Loga: Nitasajili Wakenya, Wabongo ni tabu
KOCHA Mkuu wa Simba, Mcrotia Zdravko Logarusic,
amesema iwapo ataendelea kukinoa kikosi hicho msimu ujao, ndoto ya
usajili wake ni kuchota nyota kutoka Ligi Kuu ya Kenya, kwani kuna
wachezaji wenye uwezo mzuri na wenye kuendana na weledi wa kisoka
(professionalism).
Loga ambaye aliwahi kufundisha soka nchini humo akiwa na Klabu ya Gor
Mahia, alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya soka lakini
hawana weledi, ndiyo maana wanampa tabu kufundisha.
Alienda mbali na
kusema kuwa katika kipindi alichokaa Tanzania, hajaona mchezaji mwenye
uwezo wa kucheza ligi kubwa hasa Ulaya kulinganisha na Wakenya
waliosambaa kila kona ya dunia.
“Wachezaji wa Kenya ni waelevu, wanaelewa nini kocha anachotaka
tofauti na hapa. Ndiyo, Tanzania kuna vipaji, lakini wachezaji wake siyo
welevu, ndiyo maana wananisumbua hata katika ufundishaji.
“Kama kweli nitakuwa hapa msimu ujao, nitaleta wengine kutoka kule,” alisema Loga huku akiisifia Gor Mahia kuwa ina wachezaji wazuri.
“Kama kweli nitakuwa hapa msimu ujao, nitaleta wengine kutoka kule,” alisema Loga huku akiisifia Gor Mahia kuwa ina wachezaji wazuri.
Loga ambaye mkataba wake unakwisha Mei, mwaka huu, baada ya kufika
Simba aliwasajili Ivo Mapunda ambaye ni Mtanzania aliyekuwa akicheza
soka Kenya na beki Mkenya Donald Musoti.
Post a Comment