiye na huruma hata kidogo yalikuwa yametua kwenye picha yake mwenyewe akiwa mtoto! Kumbukumbu za kuambiwa kuwa miongoni mwa watu waliokamatwa mateka kuna waliodai ni mtu na mke wake zilimrudia. Zoezi la kufyatua risasi likasimamishwa, Melania akasimama wima na kumwita msaidizi wake mkuu, Kamanda Otimanya.
“Wale mke na mume wako wapi?” alimuuliza.
“Ni wale namba tisa na kumi!”
“Mmoja ni aliyepigwa risasi mara ya mwisho?”
“Ndiyo.”
“Mungu wangu!”
“Kwani vipi mkuu?”
“Kuna kitu nimekigundua.”
“Kitu gani?”
Kamanda Janette hakujibu swali hilo, alichokifanya ni kukimbia haraka sana mbele mahali walipofungwa mateka, akasimama mbele ya mwanamke aliyekuwa amefungwa kwenye nguzo namba kumi, kwa kumwangalia tu taswira ya zamani sana kichwani mwake ikamwingia akilini, alikuwa mama yake mzazi, pamoja na ukatili wake, Kamanda Janette akaangua kilio mbele ya waasi wengine.
“Vipi?”
“Mama yangu!” akajibu akisogelea nguzo namba tisa, alipofungwa mwanaume aliyekuwa akihangaika kukata roho, risasi ilikuwa imempenya sehemu ya juu ya kifua upande wa moyo, damu nyingi zilikuwa zikimtoka na machozi yalionekana kumbubujika huku akimwangalia Kamanda Janette kwa macho ya huruma.
“Baba! Baba! Baba!” aliita mara tatu.
“Mwana…ngu nakupenda, naku…fa lakini nataka ufaha…mu mimi na mama yako tunakupe…nda sana, tumehanga…ika kwa miaka mingi msit…uni tukiwa tumea…cha kila kitu ili tuku…tafute wewe, nafu…rahi nimekuo…na kabla ya kifo changu, usisiki…tishwe sana na kilicho…tokea, bila shaka ilipa…ngwa nife kwa mtin…do huu, naku…penda Mela…nia, kwa moyo wangu wot…” Johnson hakuweza kulimalizia neno la mwisho, shingo ikaanguka upande, roho ikatoka mbele ya Melania na Loveness.
Huku machozi yakimtoka, Kamanda Janette alimfungua Johnson kwenye nguzo na kumwagiza muasi mwingine amfungue mama yake, wote wawili wakabebwa hadi kwenye hema lake, ambako Kamanda Janette aliendelea kumlilia baba yake, roho ilimuuma mno, kwa mara ya kwanza tangu aingie kambini akiwa mtoto mdogo.
“Nisamehe mama, sikujua! Akili ilishaharibika, najuta.”
“Usijali mwanangu, bahati mbaya!”
“Bila kuangalia albamu ya picha ningeweza kukuua hata wewe.”
“Tumshukuru Mungu.”
Tofauti na siku mateka wengine walipouawa kwenye kambi hiyo, siku hiyo ulikuwa ni msiba, waasi wote wakiomboleza kwamba baba wa kiongozi wao alikuwa amekufa. Askari aliyefyatua risasi hizo alimwomba msamaha sana Kamanda Janette ambaye alimwondoa wasiwasi kwa sababu ni yeye aliyetoa amri ya risasi kufyatuliwa.
Mazishi ya maiti zote yakafanyika, lakini ya Johnson ilizikwa kwa heshima kubwa zaidi ya maiti nyingine, huku Kamanda Janette akilia kama mtoto mdogo, jambo ambalo liliwashangaza mno wafuasi wa kundi hilo, hawakuwahi hata siku moja kumwona akiwa katika hali hiyo, mara zote walimchukulia kama mwanamke katili asiye na huruma.
Baada ya mazishi, kilichofuata ni maombolezo, Kamanda Janette na mama yake Loveness walijifungia ndani wakimlilia Johnson, moyo wa Kamanda Janette ulikuwa umepasuka vipandevipande kwa huzuni, hasa alipokumbuka mara ya mwisho walipoanguka na baba yake kwa ndege, walivyotembea porini mpaka alipotekwa na waasi akimwacha baba yake mahali ambako aliamini alikuwa amekufa lakini baadaye hakuikuta maiti yake.
“Kilitokea nini mpaka baba akawa hai?”
“Majeshi ya serikali yalimwokoa kutoka sehemu ulipomwacha na akapelekwa hospitali ambako
alitibiwa na kupata nafuu.”
“Wewe?”
“Nilipata matatizo makubwa sana baada ya kupata taarifa ya ndege kuanguka, mshipa ulipasuka kichwani, nikafanyiwa upasuaji, Mungu tu alisaidia, vinginevyo ningekuwa marehemu hivi sasa!”
“Pole sana, mkakutana vipi na baba?”
Loveness akamsimulia mtoto wake kila kitu kilichotokea mpaka wakaungana na Johnson tena na kwa pamoja wakaamua kuacha kila kitu ili wamtafute mtoto wao, jambo ambalo walilifanya kwa miaka mingi hatimaye wakatekwa na kujikuta kambini ambako Johnson na mateka wengine waliuawa kikatili.
Loveness akashindwa kuendelea na simulizi, alipofika eneo hilo, machozi yakaanza kumtoka na kazi ya Melania au Kamanda Janette ikawa ni kumtuliza mama yake huku akimwomba msamaha kwa yote yaliyotokea.
“Je, ilikuwaje kwako mwanangu?” Loveness aliuliza alipotulia.
“Ni habari ndefu mama, nilishakata tamaa ya maisha kabisa, sikujua ningekutana na ninyi tena.
Waliniteka, wakanifanyia kila aina ya unyama, mwisho wakanileta hapa kambini ambako nilibakwa karibu
kila siku baada ya kijana aliyenilinda na kunitetea kuuawa, baada ya hapo mbakaji wangu aliyekuwa kamanda mkuu wa waasi akanioa bila ridhaa yangu, maisha yakaendelea hivyo tukipambana na
jeshi la serikali,
nami akili yangu ikabadilika kabisa na kujikuta nimekuwa kiumbe kingine katili, alipokufa
mume wangu ndipo nikafanywa kiongozi wa kundi…” Kamanda Janette akajifuta machozi.
“Pole mwanangu!”
“Nisamehe mama, hayakuwa makusudi yangu, sikutaka kuwa hivyo.”
“Najua, sasa itakuwaje?”
“Lazima tuondoke hapa.”
“Itakuwa vizuri.”
“Lakini sijui kama wenzangu watanikubalia.”
“Kwa nini?”
“Tulishakula kiapo, najua wao watachukulia huu kama usaliti na hawataamini kama kweli wewe ni mama yangu, hata wakiamini, hawatakubali! Wanaweza kugeuka na wakatuua wote.”
“Sasa tutafanyaje?”
“Nitajaribu kuongea nao, nione kama watakubali.”
“Itakuwa vyema.”
Wiki moja baadaye, Kamanda Janette aliitisha mkutano wa hadhara wa wapiganaji wote na
kumtambulisha mama yake kisha kuwathibitishia kuwa aliyeuawa pamoja na mateka wengine
alikuwa baba yake mzazi, akawaeleza wazi kwamba wazazi wake kwa miaka mingi walikuwa porini wakimtafuta, mpaka baba yake akatoa uhai wake sadaka na sasa hakuwa na jinsi isipokuwa kuacha
uasi na kurejea uraiani.
Kama vile waasi walijua ambacho kingesemwa, walianza kupiga kelele wakilikataa jambo hilo,
huku risasi nyingi zikipigwa hewani kuashiria kutounga mkono kilichosemwa, sauti za waasi wengi zilisikika zikisema: “Huo ni usaliti, tutawaua wote!”
Kauli hizo zilimtisha Kamanda Janette, pamoja na kuwa kiongozi wa waasi lakini hakuwa na la
kuwafanya kama pia wangeasi dhidi yake! Hofu kubwa ikamwingia, si yeye tu bali pia mama yake, ambaye hakuwa na nia kabisa ya kubaki msituni, alitaka kurejea Tanzania na mtoto wake, bila kujali alishaharibika akili kiasi gani.
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo. Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi.
Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Je, nini kitaendelea? Fuatilia Ijumaa kwenye Championi Ijumaa.
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment