TRENI YAPINDUKA NA KUUA HUKO GULWE MKOANI DODOMA
Wafanyakazi
walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye
kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika
stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili
wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital
ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu
ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali
iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea
saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na
kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari
na mafuta.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)
Post a Comment