RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA 01
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI
SEHEMU YA KWANZA
"Yaani kweli RAMLA Umeamua kunitenda kiasi hiki!!, pamoja na mapenzi yote niliyokupa lakini umeamua kunisaliti!, nimepoteza pesa zangu nyingi kukusomesha chuo nikiamini we ndo utakua mama wa Wanangu Leo wema wangu umegeuka mkuki wa sumu moyoni mwangu, Ramla Why? Why?!!" Niliendelea kulalama peke yangu huku nikilia kwa uchungu, shuka yote ikiwa imeloana jasho na machozi pale katika kitanda changu..
"Kitendo ulichonifanyia Ramla kinaniua ndani kwa ndani, huu ni zaidi ya ukatili yaani umesahau ahadi zetu zote tulizowekeana!!!.. aaaah" niliendelea kujisemea peke yangu kama Mwehu..
Taarifa hizi za uchungu kua Mchumba wangu Ramla ananisaliti kwa kutoka na na Kigogo maarufu jijini Dar Es Salaam nilizoambiwa na Rafiki yangu Mwl HONDE ziliniumiza sana sikua na sababu ya kupinga sana kwakua nilimuamini sana Rafiki yangu alienipa Ukweli wa Tukio hilo, kwanza Rafiki yangu huyu nimejuana nae siku nyingi tangu nikiwa pale chuo kikuu cha Dar Es Salaam pia Rafiki yangu huyu kwa sasa ni Muhadhiri katika chuo ambacho anasoma Mchumba wangu Ramla hivyo alichoniambia ana uhakika nacho kwa asilimia zote kwa kua nay eye yuko hapo hapo chuoni
Kilichoniuma zaidi ni pale nilipotajiwa na jina la huyo kigogo, Kwanza ni Tajiri, Mfanyabiashara maarufu, anamiliki miradi mingi, ana majumba na magari ya kifahari kila kona, anamiliki Cassino kubwa na maarufu kuliko zote jijini Dar, anahusishwa pia na Biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi wa magari na nyara za serikali, huyu si mwingine na PABLO MWAKI..
"Hata nikitaka kumfanyizia ubaya huyu Tajiri sitaweza.." Niliendelea kulia kwa uchungu. Basi nikajikaza na kuinuka pale kitandani na kwenda kuoga japo baada ya saa zima nikatoka Bafuni bila ya kujimwagia hata kopo la maji, nilikua nimesimama tu kichwa kikiwa na zaidi ya Kilo mia za mawazo.. nikarudi mpaka chumbani na kupanda kitandani kulala japo usingizi wote uliniruka, Usiku kucha niliwaza na kuwazua nifanye jambo gani ili nimrejeshe mchumba wangu mikononi mwangu na hatimae nikabakiwa na maamuzi ya kupambana na Pablo Mwaki bila ya kuogopa utajiri na ujambazi wake..
*****
Karibu na Posta mpya jijini Dar es salaam kuna Jengo kubwa la kibiashara lililoandikwa MIKINDA BUSSINESS CENTER, Ndani ya Jengo hilo mashuhuri kuna kila aina ya Biashara zinaendelea humo, Spermarket, Slot machine, Bureau De Change, Branch za Benki kadhaa, na pia ndani ya jengo hilo pia kuna Cassino mashuhuri ya kuuza makahaba, mashoga, na wasagaji, kila utakachokihitaji utakapata ndani ya jingo hilo.. Naam mjengo huo na vyote vilivyomo ni mali ya PABLO MWAKI
Pablo Mwaki na Mzee wa makamo japo ukimuona huwezi kudhanai kama ana umri mkubwa kutokana na mazoezi, maisha bora na jinsi tu anavyojiweka, Ni Mweupe, Si mnene wali si mwembamba, anapendelea zaidi kunyoa Kipara..
Mbali na Mjengo huo PABLO MWAKI pia ana miliki miradi mingine kibao zikiwemo kampuni za uchimbaji madini, Kampuni za usafiri wa majini na Angani, pia ana hisa kwenye baadhi ya makampuni makubwa makubwa,Si jambo la ajabu ndani ya Dar es Salaam nyumba kadhaa na maofisi yakihusishwa kumilikiwa na tajiri huyu, Wapo waliomsujudia Pablo kutokana na utajiri wake lakini pia wapo waliomchukia na kumlaani kutokana na kuwaharibia vijana wao kwa kuwatumia katika biashara zake haramu..
Pablo Mwaki alishawahi kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumteka na kumuua kijana Samson Shirima, mfanyabiashara wa madini na kumpora pesa nyingi, Lakini alitumikia kifungo hicho kwa takriban miaka mitano tu kasha akakata rufaa na kushinda kesi hiyo ndipo aliporudi uraiani na kuanza kufanya biashara zake na ghafla kua tajiri mkubwa..
*****
Siku iliyofuata niliwasili ofisini na kuomba Ruhusa kwa Boss wangu Mr Jimmy nlimueleza kua naumwa sana tumbo, japo si kweli. Lengo langu lilikua ni kwenda kuonana na Mwl Honde ambae ni muhadhiri chuoni kwa kina Ramla na ndie alienipa ukweli wa kila kinachoendelea kati ya Ramla na Pablo.
Kila nilipomuangalia Mr Jimmy ambae ni meneja katika kampuni yetu ya SAJAM MARINE Ltd nilizidi kuumia nafsi kwakua mbali ya kua Boss wangu pia ni Mume wa mama'yake mdogo na Mchumba wangu Ramla Aliechangia mama tu na mama yake na Ramla. Nilopotoka tu ofisini nikaenda moja kwa moja mpaka Chuo cha usimamizi wa fedha(I.F.M) kwa Mwl Honde nilipofika Honde akanipokea vizuri ila hatukua katika ule ucheshi na uchangamfu wetu, nilishindwa kabisa kujizuia na kujikuta nikionesha kabisa hali isiyo ya kawaida usoni mwangu, Baada ya salamu mazungumzo yakendelea
"Nisikilize Naufal mimi nakushauri kama mtu wako wa karibu, kwakua namfahamu vizuri Pablo naamini akikujua tu utakua katika hali ya hatari”
“Kwa hiyo wewe unataka nifanyeje?”
“ukubali matokeo na uachie ngazi, Pablo humuwezi, atakupoteza"
“Yaani Honde badala ya kunishauri tufanyeje ili tuwaachanishe we unataka niachane na Ramla!!”
"Kaa ukijua Pablo Mwaki kaishatangaza Ndoa , na Ramla amelipokea kwa furaha suala hilo, sasa kama unataka kuiweka Roho yako Rehani Endelea"
"Hivi Honde una akili timamu kweli wewe?! unajua me na Ramla tumetoka wapi?, unataka nikubali kirahisi rahisi kuibiwa na bwege huyo kisa ni tajiri, Kwanza wataoana vipi wakati Ramla ni Muislam na huyo Mpumbavu Mwaki ni Mkristo”
“Upo dunia gani kaka? Ramla ameshabadili dini na sasa ni Mkristo”
“Nilichogundua na wewe ni Msaliti tu, utakua umetumwa tu, Sio bure!" nikanyanyuka kwa hasira nikaanza kuondoka bila hata ya kuaga, nilimsikia Honde akijaribu kuniita ila hata sikujisumbua kugeuka nikaenda mpaka barabarani upande wa pili ulipo ukumbi wa Makumbusho ya Taifa nikachukua Boda boda na kutokomea zangu..
Nilipofika Nyumbani nikajipumzisha kwenye kochi huku nikiwa na mawazo mapya kichwa,
“Hivi inakuaje rafiki yangu wa karibu kama Honde anashabikia tukio hili? Tena bila hata ya aibu anasema nimuache Ramla, nimeanza kumshtukia, Haiwezekani, huyu itakua nae katumwa na huyu mjinga mwenzao ili anishawishi tu nimuache Ramla wangu au pengine ni yeye ndie anaemtaka” niliendelea kujifariji huku sasa lawama na hofu zangu zote zikawa ni kwa Honde sasa. Nikainuka pale kwenye kochi nikaenda bafuni kuoga, nikiwa bafuni nilsikia simu yangu ikiita nilipokwenda kuiangalia alikua ni Honde akinipigia simu nikaiangalia simu ikiita bila kuipokea kisha nikarudi bafuni huku nikijisemea mwenyewe "Akkkh hivi huyu mjinga anafikiri mie hayawani kama yeye" nikiwa bafuni naendelea kuoga simu yangu iliita tena ila wala sikujisumbua kwenda kuiangalia nikijua atakua ni Honde tu huyo. Nilipomaliza kuoga nikaenda kuiangalia simu yangu, kumbe hakua Honde, alikua ni Ramla kipenzi cha moyo wangu, haraka nikajifuta maji mwilini kasha nikachukua simu yangu na kumpigia Ramla..
“Hellow” ilikua ni sauti nyororo ya Ramla
"Hi darl”
“Mzima mume wangu”
“Mie mzima wa afya, habari za chuo?”
“Nzuri tu, Mbona kimya sana tangu jana halafu na leo nimekuona umekuja chuo nikajua utanipigia simu tuonane lakini ukanichunia sio vizuri hivyo”
"Hapana sijakuchunia mpenzi wangu nilikua na haraka sana kuna Laptop yangu alikua nayo Mr Honde ndo nikawa nimeiijia kulikua na kazi ya muhimu sana ofisini”
"Ok Baby, kesho nitakuja kwangu nijipikie mwenyewe, nimechoka na haya mambo hostel kila siku chips tu" Tuliendelea kuzungumza kwa madaha kila mmoja akimhadaa mwenzie, mimi nilimhadaa kwa kujifanya kama hakuna tatizo lolote nililolisikia nae bila shaka alinihadaa mimi kwa kuniita majina mazuri ya baby, mume wangu, nk wakati alijua fika kua kwa sasa ni mali ya Pablo Mwaki.
Baada ya kukata simu ya RAMLA Nikajitupia kitandani nikiwa nimechoka Mwili mpaka akili, mawazo ya kila aina yakizunguka kichwani mwangu. Nilikua nusu naamini kua Ramla amenisaliti, hapo hapo nahisi kua Honde ndie anataka kutugombanisha, hapo hapo natamani nimtafute huyo Pablo Mwaki nimfanyie kitu kibaya japo haikua rahisi, ni matamanio tu yasiyowezekana waswahili wanasema Dua la Kuku..
Nikiwa pale kitandani nilisikia mlango wa Chumbani kwangu ukigongwa nikajinyanyua kwa uchovu mpaka mlangoni, nilipofungua mlango tu akaingia NTAHONDI msichana mrembo, mcheshi na mchangamfu, ni rafiki wa karibu sana na Mchumba wangu Ramla pia wanasoma wote chuoni,
“Karibu”
“Ahsante Shem”
“Mpaka nimeogopa mbona usiku? Kuna usalama kweli?”
“Hah ha usiku gani wa kutisha huu, au hautaki wageni shem?”
“Hapana sio kawaida yako, haya karibu uketi”
“Ok, ahsante” Baada ya kumkaribisha ntahondi nilirudi kwanza kuufunga mlango kasha nikaenda mpaka kwenye Friji ili nimuangalizie japo kinywaji lakini akaniwahi kwa kukataa
“Shem wala usihangaike na kinywaji, mie sio mkaaji, nataka tu tuongee haraka niondoke”
“Acha roho mbaya, hautaki hata kuniwekea Baraka ndani!!”
“Usijali nitakunywa hata siku nyingine” baada ya Ntahondi kukataa kinywaji nikarudi mpaka karibu ya kochi alilokua amekaa na mie nikakaa kwenye kiti cha uvivu, kasha Ntahondi akaanzisha mazungumzon nilijiweka sawasawa kupokea habari iliyoonekana kua ni nzito sana kwa jinsi alivyoonekana usoni Ntahondi
“Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa hili nitakalo kuambia kama nitakukwaza maana sisi binaadamu hatujakamilika, pili hata kama halitokufarahisha naomba libakie kua ndani ya moyo wako kwa kua lengo langu mimi ni kunusuru maisha yako naomba nawe uninusuru kwa kuificha siri hii hata kama hautoipenda” alikua akiongea huku akiniangalia usoni bila hata ya kukpepesa macho, Niliendelea kumsikiliza bila kuongeza neno
"Kwa kifupi masha yako yako hatarini, muda wowote unaweza kuitwa kwa jina moja tu la Maiti” baada ya kuvuta pumzi akaendelea
“ Na anaekuangamiza na ku kuua ni Mchumba wako RAMLA”
“Ramla” kivipi aniue? Mbona sikuelewi?” nilishtushwa sana taarifa hii japo nilianza kuhisi kua huenda sasa huu ni muendelezo wa ile habari niliyopewa na Honde
“Tulia na unisikilize kwa umakini, Ramla hivi sasa anakusaliti, amepata mwanaume mwingine anaetoka nae kimapenzi, mtu huyo anaitwa Pablo Mwaki, ni kigogo mmoja maarufu tu na kwasasa wanataka kufunga ndoa”
“Unauhakika Ntahondi?”
“Mpaka nimekuja hapa mimi sio mwehu, mimi nasoma na Ramla na ni rafiki yangu wa karibu,
Lake langu na langu lake, kwa kifupi PABLO Ameshapewa taarifa zako kua wewe ndie mchumba
wake na Ramla hivyo yupo kwenye mchakato wa kukusaka, akukamate hata ikiwezekana akuteke ili wao wawe huru na mapenzi yao na ndoa yao bia ya bughudha ya mtu yeyote" Ntahondi alisimama
na kuniaga,
“Mimi naondoka, ila jitahidi kua makini na Ramla kwa usalama wako anaweza kutumiwa yeye ili wafanikishe mpango wao wa kukuteka”
“Aisee mbona kama nachanganyikiwa Ntahondi, yaani Ramla anaweza kufikia hatua hiyo?”
“Na kwa taarifa yako huyo Boss wako Mr Jimmy ni rafiki wa karibu sana na Pablo Mwaki na kwenye hiyo kampuni yenu Mwaki ana hisa zake, na pia ujue kua Mke wa Jimmy ambae ni mama yake mdogo na Ramla ndie aliemshawishi Ramla akuache wewe ili awe na Pablo hivyo inawezekana hata huyo Jimmy anaujua mchezo mzima nae kua nae makini” Wakati hu tunaongea habari hizo tulikua tumeshanyanyuka kwenye kiti na tunatembea kidogo kidogo mpaka mlangoni ambako tulikua tumesimama na baada ya maelezo hayo Ntahondi alifungua mlango na kuondoka zake, niliufunga mlango nikarudi mpaka kitandani, nikiwa natetemeka wa hofu na uoga wa hali ya juu ulionivaa mwilini
******
ITAENDELEA SIKU YA KESHO
:: Endelea ku LIKE PAGE YETU na ku COMMENT chombezo hili kali na lakusisimua.
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo ZITAKAZOFUATA
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment