ad

ad

Siri imefichuka,baada ya kikao cha siri cha Lissu na Mwigulu,UKAWA hatihati kumfukuza Lissu

Picha Mh.Mwigulu Nchemba na Tundu Lissu wakiwa wametoka kwenye kikao chao ofisini kwa Mwigulu Tarehe 25./03/2014 Saa 9:36 alasiri.
Katika hali inayonekana ni Gonjwa lile lile la anayepingana na Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA kubambikiwa Usaliti ama Kanunuliwa na CCM limeendelea Mjini Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Mwenyekiti wa CHADEMA na Wanaojiita UKAWA Mh.Freeman Mbowe na Wabunge wa CHADEMA wenye Mlengo wa Mbowe Wamevurugana na Mh.Tundu Antipas Lissu kwenye kikao cha Juzi na Jana baada ya Lissu Kupendekeza Wazo jema mbele ya Kikao cha UKAWA kwamba Wapinzani wamekuwa Wakisililizwa sana kuanzia Mchakato wa Katiba Uanze na mara kadhaa wamekutana na Rais kusikilizwa hoja zao na zimekuwa zikitendewa kazi..Vilevile tangu Bunge la Katiba lianze UKAWA wamekuwa wakisikilizwa sana kuanzia Mwenyekiti wa Muda Mh.Pandu Kificho ba sasa Mh.Sitta.

Lissu anasema Kwakuwa tumekuwa tukisikilizwa sana "TAKE" hivyo kwenye hili la Kura ya Siri acha na sisi turuhusu pendekezo lao la kura ya Wazi au Kuwe na Uhuru wa Kupiga Kura(Siri na Wazi Zitumike pamoja ilokuondoa mvutano huu bungeni).

Maneno hayo ya Kizalendo ya Mh.Tundu Lissu yalikuja baada ya Kikao cha Siri kati yake na Mh.Mwigulu Nchemba (Homeboys nje ya siasa),Lissu alikuwa na hoja kwa Mwigulu kuhusu Hotuba ya Rais ilivyoiweka pabaya Rasimu ya Warioba,ambapo Mwigulu alisema ulikuwa ni Wajibu kwa Rais kuwataarifu Watanzania kwa namna Uamzi wao kuhusu Katiba na Muundo wa Serikali unavyoweza Kuvunja Nchi au Kuimarisha Nchi.

Vilevile Mwigulu alihoji Kwanini Upinzani Wanaamini Mawazo yao ndio sahihi zaidi kuliko wengine?Hapo ndipo Wakafikia hatua ya kuridhiana kuwa katika hili la Kura Ukawa wakubariane na. kura ya Wazi au Mapendekezo yoyote yatakayotolewa na Kamati ya Kanuni.

Mnadhimu huyo wa Sheria Kambi ya Upinzani na Upande wa CHADEMA baada ya kujiridhisha na Maridhiano hayo akaamua Kuwapelekea UKAWA mbele ya Mbowe,Baada ya Kuwasilisha hayo Lissu aliipata Shubiri pale pale Kwa kuambiwa amenunuliwa na CCM,Mjumbe Mmoja kutoka 201 alisikika akisema Lissu kama amechoka Mapambano ajitoe UKAWA akaungane na CCM.

Mtafaruku Mkubwa Zaidi Umekuja Usiku wa Kuamkia leo baada ya Kauli ya Mh.Mwigulu Jana alipokuwa akichangia kusema "Kwanini Mnataka Kumfukuza Lissu Wakati amewambia mambo ya Msingi,mmezoa Ku-take,Mta Give lini?.

Hivyo hadi sasa,Mh:Tundu Lissu na UKAWA wapokwenye Mtafaruku Mkubwa Dodoma na Kunahatihati Lissu ama akafukuzwa au akajiondoka Kabisa Kwenye Umoja huo wa UKAWA uliochini ya Matakwa ya CUF na CHADEMA.

Mbali na hilo Wajumbe 201 Walioteuliwa na Rais Wapokwenye hatua za Mwisho za Kupeleka Ombi kwa Spika la Kumtaka Mbunge Wenje wa CHADEMA awaombe radhi Wajumbe hao,Pia Mbowe aweke bayana kuwa Wajumbe hao Wapo Dodoma kwa Maslahi ya Tanzania na Sio UKAWA wala CHADEMA.Hatua hiyo Imefikia baad ya Wabunge wa Chadema kudai 201 wanakula rushwa Dodoma na maprofesa Walioteuliwa na Rais hawana akili na hawajitambui.

Nawasilisha


No comments

Powered by Blogger.