AIRTEL "SMART PHONE" OFA PATA SAMSUNG S5 LEO
Ofisa
Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akionyesha simu aina ya Samsung S5
mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu
hiyo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data
bure.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa
ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja
na data bure.
Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa
Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha
kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya
Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure.
SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na
kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi
katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya
internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa
mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya
Samsaung S5”.
Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika
maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka
yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu za smart phones
yaliyoko nchi nzima.
Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde.

Post a Comment