SIMBA SC YAIANGUSHIA KICHAPO CHA BAO 4-0 JKT OLJORO
Mshambuliaji wa Simba SC, Amissi Tambwe aliyetupia 'hat trick' dhidi ya JKT Oljoro.
TIMU ya Simba SC imeishushia kichapo cha bao 4-0 timu ya maafande ya
JKT Oljoro siku ya jana katika mtanannge uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Amissi Tambwe aliyetupia 'hat trick' wakati lingine likifungwa na Jonas Mkude.
Kwa matokeo ya siku ya jana Simba imefikisha pointi 30 baada ya kucheza michezo 15 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara.
KIKOSI SIMBA KILICHOPELEKA KILIO KWA MAAFANDE WA JKT OLJORO:
Ivo Mapunda, William Lucian, Baba Ubaya, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadhi Juma, Amri Kiemba, Amissi Tambwe na Ramadhan Singano 'Messi'.
Post a Comment