ad

ad

RAY C AANZISHA KIPINDI CHA TV,KUANZA KUONEKANA HIVI KARIBUNI


STAA wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’ ameanzisha kipindi cha televisheni kiitwacho Pamoja Inawezekana ambacho kinatarajiwa kuanza kurushwa hivi karibuni,ambapo kuna picha ambazo msanii huyo amezipost kwenye mtandao akiwa na wasanii akiwafanyia interview. Kupitia Instagram Ray C aliandika hivi…Kipindi cha Pamoja Inawezekana kinaletwa kwenu na Ray C foundation na kitaanza rushwa kwenye TV zenu hivi karibuni. Kitakuwa na mambo mbalimbali
yanayohusu matatizo au athari za madawa ya kulevya,tutawatangazia hivi karibuni.ewe ndugu
 jamaa rafiki anayesumbuliwa na madawa ya kulevya usisite kuwasiliana na sisi Tutakusaidia kwa hali na Mali.
CREDIT: CLOUDS FM

No comments

Powered by Blogger.