ad

ad

Hii Ndio Nchi Atakayoichezea Adnan Januzaj Kwenye Kombe La Dunia

MrInfo anakujulisha kuwa Januzaj alinunuliwa na Man kutoka Anderlecht kwa ada ya £297,000. Kijana huyu angeweza kuichezea Uingereza mwaka 2018 kama angeishi kwenye inchi hio kwa miaka mitano bila kuhama na awe amefikisha miaka 18, hii ni sheria ya Fifa.
Januzaj alionekana kwenye jezi ya Man Utd kwa mara ya kwanza kwenye mechi yao dhidi ya Crystal Palace, walishinda bao 2-o huku magoli yote yakifungwa na Januzaj, kwenye game ya Man dhidi ya Sunderland alifunga tena na kusababisha ushindi wa bao 2-1, ilikuwa 5 october 2013.

Manchester United winger Adnan Januzaj amefanya maamuzi ya kuichezea timu ya taifa ya Ubeljiji .
Kocha wa Timu ya taifa ya Ubeljiji Marc Wilmots ametangaza kupitia twitter kuwa amefurahishwa na uamuzi wa Adnan wa kuichezea timu ya taifa ya Belgium.

Januzaj alizaliwa mji mkuu wa Ubeljiji ambao ni Brussels na alijiunga na Man United mwaka 2011.
Adnan mwenye miaka 19 angeweza kuichezea  Kosovo, Albania, Turkey, Serbia na hata Uingereza kwenye maisha ya mbele.

Januzaj sasa anachukuliwa kama raia wa Ubeljiji na atacheza kwenye timu yao ya taifa kwenye kombe la dunia mwaka huu. Kikosi cha timu ya Belgium cha watu 30 kita tajwa tarehe 13 May.
Mpaka sasa Januzaj hajacheza mechi kubwa ya kimataifa ila MrInfo anapenda ufahamu kuwa alisha alikwa na Kosovo kuicheza mechi ya kirafiki.

Baada ya mafanikio mazuri uwanjani, Wilmots alisema Januzaj aicheze Belgium, Huku kocha wa Uingereza Manager Roy Hodgson akisema alimwangalia kwa ajili ya Uingereza.
12 13 14

No comments

Powered by Blogger.