CHELSEA YAKOMAA NA WABABE WA BARCA UGENINI, NGOMA DROO
CHELSEA
imelazimisha sare ya bila kufungana na Atletico Madrid katika Nusu
Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kamkia leo Uwanja wa Vicente Calderon
Maana
yake, Chelsea itahitaji ushindi mwembamba katika mchezo wa marudiano
Uwanja wa Stamford Bridge, London dhidi ya timu iliyoitoa Barcelona
katika Robo Fainali ili kutinga Fainali.
Chelsea
leo ilimpoteza kipa wake wa kwanza Petr Cech mapema dakika ya 17 baada
ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Schwarzer aliyemalizia vizuri
mchezo.

Post a Comment