SERIKALI YAIPONGEZA AIRTEL KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU JIJINI ARUSHA
Wanafunzi wa shule ya
Sekondari Naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara baada ya
kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela
aliwashukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura
na kusema kuwa licha ya kuwa ni jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa
shule lakini imekuwa ikizidiwa na majukumu mengi hivyo kwa msaada huo
Airtel wanapaswa kupongezwa kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa
msaada wa vitabu kwa Shule ya sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya
mpango wake maalumu wa “shule yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha
Bwana John Mongela alikuwa mgeni rasmi.
Bwana Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo
ya msingi ya kupata maarifa hivyo kwa Airtel kujikita katika kusaidia
jamii kupitia vitabu kwa shule za sekondari kutawawezesha wanafunzi na
jamii kupata hazina kubwa ya maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi
kupitia vitabu hivi.
Napongeza sana jitihada hizi na mpango huu
ambao ni endelevu na yenye kugusa shule nyingi na jamii kubwa ya
watanzania kwa ujumla”.Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini
Brightone Majwala akizungumzia msaada huo amesema mpango huo unaolenga
kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni yaani vitabu vya hisabati,physikia, chemia na biologia una lengo la
kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni, tunayofuraha kutoa
msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari Naura kwani tunaamini wanafunzi
wengi zaidi watanufaika na kuhamasika kujiunga na kusoma masomo ya
sayansi
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Gasper Mushobozi aliwashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu vya sayansi shuleni hapa , lakini alibainisha kuwa msaada huu pia uendelezwe kwa kutuboreshea maabara ya shuleni hapo ili kuweza kupata tecknologia ya sayansi kikamilifu.

Post a Comment