AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU YA 07
Na Nyemo Chilongani.
BABA:
Kwani ukinywa kinywaji chochote utavimbiwa?
AZIZ:
Hapana. Nimekwishakunywa.
BABA: Ibra,
ni kweli anayoyasema?
MIMI:
Hapana. Hapo kakupiga fix.
AZIZA:
Hahaha!
BABA: Jisikie
huru. Uletewe kinywaji gani?
AZIZA: Maji
tu yanatosha.
MIMI: Ok!
Ila kuna maji ya chumvi...utakunywa?
AZIZA:
Mmmh! Maji ya chumvi?
MIMI: Sasa
unashangaa nini? Au haujui kama Dar es Salaam kuna bahari ya Indi?
AZIZA:
Niletee hata hayo nitakunywa tu.
Mtu mzima
nikanyanyuka, kumbuka hapo bado sikuanza kumtambulisha Aziza kwa mzee kwamba
alikuwa nani na alifuata nini nyumbani. Juu ya hilo, sikuwa na wasiwasi sana
kwani kwa umri ambao nilikuwa nimefikia, mzee hakuwa muongeaji sana zaidi ya
kunitaka kuwa makini kila siku kwa kila nikifanyacho. Nilipochukua maji, nikamletea,
tena kwa makusudi, nikamletea kwenye kikombe cha plastiki, nilichokuwa
nikikihitaji ni kumuonyeshea maisha fulani ya tofauti sana, maisha ambayo
alikuwa akiyaamini kichwani mwake kwamba yalikuwa yakiishiwa na watu waliokuwa
wakikaa Tandale uswahilini.
MIMI: Baba
huyu ni rafiki yangu anaitwa Judith. Nilisomanae Faraja Seminari ila nilimuacha
darasa moja. Kwa sasa yupo hapo I.F.M anasomea sheria.
BABA:
Asante kwa kumfahamu. Karibu Judith na jisikie huru.
AZIZA:
Asante.
MIMI:
Judith, huyu ndio mzee Akilimia. Huyu ndiye ambaye nimemuibia hiki kipaji cha
kuandikaandika.
AZIZA:
Nashukuru kumfahamu.
Kwa sababu
tulikuwa na safari, hatukutaka kukaa sana mahali hapo, tukasimama na kisha kuaga
na kuondoka. Njiani, Aziza alionekana kushangaa sana, hakuamini kama nilikuwa
na uhuru mkubwa wa kuongea na mzazi kwa kiasi kile.
AZIZA:
Mbona baba yako unaongea nae namna ile?
MIMI:
Kivipi?
AZIZA:
Ulivyokuwa ukiongea. Yaani kama unaongea na vijana wenzako.
MIMI:
Nisikilize Aziza, mzazi ni rafiki, hautakiwi kumuogopa sana mzazi mpaka kukosa
uhuru, wazazi wetu hawakutulea katika mazingira hayo, walitulea katika
mazingira ya kirafiki zaidi, mazingira ambayo yametufanya kuwa huru kwao.
AZIZA:
Basi hongereni. Mzee wangu ukae chini na kuongea nae namna ile, mh! Mtu
hujiamini. Kwanza akirudi tu, amani nakosa, muda wote utasikia Azizaaaa.
MIMI:
Hahaha! Ila hao wazee ndio fresh. Mzee unakuwa bandidu kama hivyo, hakuna
utani, hakuna masihala...hahaha!
AZIZA:
Kuna uzuri gani? Baba akirudi unajificha chooni. Ngoja nikuulize swali.
MIMI:
Uliza.
AZIZA: Kwa
nini umemdanganya jina langu na kila kitu kuhusu mimi?
MIMI: Pale
ningemwambia unaitwa Aziza, angeshtukia mchezo.
AZIZA: Kivipi?
MIMI:
Unajua nimesoma seminari, sasa niliposema kwamba nimesoma na wewe, kidogo
angetilia mashaka. Nilichokifanya ni kucheza na akili yake kabla ya yeye
kucheza na akili yangu, nikamuwahi. Hahaha!
AZIZA: Ibra
una visa sana.
Tuliendelea
kwenda mtaa wa juu, tulipofika, watu wengine bado walikuwa wakishangaa, wala
sikutaka kuwa na wasiwasi, kama kuuza tayari nilikuwa nimeuza sana,
nilichokifanya ni kushukuru kwa niaba yake kwa washikaji waliokuwa wakililinda
gari na kisha kuingia garini.
AZIZA:
Sasa hapa safari ni kwenda nyumbani. Unatakiwa kuwa huru, baba yangu ni mkali
sana ila kwa sasa hayupo. Jiamini, usiwe na wasiwasi. Umenisikia.
MIMI:
Ooopsss...nimekuelewa. Sasa kama akirudi ghafla?
AZIZA:
Usiwe na wasiwasi. Kila kitu kipo under control.
MIMI:
Mmmh! Aya bhana japokuwa huwa ninahofia sana kwenda nyumbani kwa mwanamke.
AZIZA:
Hahaha! Kwa nini unaogopa?
MIMI:
Unaweza kugeuzwa mwanamke....hahaha
AZIZA: Usijali
Ibra. Hakuna mtu anayeishi nyumbani ambaye ametokea Mombasa. Kuwa na amani.
MIMI: Aya
(Nilisema na Aziza kuwasha gari na kuondoka mahali hapo huku nikiwa nimezoa
maksi nyingi sana kwa kila aliyeniona na Aziza).
Ila pamoja
na hayo yote yaliyokuwa yakiendelea, nadhani sikutakiwa kwenda kwa kina Aziza.
Mungu ametufumba macho kutojua mambo yanayotokea mbele yetu, kama angetupa
uwezo, nadhani nisinge kwenda kwa kina Aziza kwani hali ilikuwa ni balaa
tofauti na uhakika ambao alikuwa amenipa.....chezea wazee wa kiarabu kwa
mabinti zao
MIMI:
Mmmh! Mbona mapigo ya moyo yananidunda hivi?
AZIZA:
Hahaha! Uoga wako tu. Au una BP?
MIMI:
Hapana. Yaani kama kuna jambo baya linakwenda kunitokea.
AZIZA:
Jambo gani na wakati nimekwishakwambia kwamba baba hayupo, nipo peke yangu.
MIMI: Na
mama je?
AZIZA: Nae
hayupo. Yaani kurudi kwao mpaka saa mbili usiku.
MIMI: Hapo
mwakemwake.
Kiukweli
nilikuwa na wasiwasi sana ila Aziza alijitahidi sana kuniondoa wasiwasi. Ngoja
nikwambie kitu kimoja, hakuna wazee ambao ninawaogopa kwa mabinti zao kama
wazee wa Kiarabu. Huwa hawataki utani kabisa, huwa hawataki ulete masihala kwa
mabinti zao hata mara moja.
Kukutoa
roho kwa sababu umemfuata binti yake wala haoni tatizo hata mara moja. Kwa
Aziza, akajitahidi sana kuniondoa wasiwasi lakini sikufichi rafiki yangu, hofu
bado ilikuwa ikiendelea moyoni mwangu.
Nikaona
haina noma, mzee wa Kiarabu angenitishaje mimi mtoto wa Tandale na wakati kama
fujo nimekwishazizoea? Mzee wa Kiarabu angenitishaje mtoto wa Tandale na wakati
kama ugomvi tushazoea ? Nilikuwa nikijipa moyo ila nilipofikiria kwamba wazee
wa Kiarabu walikuwa wakitumia hata bunduki kukudedisha, nikaona mweeeee...kazi
ipo.
AZIZA:
Tumekwishafika nyumbani. Karibu.
MIMI:
Asante.
Mlinzi
akafungua geti na kisha Aziza kuliingiza gari ndani. Nikabaki nikishangaa tu,
sikuamini kama hapa Tanzania kulikuwa na watu ambao walikuwa wakiishi katika
majumba makubwa kama ule mjengo aisee. Kulikuwa na bonge la bwawa la kuogelea,
bustani kubwa ya maua pamoja na sehemu ya kuegesha magari. Mazingira ya nyumba
yakanivutia sana, tukateremka na kisha kuanza kuangalia huku na kule, nilitaka
kuyazoea mazingira japokuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu.
AZIZA:
Mbona unaangalia hivyo.
MIMI:
Lazima niyazoee mazingira, naangalia vichochoro vya kufanyia uninja wangu mara
mzee wako atakapotokea ghafla.
AZIZA:
Acha hizo bwana. Mzee harudi sasa hivi, mpaka saa mbili usiku.
MIMI: Basi
hakuna noma. Kuna nani mwingine ndani ya nyumba?
AZIZA:
Mfanyakazi wa ndani. Wadogo zangu wote wapo shule nchini Kenya.
MIMI:
Hakuna noma.
Tukaingia
ndani na kisha kutulia. Macho yangu hayakutulia sehemu moja, yalikuwa
yakiangalia huku na kule kama mtu ambaye nilikuwa natafuta jambo fulani. Sebule
ilikuwa nzuri, ilivutia na kupendesha macho ya kila aliyekuwa akiiangalia.
Nikakaribishwa katika mkochi mmoja mkubwaaaa, ile kukaa tu, nikayahisi makalio
yakiingia ndani kabisa na kuzama kochini.
AZIZA:
Hapa ndipo nyumbani. Karibu
MIMI:
Asante
AZIZA:
Nikuletee nini?
MIMI:
Kwani kuna nini na nini?
AZIZA:
Kuna juisi, soda, maziwa na maji.
MIMI: Kwa
sababu nyumbani ni ngumu sana kunywa maziwa, hebu niletee maziwa.
AZIZA:
Hahaha! Aya. Kuna kingine unachokitaka?
MIMI: Kama
kuna vitafunio itakuwa full mzuka.
AZIZA:
Unataka vitafunio gani?
MIMI:Kwani
kuna nini na nini?
AZIZA:
Kuna keki, mandazi, baga, pizza, chapati
MIMI: Duh!
Utafikiri nimeingia hotelini. Fanya hivi. Kwa sababu sijawahi kula baga zaidi
ya kuisikia kwa watu, hebu niletee hiyo na kwa sababu nasikia sikia watu
wakitamba facebook sijui pizza tamu, nami niletee kwanza.
AZIZA:
Utamaliza vyote Ibra?
MIMI:
Kwani vikibaki si nitabeba! Au hairuhusiwi kubeba?
AZIZA:
Inaruhusiwa.
MIMI: Basi
niletee.
Usinishangae
aiseee, hivi ndivyo nilivyo na nilikwishazoea kuishi maisha ya namna hiyo.
Tandale hakukuwa na sehemu inayouza baga wala pizza, kwa hiyo kwa nini
nisiagize baga na pizza nami nitoe ushamba mdomoni mwangu? Nikaletewa vitu
nilivyovitaka, aiseee, kwanza nikajifanya kutokujua baga ipi pizza ipi,
ikanibidi niulize.
MIMI:
Pizza ipi na baga ipi?
AZIZA:
Pizza hiyo ya duara na baga ni huo mkate wenye vitu mbalimbali.
MIMI: Mweee...kazi
ipo. Nahisi leo nitaumwa sana tumbo.
AZIZA: Kwa
nini?
MIMI:
Tumbo langu halijazoea kula vitu hivi Aziza.
AZIZA:
Usiogope, vitu vya kawaida tu.
Nikaanza
kula buana, vilikuwa vitamu sana, tofauti na Aziza alivyofikiria kwamba
ningebakisha, haikuwa hivyo, nikala vyote na kushushia na maziwa. Muda wote
Aziza alikuwa akiniangalia, sijui alinionaje, sikutaka kujali, nilichokijali ni
kupiga msosi tu.
Hayo ndio
yalikuwa matukio ambayo niliyafanya mahali hapo, bado nilikuwa nikitaka
kumuonyeshea Aziza kwamba mimi nilikuwa mtoto wa uswahili. Najua wale
masharobaro wangeomba maji na pia kama wangeambiwa kuhusu chakula wangesema
wameshiba, ila kwangu mimi mtu nisiyekuwa sharobaro, hahaha! Nikaagiza vitu
ambavyo vilikuwa adimu kupatikana Tandale.
Nilichokuwa
nikikifanya ni kucheza na akili ya Aziza tu, unajua unapoona umekuwa na
msichana wa matawi ya juu halafu wewe unatoka uswahilini, usijifanye matawi
sana na wakati kwenu ni wababaishaji tu. Nilitaka kumtia kipofu Aziza,
nikajifanya sijawahi kula pizza na wakati mara nyingi nilikuwa nakwenda
kuzinunua Magomeni karibu na msikiti wa Kichangani. Nikajifanya kwamba hata
baga sijawahi kula na wakati nilikuwa nikipenda kuzinunua pale Kijitonyama
katika sheli ya mafuta karibu kabisa na jengo la TTCL. Aziza akaniona kwamba
kweli nilikuwa mtoto wa uswahilini
MIMI:
Nashukuru kwa chakula chako na kinywaji chako. Nadhani sasa ni wakati.
AZIZA:
Asante kwa kushukuru. Wakati gani?
MIMI: Wa
kuniambia kile ambacho kila siku nilikuwa nikikihitaji sana kwako.
AZIZA:
Kipi?
MIMI: Kuwa
msichana wangu wa dhati.
AZIZA: Hahaha!
Hausahau?
MIMI:
Nitasahau vipi na wakati ninakupenda. Then ukiona nakumbuka basi jua kwamba
wewe ni mtu muhimu sana kwangu. Kama usingekuwa muhimu, nisingekumbuka.
AZIZA: Hahaha!
Nisikilize Ibra, najua kwamba unanipenda ila...
MIMI: Ila
nini tena?
AZIZA:
Nahofia.
MIMI:
Unahofia nini?
AZIZA:
Kuwa na wewe. Naweza kufa kwa presha.
MIMI:
Haha! Hakuna kitu kama hicho. Nahitaji kuwa na wewe tu. Hebu fikiria muda wote
ambao nimeupoteza kwa ajili yako Aziza, umekuwa rafiki yangu mkubwa, rafiki
ambaye sikutaka kumpoteza katika maisha yangu yote.
AZIZA: Najua.
Tuendelee kuwa marafiki.
MIMI:
Nisikilize Aziza. Kila kitu kinakwenda na nyakati pamoja na mabadiliko. Najua
kabisa kwamba kabla ya baba yako kumuoa mama yako walikuwa marafiki, si ndio?
AZIZA: Ndio.
MIMI:
Baadae wakabadilika na kuwa wapenzi, si ndio?
AZIZA: Ndio.
MIMIl Na mwisho
kabisa wakawa mke na mume. Nimekosea?
AZIZA:
Haujakosea.
MIMI: Yeah!
Hayo ndio maisha yalivyo. Tumekuwa marafiki kwa kipindi kirefu, inatupasa
tubadilishe kila kitu kwa wakati huu, kutoka kwenye urafiki mpaka kuwa wapenzi,
tukitoka hapo, itatupasa tubadilike pia, tuje kuwa wachumba na hatimae mke na
mume.
AZIZA:
Mmmh! Ibra una malego ya mbali.
MIMI: Yeah!
Hayo ndio maisha yanavyotakiwa kuwa. Hatutakiwi kila siku tufikirie kuhusu hapa
tulipo, yatupasa tufikirie kule tutakapokuwa kesho. Ukiona mtu anafikiria zaidi
hapa, kidogo atakuwa na matatizo fulani kichwani.
AZIZA: Naomba
nikuulize swali. Unanipenda?
MIMI: Nadhani
macho yangu yanaelezea kila kitu. Siku zote mapenzi ya msichana huonekana
katika tabasamu lake ila mapenzi ya mvulana huonekana machoni mwake. Unaona
nini machoni mwangu?
AZIZA: Mapenzi.
MIMI: Yeah!
Hicho ndicho kitu kilichomo moyoni mwako juu yako. Nakupenda sana.
AZIZA: Najua.
MIMI: Naomba
kitu kimoja Aziza.
AZIZA:
Kitu gani?
MIMI: Lipsi
zako.
AZIZA:
Zimefanyaje?
MIMI:
Nataka kuona ni jinsi gani zilivyo laini.
MIMI:
Unamaanisha nini?
MIMI:
Haujajua namaanisha nini? Subiri.
Nikainuka
pale nilipokuwa na kisha kumsogelea. Lengo langu kubwa mahali hapo lilikuwa ni
moja tu, kubadilishana mate na kisha nione lipsi zake zilikuwa laini kiasi gani.
Hakuonekana kuwa mchoyo, akanipokea, huku lipsi zetu zikiwa zinatamaniana tu,
ghaflaaaaa....tukasikia honi ya gari getini. Kwa haraka sana Aziza akainuka na
kisha kuchungulia dirishani, geti lilipofunguliwa, alikuwa baba yake.
AZIZA:
Mungu wangu! Baba!
MIMI:
Unasemaje?
AZIZA:
Baba. Baba amerudi.
MIMI:
Amerudi (Nikainuka na kwenda kuchungulia dirishani, gari aina ya Range la baba
yake lilikuwa linaingia)
AZIZA:
Mungu wangu! Sijui nifanye nini.
MIMI: Wewe
si ulisema baba yako anarudi saa mbili usiku?
AZIZA:
Ndio. Sijui leo imekuwaje.
MIMI:
Mmmh! Hiki kifo (Nilijisemea moyoni huku nikitetemeka na haja ndogo ikitaka
kunitoka)
Aziza
alionekana kama kupigwa ganzi, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya
kwa wakati huo, nilimuona akianza kutetemeka huku kwa mbali kijasho chembamba
kikianza kumtoka. Hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali
pale.
:: Endelea ku LIKE PAGE YETU na ku COMMENT chombezo hili kali na lakusisimua.
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo hili kila litakapokuwa likitoka litakuwa katika wall yao. LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo hili kila litakapokuwa likitoka litakuwa katika wall yao. LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
ITAENDELEA JUMATATU

Post a Comment