WELBECK ANASWA AKIBANJUKA SAA TISA USIKU
MANCHESTER, England
SIKU chache baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, wachezaji wa Manchester United, Danny Welbeck na Tom Cleverley wamenaswa wakitoka kwenye mida ya starehe saa tisa usiku huku wakiwa na marafiki zao.
Wachezaji hao ambao timu yao imekuwa na mwenendo mbaya msimu huu, huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutolewa na Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, walionekana ‘wakijiachia’ huku wakiwa na furaha na kuimba nyimbo mbalimbali.
Picha zilizopigwa na watu waliowashuhudia usiku wa juzi, ziliwaonyesha Welbeck, 23, na Cleverley, 24, wakifurahia maisha huku wakiongozwa na marafiki zao ambapo kuna kipindi Welbeck alionekana kuvutana na mdada ambaye haikujulikana ni nani yake.
Man United ipo kwenye mapumziko ya siku 10 ambapo inajiandaa kukipiga dhidi ya Everton katika Premmier mnamo Aprili 20, mwaka huu.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment