Beki Ruvu: Okwi ndo nani, mbona wa kawaida tu?
NAHODHA wa Ruvu Shooting, Michael Pius, ameibuka na kusema nyota wa Yanga, Emmanuel Okwi, si lolote kwani wamekutana mara kadhaa na amekuwa akimchukulia mtu wa kawaida kama wachezaji wengine wa Yanga.
Timu hizo zitakutana wikiendi hii katika michuano ya Ligi Kuu Bara, ambapo Pius ambaye hucheza beki wa kulia, amesema Okwi asitarajie mteremko kwake iwapo Yanga wataamua kumtumia.
“Mbona Okwi mchezaji wa kawaida? Sema tu ninyi waandishi wa habari ndiyo mnakuza watu ili waonekane mastaa, lakini kwangu si lolote.
“Tumekutana mara nyingi sana tangu akiwa Simba, tukakutana tena kule Kenya (katika michuano ya Chalenji), sijaona umaarufu wake kama mnavyompamba.
“Hata Jumamosi, siamini kama atapata nafasi ya kutusumbua, kama unafikiria jambo hilo, labda asicheze,” alisema Pius.

Post a Comment