CHOMBEZO: AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU....01
FACEBOOK
CHATTING

Na Nyemo
Chilongani.
Najisikia
nimechoka sana, nimechoka sana kwa sababu nilikuwa nimetoka kucheza mpira
uwanjani huku nikiwa nimechafuka kupita kawaida. Ninapofika nyumbani, ninaoga
na kisha kuchukua simu yangu kwa ajili ya kuangalia updates za facebook,
sikukuta hata meseji moja zaidi ya notification tu, tena wala hazikuwa nyingi.
Nilichokifanya ni kuanza kuzugazuga hapa na pale na kisha kutulia. Mara ghafla
nikaona namba moja nyekundu kwenye sehemu ya meseji, kulikuwa na meseji
imeingia, nilichokifanya, nikaifungua na kuanza kuchati na mtu huyo huyo.
EDUADO:
Mambo vipi Shahruk Khan.
MIMI: Hahahha!
Poa. Inakuwaje wewe mtu.
EDUADO:
Kama kawa. Nilikuwa nakusubiri sana hewani. Nilikuwa na mzuka na wewe ile mbaya.
MIMI: Duh!
Mzuka na mimi! Kuna nini tena?
EDUADO:
Kuna bonge la kazi hapa. Unataka?
MIMI: Kwa
nini nisitake? Nipe mawasiliano yao niandike barua ya kuomba kazi fasta.
EDUADO: Hahahaha!
Kaka unakosea. Niliposema kazi sikumaanisha hiyo.
MIMI: Wewe
ulimaanisha ipi sasa?
EDUADO:
Kazi moja hivi. Kazi ambayo watu wengi wameishindwa hasa masharobaro.
MIMI:
Hahahaha! Itakuwa kubeba zege hiyo watoto wa mama hawaiwezi. Mimi naiweza, hebu
niambie ni jengo gani.
EDUADO:
Sio kazi ya kubeba zege. Kuna mtu nataka umfanyie kazi.
MIMI: Mtu
gani?
EDUADO:
Kuna mrembo fulani nipo nae hapa UDSM ni mkali ile mbaya. Yaani mkali mpaka
nashindwa kusema ukali wake unafanana na nini.
MIMI: Hebu
acha masihala kaka. Kwa hiyo kama mkali mimi nifanyeje nini?
EDUADO:
Huyu mrembo anaringa mbaya. Yaani mrembo ananata utafikiri akanyagi ardhi hii
tunayochimbia vyoo.
MIMI: Ok!
Wazuri wapo wengi na hata wenye maringo wapo wengi pia. Hebu niambie kuhusu
huyo. Kwanza anaitwa nani. Nipe maelezo ya kujitosheleza na sio naanza
kumtengeneza mrembo mkali kichwani mwangu ikawa ndivyo sivyo.
EDUADO:
Huyu mrembo anaitwa Aziza Moody, anaishi Msasani, baba yake ni mfanyabiashara
mkubwa sana aisee. Ni mrembo fulani pini…yaani ni pini sana.
MIMI: Hebu
acha masihala. Sasa inakuwaje watoto wa kisharobaro wamemshindwa.
EDUADO:
Huyu mrembo hafagilii muonekano, ni mrembo fulani ambaye anapenda mtu anamfuate
kama jinsi alivyo. Yaani kama wewe ni mtu wa chini, mfuate hivyo hivyo ila
tatizo watoto wa hapa chuo wanapenda kumfuata kisharobaro kaka.
MIMI: Dah!
Kwa hiyo kazi unayotaka kunipa ni ipi?
EDUADO:
Umchukue huyu mtoto. Yaani ukifanikiwa, moyo wangu utakuwa mweupeeeeeee kama
theluji.
MIMI:
Hahaha! Usitake kunichekesha EDUADO, hivi unamkumbuka Sikitu?
EDUADO: Sikitu
yupi?
MIMI: Si
yule mrembo wa mwaka jana ambaye ulikuwa unamsifia sanaaaaa kwamba mkali kumbe
wala hakuwa mkali kama ulivyokuwa ukimsifia, mbaya zaidi alikuwa anakaa mbali,
Musomaaaaaa.
EDUADO:
Acha na hayo, yule msahau kwani mimi mwenyewe alinitumia picha ambayo sio yake.
Ila kaka kiukweli Aziza ni mrembo mmoja mkali sana. Hapa chuo amekuwa gumzo
kila kona, vijana wengi wamechemka.
MIMI: Sasa
kama wengine wamechemka mimi nitaweza vipi?
EDUADO:
Hahahaha! Kaka ninakuamini sanaaaa, wewe mtu unaweza sana kuongea, unaweza sana
kuandika. Endapo kazi nikakupa na kisha ukashindwa, haki ya Mungu nitajua kweli
duniani kuna wasichana wagumu.
MIMI: Kwa
hiyo kazi yako ina malipo au?
EDUADO:
Ikitokea umempata, nitakupa zawadi kaka. Yaani ninachokitaka huyu mrembo
umchukue tu, basiiiiiiii. Anaringa sana, ananata sana, yaani sijui niseme vipi.
MIMI: Ila
si anaringa kwa sababu mzuri?
EDUADO: Ndio.
Ila yeye kazidi.
MIMI: Ila
kwa sasa aisee nahisi nimepoteza kumbukumbu zangu za kuongea na hawa watoto wa
kike, sijui kama nitaweza.
EDUADO:
Acha kunitania kaka. Nakuamini sana kwamba unaweza kuliko mtu yeyote na ndio
maana nikakufuata wewe. Hivi haujiulizi kwa nini sikumfuata Thomas? Thomas
kwenye kuongea mkali sana ila kwenye kuandika hakuna kitu, ila wewe, aisee una
kipaji kila kona, nafikiri hata ukimtokea kiziwi, hachomoiiiiiiiiii.
MIMI:
Hahaha! Hebu acha kunipamba. Hebu niambie, huyo mrembo yupo Facebook?
EDUADO:
Amejaa teleeee…yaani kajaa teleeee. Anajiita Aziza M Aziza. Ni mrembo mkali
sana. Hebu mcheki kwanza.
MIMI:
Sawa.
Sikutaka
kuchelewa, tayari kichwa changu kikaanza kujazwa na sura nyingi za wasichana
wazuri huku nikianza kuzigawanya kimakundi kwamba huyu alikuwa Aziza mwenyewe
huyu hakuwa mwenyewe. Nilikuwa namfahamu EDUADO toka tupo katika shule ya
sekondari, alipokuwa akisema msichana fulani ni mzuri, mzuri kweli japokuwa kwa
Sikitu alikuwa ameniingiza choo cha kike. Sikutaka kuremba, mara baada ya kuona
majina kadhaa, nikamfuata Eduado inbox.
MIMI: Oyaa
Akshey.
EDUADO:
Vipi ushampata?
MIMI:
Wamekuja wakina Aziza wengi hao, mpaka wengine wanakaa India.
EDUADO: Hebu
subiri.
Sikujua
alikuwa akifanya nini, kwa sababu aliniambia kwamba nisubiri, wala sikuwa na
presha, nikamsubiri nione angeniambia kitu gani baada ya hapo. Nilimsubiri kwa
kipindi kama cha dakika moja hivi, akanijia tena inbox.
EDUADO:
Umeiona hiyo picha yenye mdoli wa Barbie?
MIMI: Yeah!
EDUADO:
Ndiye yeye huyo. Ibra huyo ni mrembo mkali ambaye sijawahi kuona.
MIMI: Acha
utani.
EDUADO:
Shua. Unamkumbuka Silvia tuliyesoma nae? Sasa Silvia haingii kwa Aziza.
MIMI: Acha
utani kaka. Silvia haingii?
EDUADO: Kweli
tena. Tena hagusi hata robo.
MIMI: Sasa
mbona hajaweka picha yake, nitamjua vipi kama ni mkali. Hebu nipe sifa kwanza
manake naona picha zake kazipiga pini watu wasio marafiki zake wasizione.
EDUADO: Kwanza
mrembo ni pini sana, mrembo kwao wana mahela ya kumwaga, chuo anakuja na gari,
Verrosa moja nyeusi, mtoto anamiliki laptop aina ya Apple ile inaayouzwa
milioni tatu, mtoto anamiliki anamiliki iPhone 5 huku akisema kwamba iPhone 6
ikianza kuuzwa atataka kuanza kuitumia kwani anapenda kwenda na wakati.
MIMI: Kaka
utakuwa unanitania tu.
EDUADO: Kweli tena. Halafu kuna cha zaidi.
MIMI:
Kipi?
EDUADO:
Otea.
MIMI: Hebu
niambie kipi?
EDUADO:
Ugonjwa wako.
MIMI:Unamaanisha
nini?
EDUADO:
Mtoto Mpemba.
MIMI: Hahahaha!
Kaka acha utani, utanifanya nimfuate sasa hivi.
EDUADO:
Ndio hivyo. Mtoto ni pini sana, pini ile iliyosimama.
MIMI:
Hahaha! Pini kama ya Blackberry vile.
EDUADO:
Acha kaka. Mtoto ni pini zaidi ya zile za Blackberry. Kwanza ukimuona tu, mtoto
utampenda. Mavazi yake sasa…weeeeeee.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
PATA NEWS NA SIMULIZI FASTA, LIKE PAGE YETU HAPA ==> 2JIACHIE
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
PATA NEWS NA SIMULIZI FASTA, LIKE PAGE YETU HAPA ==> 2JIACHIE
Post a Comment