BARCA YAKALISHWA NA VALENCIA, MESSI NDANI
REKODI ya kutofungwa ya Barcelona usiku huu imekomea kwenye mechi ya 31, baada ya kufungwa mabao 3-2 na Valencia.
Mabao
ya Barca yalifungwa na Alexis dakika ya saba na Messi kwa penalti
dakika ya 51, wakati mabao ya Valencia yalifungwa na Parejo dakika ya
44, Piatti dakika ya 46 na Alcacer dakika ya 58.
Kocha
wa Manchester City, Manuel Pellegrini bila shaka aliuangalia mchezo huo
kabla ya timu hizo kukutana Februaryi 18 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matokeo
hayo yanatoa nafasi kwa Barca kuipisha Real Madrid kileleni, kwani
inabaki na pointi zake 54 sawa na Atletico Madrid, ikiwa imecheza mechi
moja zaidi. Real ina pointi 53 na imecheza mechi 21, wakati Barca 22.


Post a Comment